Hicho ndicho kilio cha wana Morogoro mjini walio wengi. Wanalalamika uwakilishi usiokata kiu ya maendeleo ya wakaazi wa Jimbo hilo. Wasomi na wasio wasomi, hii inajumuisha pia wananchi wa kada zote jimboni hapa wanalalamika kuwa na mwakilishi kwa miaka 15, asiye na maono ya kimikakati na amebaki kujigeuza kama mfadhiri ilhali anavyovifadhiri havina tija kwa jamii pana na kwa kesho ya wananchi wa jimbo hilo.
" Hatuhitaji vitu vinavyonufaisha mtu mmoja mmoja. Hatuhitaji misaada ambayo sio endelevu kwa kesho ya wanaMorogoro. Tunahitaji Mbunge ambaye atakuwa na uwezo wa kujenga hoja, kupanga mikakati ya muda mfupi wa kati na muda mrefu kwa ajili ya kuipeleka Manispaa yetu mbele. Mbunge ambaye atashirikiana vyema na wataalamu na watendaji wa Manispaa kwa ajili ya kusukuma gurudumu la maendeleo. Wamenukuliwa baadhi ya wananchi wakisema.
Ombi kwa CCM
Wananchi wa Morogoro wanakipenda chama CCM, wanakiomba chama hicho kiwaletee mgombea msomi, makini, mjenga hoja na ambaye hatatafsiri kuwa ubunge ni kutoa vimisaada ambavyo havibadilishi maisha ya jamii pana. Wanaomba chama hicho kiwaletee mtu makini na asiye na chembe za ubepari. Ndiyo! Wanaomba chama CCM kiwaletee mgombea asiye na chembe za ubepari ambapo kwake siasa isiwe kivuli cha kujinufaisha na kulinda amali zake bali liwe ni jukwaa la kupanga na kutekeleza mikakati ya maendeleo.
"Rais Dkt John Pombe Magufuli anahitaji watu makini wa kumsaidia. Anahitaji wapanga na watekeleza mikakati. Anahitaji wasomi, wabunifu na wenye uzalendo na uchungu wa maendeleo ya nchi. Ni vema safari hii akiwa Kama mwenyekiti wa CCM akatuletea watu/mtu makini jimbo la Morogoro mjini. Huyu apumzike aendelee na biashara zake amepwaya kwa kiasi kikubwa katika muktadha wa kuleta maendeleo endelevu jimboni hapa" Alisema mmoja wa watu wenye ushawishi kwa siasa za Morogoro ambaye ni msomi wa sayansi ya siasa.