Elections 2015 Jimbo La Bukoba mjini mmefanya makosa makubwa kumuondoa Sued Kagasheki

Ambulensi Hajanyang'anya, Watu Wahongo, Kafuta Neno IMETOLEWA NA MBUNGE WA BUKOBA MJINI, KAWEKA IMETOLEWA NA KHAMIS KAGASHEKI

Nasema hivi hiyo AMBULANCE haijarudishwa Hospital, imepaki Kasibante Radio!!!
 

inawezekana hayo hayakuwa vipaumbele vya wapiga kura wake, wao walitaka mabadiliko ya kuzungusha mikono na wamepata, alipaswa awape kazi twaweza na repoa wamfanyie research ili ajue priorities za wananchi wake. Isitoshe watu wa kagera ni wa ajabu sana kama walimshangilia Idd Amin huku wamebeba majani ya migomba pamoja na kuwapiga risasi.
 
hakuna mji wenye unafiki kama ule Tanzania hii...we jua hivyo tu...ila vicfish ni yake kweli?..mi najua anamiliki ASU ambapo pia kuna ajira za kutosha...wataona mabadiliko.
 
Hakika watu wa Bukoba na Kagera kwa ujumla miaka yote wamesifika kwa ujasiri wa kujitegemea, ujasiliamali na kusaka elimu. Kwa historia yao iliyotukuka wana Bukoba wanahitaji kuwezeshwa kimiundombinu na kimitaji ili waweze kuinua maisha yao. Mbunge au kiongozi wa aina ya Kagasheki anayejikita katika uhisani wa wateule wachache hafai. Mbunge na wote wenye madaraka wanahitaji kuelekeza nguvu kwenye miradi mikubwa na endelevu yenye kugusa maisha ya maelfu ya wenyeji waliopigika kiuchumi na sasa kielimu.

Bukoba tunahitaji SOKO jipya na la kisasa ili kuwawezesha maelfu ya wauzaji na wanunuzi kuendesha shughuli zao kwa ufanisi na tija. Zile chokochoko baina ya Kagasheki na mtu wake Aman zilizosababisha kushindwa kwa mradi huu ni sababu tosha ya kumkosesha ubunge Kagasheki. Bukoba tunahitaji stendi mpya na ya kisasa ya mabasi. Wana Bukoba na Kagera tunahitaji usafiri wa meli wa uhakika zaidi ya miaka 15 tangu tuwapoteze ndugu zetu zaidi ya 800 kutokana na matumizi wa meli mbovu.
Mwisho Kagera tunahitaji Chuo Kikuu kikubwa na cha hadhi ya kimataifa - siyo matawi ya vyuo vya makanisa vya SAUT na TUMAINI. Kwa mkoa wenye zaidi ya wakazi millioni mbili na historia ya wenyeji wapenda elimu (nshomile) ni aibu kuzidiwa sana na mikoa ya Morogoro na Kilimanjaro yenye vyuo vikuu zaidi ya vitatu vyenye hadhi ya kimataifa. Wabunge wetu wapya walete mabadiriko katika maeneo haya na siyo kuleta bodaboda na ambulance ambalo ni jukumu la serikali.
 
Wewe ndio umemaliza, mambo yote aliyoongea huyu ni ya hisani, hatuwezi kuwa na wabunge wa aina ya Dewji, miaka 5 hajawakilisha wananchi mara anachimba kisima hapa na pale.

Sisi wabunge maskini tutawezaje kufanya kazi za serikali?

Kweli kabisa mkuu na yote haya ni kuishi chini ya mfumo mbovu wa watawala wetu ambao wanawadanganya wananchi eti kazi ya mbunge ni kuchimba visima au kujenga mitalo na kuiacha serikali ikitumia kodi kwa anasa
 
Hiyo misaada inatolewa na WAHISANI na si yeye acheni kutudanganya. WANABUKOBA WAMEGUNDUA KUA ANACHOWAPA SIO ANACHOPOKEA.
 

Said Kagasheki ndio nani aisee
 
Kweli kabisa mkuu na yote haya ni kuishi chini ya mfumo mbovu wa watawala wetu ambao wanawadanganya wananchi eti kazi ya mbunge ni kuchimba visima au kujenga mitalo na kuiacha serikali ikitumia kodi kwa anasa

Sijui kama watakuelewa
 
kwahiyo unahisi hizo ndio kazi na majukumu ya mbunge?
 
Britanicca hayo ni mahaba kwa Kagasheki. Kafanya mambo mazuri, well and good. Amuachie kijiti mwingine aendeleze kwa viwango vya juu zaidi.
 
Word. Well said

 
Angekuwa kwel anayafanya hayo yote sizan kama raia wangempiga chin!!

Vip mbona ambulace kazikusanya tena?
 
Kama haya yote alikuwa anatoa kwenye mfuko wake mwenyewe, basi hafai hata kidogo. Uwepo wa viongozi wa namna hii unaifanya serikali inayokusanya kodi zetu ilale saaana na kuwafanya wachache kuiibia serikali. Kazi ya mbunge sio kugawa haya mavitu, ni kuwawakilisha raia na kuisimamia serikali. Sasa huduma ambayo ilipaswa itolewa na serikali inatolewa na mbuge (sijui kwa raha ipi), basi mbunge ndiye serikali na endapo atakula fedha za umma ni vigumu kumuwajibisha maana anavokwimba katika eneo moja anavileta kwa mkono mwingine. Hii sio kwa kagasheki tu, nadhani raia nchi hii wanadhani mbunge anawajibika kuleta maji, kujenga barabara badala ya KUISIMAMIA serikali ifanye hayo na mengine zaidi ya hayo. Sasa Bukoba mjini, wambane mbunge wao mteule ahakikishe anaibana serikali inavileta hivyo vitu badala ya kumtegemea binadamu. Obama anasema Africa needs strong institutions not individuals!!!!!!!
 
Ambulance huko kwenu Bkb nilisoma mahala kuwa kashaichukua na kuondoa yaliyokuwa yameandikwa...kumbuka ilikuwa ya msaada walivyosema.
 
Kwanini Sasa Aendelee Kutoa Misaada Kwa Wanafiki,

Kwani hana kazi ingine ya kufanya? Ubunge sio yeye tu ndio maana kuna uchaguzi.

Akachunge ng'ombe, kumbuka aliachishwa kazi kiongozi gani anasimamishwa kazi.

Pole mwana familia, lazima na wewe ulikuwa unakula vya wananchi kichinichini na kijuu juu.
 

Umenena misaada ya watu wema ulivyoandika ma mleta mada ni misaada alinebea jina lake.

Si ni mhaya au aliamia bkb?

Nilikuwa simjui hadi alipofukuzwa kazi ndio nikayajua ya Bukoba kuwa napo wapo wapenda vyeo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…