Jimbo la Kigamboni lipo wazi, hongera Ndugulile

evangelical

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2011
Posts
5,035
Reaction score
8,218
Baada ya Dr. Faustine Engelbert Ndugulile kuchaguliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Dunia (WHO) hapo jana jimbo la Kigamboni ambalo alikuwa anahudumu yeye kama mbunge lipo wazi kwani kwa kuchaguliwa katika nafasi hiyo hastahili kuendelea na majukuhu hayo ya kisiasa.

1724824494628.jpeg

Pia soma: Dkt Faustine Ndugulile ashinda kinyang'anyiro cha ukurugenzi Mkuu wa WHO kanda ya Afrika
 
Kigezo cha Msigwa ajitupe huko agombee, halafu aone kama hata hio kura yake ataiona Imepitia wapi halafu apite kwenye majukwaa kumlaumu Mbowe kwa kumfanya asishinde jimbo la Kigamboni kwa chama chake kipya. Maana mbowe sijiui kamfanya nini
 
aingie katika kinyanganyiro kura za maoni halafu ajipime ndani ya CCM kabla ya uchgauzi mkuu 2025.
Hii itamsaidia sana katika harakati za kisiasa akiwa na chama kipya
 
Msigwa mwambie jimbo liko wazi aingie kura za maoni, ili apate kumsingizia Mbowe
 
Baada ya Dr. Faustine Engelbert Ndugulile kuchaguliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Dunia (WHO) hapo jana jimbo la Kigamboni ambalo alikuwa anahudumu yeye kama mbunge lipo wazi kwani kwa kuchaguliwa katika nafasi hiyo hastahili kuendelea na majukuhu hayo ya kisiasa.

Pia soma: Dkt Faustine Ndugulile ashinda kinyang'anyiro cha ukurugenzi Mkuu wa WHO kanda ya Afrika
Ni kweli jimbo liko wazi ila kwa mujibu wa katiba yetu, jimbo likiwa wazi chini ya miezi 12 kabla ya kuvunjwa Bunge, hakutafanyika uchaguzi mdogo wowote.

Ibara ya 49 (5) ya Sheria Mpya ya Uchaguzi inasema (5) Endapo uchaguzi mdogo unatakiwakufanyika na tarehe ya kuvunjwa kwa Bungeimetangazwa au imejulikana kwa mujibu wa matukioyaliyoainishwa katika Ibara ya 90(3) ya Katiba,uchaguzi mdogo hautafanyika katika muda wowotewakati wa kipindi cha miezi kumi na mbili mara tubaada ya tarehe ya kuvunjwa kwa Bunge.

Ndio maana pia nimewashauri hata wale rafiki zangu wenye wivu wa kike kuwaonea vivu wale wanawake mashujaa 19, waachane nao tuu, kwasababu hakuna uchaguzi wowote au uteuzi isipokuwa kwa nafasi za Rais tuu!. Ushauri wa bure: CHADEMA iachane na issue ya Wabunge wake 19, iwasamehe waendelee na Ubunge wao. Kwa muda uliobakia kuwatengua hakuna maslahi yoyote!

P
 
Inabidi kipengele cha kufanya replacement ya mbunge wa jimbo kiangaliwe vizuri kwani hao wananchi watakosa mwakilishi bungeni .
Kiwekwe kipengele kwamba ikitokea mbunge wa jimbo amejiudhulu mwenyewe anayefuatia kwa kura za maoni ateuliwe kumalizia kipindi kilichobaki. Ila ikitokea amefariki ndio uchaguzi ufanyike
 
Back
Top Bottom