Uchaguzi 2020 Jimbo la Kigamboni - Mipango na mikakati ya kuchukua Jimbo

Nashukru mkuu kwa kunisaidia kuandika manifesto ya ubunge, haya yote uliyoandika na yale ya kwangu nitaenda kuyatekeleza! Ingawaje umechemka kwenye muda wa ubunge, yaani tukae miaka 15 wenzetu wanatusubiri tu?
 
Naomna nikuulize upande wa Elimu:
..
Umesema mpango mkakati wako ni kutoa Elimu kwa wote watalipiwa na Serikali kwa shule za Binafsi na Serikali.

Swali:
1. Unafahamu kuwa Tanzania hii kuna shule binafsi amabzo ada ni Zaidi ya Milioni 75@ Mwaka kwa mtoto wa Form 1? Rejea Int. School of Tanganyika (Gharama ya mwanafunzi mmoja ni sawa na kulipia wnfnz 1000 wa serikali kwa mwaka.

2. Je hiyo serikali unayosema imekupa assurance hiyo ya kuwalipia hao wanafunzi?

3. Je ipo kwenye sera na ilani ya CCM? Maana chama chako hakiwezi unda serikali
 
Nashukru mkuu kwa kunisaidia kuandika manifesto ya ubunge, haya yote uliyoandika na yale ya kwangu nitaenda kuyatekeleza! Ingawaje umechemka kwenye muda wa ubunge, yaani tukae miaka 15 wenzetu wanatusubiri tu?
miaka 15 ni terms kwa kutegemea ridhaa ya wananchi ila baada ya hapo huruhusiwa kugombea
 
Nipo hapa mkazi wa Kigamboni, ila naona matatizo yetu mengi hujaainisha
Matatizo ya Kigamboni ambayo tayari yapo kwenye mipnago ni kama ifuatavyo:

  1. Issue ya maji hasa Tayari iko kwenye sera
  2. Issue ya Access roads za Public Beaches tayari iko kwenye sera
  3. Issue ya uhaba wa madawati kwenye shule tayari iko kwenye sera
  4. Issue ya Barabara ya kutoka Mji Mwema-Tungi na Barabara ya Dege-Mbutu,Barabara ya Kibada-Kisarawe 2,hizo tayari ziko kwenye sera
  5. Vile vile Tunaendelea kupita kwenye KATA na MITAA kufuatilia KERO na CHANGAMOTO ZA WANANCHI MBALIMBALI
 
Kitu kidogo kama utamhulisho wako umeweka Fake Id, Itakuwaje ahadi zako?
Naona umeshindwa hata kabla ya kutangaza nia!
Mkuu behold Sijaficha utambulisho wangu,Nimeleta mjadala wa sera kwanza.Ikifika Wakati wa kujitambulisha nitaleta Verified ID hapa.
 
Small Mind,
Mambo mengi uliyoyabainisha hutaweza kuyafanya maana ni nje ya mandate ya ubunge.

Isipokuwa sema utaishawishi serikali itakayokuwa imechukua dola kufanya mambo hayo mazuri kuhusu Maendeleo ya Watu.
 
Small Mind,
Mambo mengi uliyoyabainisha hutaweza kuyafanya maana ni nje ya mandate ya ubunge.

Isipokuwa sema utaishawishi serikali itakayokuwa imechukua dola kufanya mambo hayo mazuri kuhusu Maendeleo ya Watu.
Mkuu,Hilo neno sitaweza nalikataa,Ilo la kushawishi ndio hatua ya kwanza ya utekelezaji.Political ambition yangu sio tu kuwa Mbunge bali ni kuleta mabadiliko ya kimfumo kupitia vuguvugu la mabadiliko litakaloongozwa na wananchi.Ninaenda Bungeni kwa ajili ya kutengeneza jukwaa tu.Ndio maana ukiangalia sera zangu utaona kabisa hazilengi tu kujenga mazingira mazuri kwa wakazi wa Kigamboni bali ni kutengeneza mfumo ambao unaweza kutumiaka katika jimbo lolote kuleta mabadiliko

Kwa sasa hivi niko natafuta wagombea udiwani makini ambao watakuwa tayari kushika na kuliendesha jimbo la kigamboni.Ninafasi ya kugombea uongozi ambayo Mgombea hatakuwa na gharama kubwa za kampeni wala hatatoa rushwa bali atashinda kwa kutumia mtaji wa watu wanaotaka mabadiliko.LENGO LANGU NI KUANZISHA MOVEMENT YA MAENDELEO AMBAYO ITATIKISA KABISA MISINGI YA MIFUMO ILIYOPO.
 

Hah Hah Mkuu unaweka sera na ilani zako kama mgombea binafsi asiye na chama mwenye nia ya kugombea nafasi za uongozi ktk dola.

Tanzania ya kiCCM inalazimisha vyama vya siasa vilivyosajiliwa pekee ndiyo vina majukumu ya kutayarisha sera na ilani za vyama halafu wanachama na wagombea kuzinadi.

Bahati mbaya mgombea binafsi ngazi ya ubunge na urais bado haijaruhusiwa kisheria Tanzania.

Ingawa Mahakama ya Afrika Mashariki na ile Mahakama ya Afrika kupitia kukazia hukumu zao ktk kesi za msingi za wanaharakati kudai wagombea binafsi zilikubali haki hiyo ya msingi ya kikatiba.

Hukumu tayari zilitolewa na mahakama hizo za juu za kanda na bara la Afrika waliitaka serikali ya Tanzania kuruhusu haki hiyo ya kikatiba kuchagua na kuchaguliwa wagombea binafsi itekelezwe nchini Tanzania lakini serikali ya CCM imekuwa kaidi.
 


Ulipogombea kupitia ccm ,ujakubari tu kuwa upendwi.
 
Mkuu msingi wa Ugombea wangu sio mdogo bali ni mkubwa sana,Ntaka kuanzisha movement ya mabadailiko ambayo yatakuwa yananzia kwa watu,Nataka kuanzisha Movmement yangu katika Jimbo la Kigamboni.Suala la chama kwa sasa hivi sio tatizo tatizo ni jinsi ya kuiweka hio movement iwe ya kitaifa .Nitaanzia Kigamboni kwa sababu Najua kwamba Kigamboni ni Jimbo lenye Upekee fulani,kihistoria,Kidemographia na Kisiasa.

Moja kati ya ajenda zangu nitakazosimamia ni hizo kwani mimi Ni mwanamageuzi wa Kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…