Uchaguzi 2020 Jimbo la Kigamboni - Mipango na mikakati ya kuchukua Jimbo

Uchaguzi 2020 Jimbo la Kigamboni - Mipango na mikakati ya kuchukua Jimbo

Nashukru mkuu kwa kunisaidia kuandika manifesto ya ubunge, haya yote uliyoandika na yale ya kwangu nitaenda kuyatekeleza! Ingawaje umechemka kwenye muda wa ubunge, yaani tukae miaka 15 wenzetu wanatusubiri tu?
 
Jimbo la Kigamboni ni moja kati ya majimbo ya uchaguzi katika jiji la Dar es Salaam

Kama mmoja wa watia nia katika Jimbo hili ninakusudia kuchukua FOMU ya kugombea Ubunge katika Jimbo Hili

Zifuatazo ni baadhi ya sera:

MUHTASARI WA SERA NA MALENGO YA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KIGAMBONI
Moja kati ya sababu zilizonisukuma kutia nia hii ya kugombea Ubunge katika jimbo la Kigamboni ni pamoja na hamu yangu ya kutaka kuona mabadiliko ya kijamii na kiuchumi katika Jimbo hili na katika taifa kwa ujumla.
Kati ya mambo ambayo ninalenga kuyasimamia katika kipindi changu cha utumishi ni pamoja na haya yafuatayo:

AFYA
  • Kwanza ni uanzishwaji wa huduma ya Universal Health Insurance BIMA YA AFYA KWA WOTE ambayo itakuwa subsidized (kupewa ruzuku) na serikali kwa wananchi wote.Lengo langu ni kuhakikisha kwamba wananchi wote wanakuwa na Access ya Huduma ya Afya ya Msingi-Basic Health Service ambayo ni subsidized na Serikali.
  • Ili kuonesha msisitizo nitafanya Mpango wa Majaribio Jimboni kwa ajili ya kuwafikishia Wakazi wa Kigamboni hasa Watoto huduma hio kwa Mfumo wa subsidy.Nimepanga na ninaahidi kutumia sehemu ya Mapato yangu ya kibunge pamoja na michango ya wahisani katika kufanya Jambo hilo katika Jimbo la Kigamboni
ELIMU
  • Pili ni uanzishwaji wa huduma ya elimu kwa wote EDUCATION FOR ALL(EFA) ambapo wanafunzi wote katika ngazi yoyote ya ELIMU katika shule binafsi na serikali watapata elimu kwa gharama za serikali. Katika hili ninapendekeza kuwepo kwa subsidies kwa shule Binafsi za msingi na sekondari.Mfumo huu wa subsidy utakuwa ni pro rata na utalenga zaidi zile Gharama za Msingi za kuendesha shule-(Basic Costs).
  • Pia nitapendekeza mabadiliko katika Mfumo wa Mkopo wa Elimu ya Juu hasa katika swala Means testing-Swala hili lihusike tu katika fedha za kujikimu badala ya kuhusika katika Ada na Malipo ya Chuo.Ada za chuo ziwe Covered kwa 100% kwa wanufaika wote katika Msingi wa Merit(Kiwango cha Ufaulu na Kozi anayosoma Mtu)
  • Nitasimamia kwa ukaribu ujenzi wa madarasa na madawati na kuhakikisha kwamba walimu wanakuwa na motisha na vitendea kazi katika kutoa elimu kwa watoto wetu.
  • Tatu ni kuboresha utoaji wa elimu katika shule za sekondari kwa kuhakikisha kwamba shule zote katika wilaya ya Kigamboni zinakuwa na Maabara za Computer pamoja na Maktaba.Katika hili nimedhamiria kutenga sehemu ya mapato yangu ya Kibunge na pia kuhamasisha michango ya wadau.
KODI NA TOZO
  • Nne ni katika suala la kodi ambapo nitapendekeza kupunguzwa kwa kiwango cha VAT kutoka 18% mpaka 13% kama mkakati wa kusisimua shuguli za kiuchumi na kupunguza gharama za maisha.Hii itasaidia sana kuongeza uwekezaji hasa kutokana na kuzorota kwa uchumi katika kipindi hiki cha changamoto za Corona.
  • Nitasimamia mabadiliko ya ukusanyaji wa Mapato katika halmashauri kwa kuleta mfumo wa SERVICE BASED TAXES ambapo badala tu ya watu kuchukua Leseni kunakuwa na mfumo wa elimu endelevu/mafunzo kabla ya kupewa leseni.Lengo ni kuhakikisha Wananchi wanakuwa na elimu ya biashara ili kupunguza kufa kwa biashara ndogo ndogo.
MRADI WA MJI WA KISASA WA KIGAMBONI
  • •Nitafuatilia kwa ukaribu sana kuhusu suala la Mradi wa Ujenzi wa Mji wa Kisasa wa Kigamboni ili kwa kuzingatia sababu za kukwama tuweze kufufua ndoto hio ya kuwa na mji wa kisasa wenye miundo mbinu mizuri na maisha bora kwa watu.
  • Nitafuatilia kwa ukaribu miradi mikubwa ya wawekezaji naya serikali iliyokwama ili kutafuta suluhu na kuhakikisha inakamilika
ARDHI
  • Nitafuatilia kwa ukaribu suala la Migogoro ya ardhi kwa kuzingatia mpango wa matumizi bora ya ardhi na haki kwa wote ili kuhakikisha kwamba watu wote wanaomiliki ardhi inakuwa na tija na kutumika katika kuleta maendeleo.
  • Tutahamisha utoaji wa hati za ardhi ili kuwezesha wananchi kutumia hati zao kupata mikopo katika taasisi za fedha
USIMAMIZI WA MIRADI•
  • Nitafuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoendeshwa katika halmashauri na kuhakikisha kwamba inafanyika katika ubora unaostahili na kwa thamni ya pesa na kwa wakati.
HUDUMA KATIKA OFISI YA MBUNGE
  • Nitaweka mfumo mzuri katika ofisi ya Mbunge kwa kushirikiana na Watumishi wengine.wa serikali katika kushughulikia kero za wananchi kwa kuzingatia misingi ya huduma bora kwa raia,uwazi na usawa.Wanawake,Walemavu na watu wenye mahitaji maalum watapewa huduma rafiki.
RUSHWA
  • •Nitahamisisha vita dhidi ya Rushwa na uonevu katika halmashauri kwa kuweka mifumo rafiki ya utoaji huduma na utoaji taarifa.Hii itaenda sambamba na kuondosha ukiritimba na uzembe katika utumishi wa umma na kuhamasisha dhana ya uwajibikaji
UWEKEZAJI NA BIASHARA
  • Nitasimamia uanzishwaji wa Club ya wawekezaji katika wilaya ya Kigamboni ili kuwawezesha wawekezaji wakubwa kupata huduma rafiki kwa wawekezaji huku wakishiriki katika shughuli za kijamii pamoja na wakazi a Kigamboni.
  • Vile vile nitafuatilia uanzishwaji wa SOKO KUU LA KISASA pamoja na STAND YA MABASI ya kisasa kwa ajili ya Wakazi wa Kigamboni katika kuhamasisha Shughuli za uzalishaji mali na biashara.
MAENDELEO ENDELEVU
  • •Kuanzisha Mpango Mkakati wa kuhamasisha maendeleo endelevu(Sustainable Development) na uhifadhi wa mazingira kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa maendeleo wilaya ya Kigamboni.
UKOMO WA MUDA WA UBUNGE
  • Nitawakilisha Bungeni mapendekezo ya Ukomo wa muda wa utumishi wa Bunge ambapo,Mbunge atahudumu kwa muhula mmoja hadi mitatu inayofuatana iwapo atapata ridhaa ya wananchi.Pia nitapendekeza kwamba wabunge ambao walipwe mafao yao ya kumaliza ubunge pale tu ambapo ama hawana nia ya Kuongeza muhula mwingine au pale wanapotimiza mihula mitatu kwa mujibu wa sheria.
  • Kiwango cha kinua mgongo cha wabunge kikokotolewa kwa kuzingatia Muda wa Ubunge na hali ya uchumi kwa kuzingatia kiwango cha makusanyo ya kodi na hali ya uchumi.
URAIA PACHA NA UHAMIAJI
  • Nitapendekeza marekebisho ya sheria ya uraia ili kuruhusu uraia Pacha.Hii itasaidai kuhamasisha ushiriki wa Watanzania wa ughaibuni kuweza kushiriki katika ujenzi wa taifa na kuhamasisha uwekezaji kutoka nje ya nchi.
NAFASI NA MAJUKUMU YA BARAZA LA MAWAZIRI
  • •Nitawakilisha Bungeni Mapendekezo ya marekebisho ya sheria ambapo Nafasi ya mawaziri katika baraza la mawaziri yasiwe kwa ajili ya kuwajibika kwa Rais bali yawajibike kwa Wabunge.Baraza la Mawaziri liteuliwe na Waziri Mkuu kwa kushauriana na Mheshimiwa Rais kuhusu Mahitaji.Rais atakuwa Mkuu wa UTUMISHI WA UMMA na Baraza la Mawaziri litawajibika kwa Waziri Mkuu na Bunge.Watumishi wengine wa Umma kama vile,Makatibu wakuu wa wizara,Wakuu wa Mikoa na Wilaya ndio watateuliwa na Rais.
  • Uamuzi wa idadi ya Wizara utafanywa na Rais ila uamuzi wa uteuzi utafanywa na waziri mkuu na kupitishwa na Bunge kwa kuzingatia Mfumo wa Mchujo wa Kibunge katika kamati husika kwa ajili ya vetting.•
  • Nitawakilisha Mapendekezo ya Marekebisho ya sheria kuhusu muundao na mfumo wa uendesha wa Baraza la Mawaziri-cabinet ambapo,Makatibu wakuu wa Wizara watakuwa Wajumbe wa Baraza la Mawaziri-Kama Wataalamu,Mawaziri watakuwa kama wabunge na Judge Mkuu wa Mahakama atahudhuria kama Mtazamaji.Maamuzi katika baraza la mawaziri yatafanyia kwa KURA ambayo itapigwa na Mawaziri TU.Mambo yatakayofanyiwa uamuzi katika Baraza la mawaziri ni mambo ya kiutendaji tu ikiwamo mambo ya SERA,Mipango na utekelezaji
  • Lengo la mabadiliko haya ni kuhakikisha kwamba tunajenga Jamii iliyo huru na yenye Usawa na haki.
Vipaumbele hivi ni vile nitakavyoanza kufanyia kazi katika siku zangu 100 za mwanzo za ubunge.Vile vile nitashughulikia na kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa wadau na wananchi kwa ujumla katika kuhakikisha Kigamboni inakuwa na Maendeleo.

Ofisi yangu ya Kibunge itakuwa na Idara madhubuti kwa ajili ya kushughulikia kero za wananchi,wafanyabiashara na wadau wengine katika kuhakikisha taifa linasonga mbele. Nitalifanya Jimbo la Kigamboni liwe jimbo la kisasa la kupigwa mfano katika uendeshaji wa shughuli za kiserikali na kuwapa wananchi maisha bora.

Pia ninapokea maoni na ushauri kuhusu masuala ambayo yanapswa kuzungumziwa zaidi katika kipindi uchaguzi huu.Iwapo nitafika katika hatua ya kuwa mgombea kamili,nitakutumia nakala kamili ya SERA,MIPANGO,MALENGO na Ahadi zangu kwa wakazi wenzangu wa Kigamboni katika kuleta maendeleo ya Taifa Letu.

Tuungane Mkono Katika hili

Iwapo unapenda kuwa sehemu ya safari hii tafadhali tuwasiliane PM. Sifa uwe ni mkazi wa Kigamboni, Mwenye Umri wa Kupiga Kura na ambaye una uwezo wa kushawishi na kuhamasisha wananchi katika uchaguzi.

Tafadhali PM kwa mawasiliano zaidi.
Naomna nikuulize upande wa Elimu:
..
Umesema mpango mkakati wako ni kutoa Elimu kwa wote watalipiwa na Serikali kwa shule za Binafsi na Serikali.

Swali:
1. Unafahamu kuwa Tanzania hii kuna shule binafsi amabzo ada ni Zaidi ya Milioni 75@ Mwaka kwa mtoto wa Form 1? Rejea Int. School of Tanganyika (Gharama ya mwanafunzi mmoja ni sawa na kulipia wnfnz 1000 wa serikali kwa mwaka.

2. Je hiyo serikali unayosema imekupa assurance hiyo ya kuwalipia hao wanafunzi?

3. Je ipo kwenye sera na ilani ya CCM? Maana chama chako hakiwezi unda serikali
 
Nashukru mkuu kwa kunisaidia kuandika manifesto ya ubunge, haya yote uliyoandika na yale ya kwangu nitaenda kuyatekeleza! Ingawaje umechemka kwenye muda wa ubunge, yaani tukae miaka 15 wenzetu wanatusubiri tu?
miaka 15 ni terms kwa kutegemea ridhaa ya wananchi ila baada ya hapo huruhusiwa kugombea
 
Nipo hapa mkazi wa Kigamboni, ila naona matatizo yetu mengi hujaainisha
Matatizo ya Kigamboni ambayo tayari yapo kwenye mipnago ni kama ifuatavyo:

  1. Issue ya maji hasa Tayari iko kwenye sera
  2. Issue ya Access roads za Public Beaches tayari iko kwenye sera
  3. Issue ya uhaba wa madawati kwenye shule tayari iko kwenye sera
  4. Issue ya Barabara ya kutoka Mji Mwema-Tungi na Barabara ya Dege-Mbutu,Barabara ya Kibada-Kisarawe 2,hizo tayari ziko kwenye sera
  5. Vile vile Tunaendelea kupita kwenye KATA na MITAA kufuatilia KERO na CHANGAMOTO ZA WANANCHI MBALIMBALI
 
Kitu kidogo kama utamhulisho wako umeweka Fake Id, Itakuwaje ahadi zako?
Naona umeshindwa hata kabla ya kutangaza nia!
Mkuu behold Sijaficha utambulisho wangu,Nimeleta mjadala wa sera kwanza.Ikifika Wakati wa kujitambulisha nitaleta Verified ID hapa.
 
Small Mind,
Mambo mengi uliyoyabainisha hutaweza kuyafanya maana ni nje ya mandate ya ubunge.

Isipokuwa sema utaishawishi serikali itakayokuwa imechukua dola kufanya mambo hayo mazuri kuhusu Maendeleo ya Watu.
 
Mkuu,Hilo neno sitaweza nalikataa,Ilo la kushawishi ndio hatua ya kwanza ya utekelezaji.Political ambition yangu sio tu kuwa Mbunge bali ni kuleta mabadiliko ya kimfumo kupitia vuguvugu la mabadiliko litakaloongozwa na wananchi.Ninaenda Bungeni kwa ajili ya kutengeneza jukwaa tu.Ndio maana ukiangalia sera zangu utaona kabisa hazilengi tu kujenga mazingira mazuri kwa wakazi wa Kigamboni bali ni kutengeneza mfumo ambao unaweza kutumiaka katika jimbo lolote kuleta mabadiliko

Kwa sasa hivi niko natafuta wagombea udiwani makini ambao watakuwa tayari kushika na kuliendesha jimbo la kigamboni.Ninafasi ya kugombea uongozi ambayo Mgombea hatakuwa na gharama kubwa za kampeni wala hatatoa rushwa bali atashinda kwa kutumia mtaji wa watu wanaotaka mabadiliko.LENGO LANGU NI KUANZISHA MOVEMENT YA MAENDELEO AMBAYO ITATIKISA KABISA MISINGI YA MIFUMO ILIYOPO.
 
RUSHWA
  • •Nitahamisisha vita dhidi ya Rushwa na uonevu katika halmashauri kwa kuweka mifumo rafiki ya utoaji huduma na utoaji taarifa.Hii itaenda sambamba na kuondosha ukiritimba na uzembe katika utumishi wa umma na kuhamasisha dhana ya uwajibikaji
Mkuu,Hilo neno sitaweza nalikataa,Ilo la kushawishi ndio hatua ya kwanza ya utekelezaji.Political ambition yangu sio tu kuwa Mbunge bali ni kuleta mabadiliko ya kimfumo kupitia vuguvugu la mabadiliko litakaloongozwa na wananchi.Ninaenda Bungeni kwa ajili ya kutengeneza jukwaa tu.Ndio maana ukiangalia sera zangu utaona kabisa hazilengi tu kujenga mazingira mazuri kwa wakazi wa Kigamboni bali ni kutengeneza mfumo ambao unaweza kutumiaka katika jimbo lolote kuleta mabadiliko

Kwa sasa hivi niko natafuta wagombea udiwani makini ambao watakuwa tayari kushika na kuliendesha jimbo la kigamboni.Ninafasi ya kugombea uongozi ambayo Mgombea hatakuwa na gharama kubwa za kampeni wala hatatoa rushwa bali atashinda kwa kutumia mtaji wa watu wanaotaka mabadiliko.LENGO LANGU NI KUANZISHA MOVEMENT YA MAENDELEO AMBAYO ITATIKISA KABISA MISINGI YA MIFUMO ILIYOPO.

Hah Hah Mkuu unaweka sera na ilani zako kama mgombea binafsi asiye na chama mwenye nia ya kugombea nafasi za uongozi ktk dola.

Tanzania ya kiCCM inalazimisha vyama vya siasa vilivyosajiliwa pekee ndiyo vina majukumu ya kutayarisha sera na ilani za vyama halafu wanachama na wagombea kuzinadi.

Bahati mbaya mgombea binafsi ngazi ya ubunge na urais bado haijaruhusiwa kisheria Tanzania.

Ingawa Mahakama ya Afrika Mashariki na ile Mahakama ya Afrika kupitia kukazia hukumu zao ktk kesi za msingi za wanaharakati kudai wagombea binafsi zilikubali haki hiyo ya msingi ya kikatiba.

Hukumu tayari zilitolewa na mahakama hizo za juu za kanda na bara la Afrika waliitaka serikali ya Tanzania kuruhusu haki hiyo ya kikatiba kuchagua na kuchaguliwa wagombea binafsi itekelezwe nchini Tanzania lakini serikali ya CCM imekuwa kaidi.
 
Ulipogombea kupitia ccm ,ujakubari tu kuwa upendwi.
 
Mkuu msingi wa Ugombea wangu sio mdogo bali ni mkubwa sana,Ntaka kuanzisha movement ya mabadailiko ambayo yatakuwa yananzia kwa watu,Nataka kuanzisha Movmement yangu katika Jimbo la Kigamboni.Suala la chama kwa sasa hivi sio tatizo tatizo ni jinsi ya kuiweka hio movement iwe ya kitaifa .Nitaanzia Kigamboni kwa sababu Najua kwamba Kigamboni ni Jimbo lenye Upekee fulani,kihistoria,Kidemographia na Kisiasa.

Moja kati ya ajenda zangu nitakazosimamia ni hizo kwani mimi Ni mwanamageuzi wa Kweli.
 
Back
Top Bottom