Uchaguzi 2020 Jimbo la Morogoro mjini linamuhitaji Mbunge msomi na mwenye mikakati

Uchaguzi 2020 Jimbo la Morogoro mjini linamuhitaji Mbunge msomi na mwenye mikakati

Ila aboud bhn, kwenye misiba anatoa bus lililokongoroka. 😁

All in all Moro kwa Aboud huwaambii kitu. Wanampenda sana. Labda jina lake likatwe.

Huyu Abood kila ukitajwa mchango wake kwa wana Moro ni swala la kuchangia misiba tu nasikia. Hakuna jambo lingine analosaidia jamii hapo zaidi ya kuwaombea mfe ili atoe mabasi?
 
Alipogombea Profesa, mkamletea mizengwe ya udini na ukabila...mkamchagua mhindi kisa anatoa basi lake kwenye misiba...kaeni na huyo muhindi wenu anawatosha kwa akili zenu
Angekua ni wa muhimu sana kama angetoa misaada kwa wagonjwa sio wafu,ukifa hata asipotoa bus lake tutazikana tu.
 
Watu wa Morogoro, hasa Moro Mjini wamelaza Sana akili, wanaenda vya bure wanavyogawiwa na Avoid. Lakini Moro Kuna changamoto nyingi Sana Kama za barabara,maji n.k
Utawasikia wakisema tunampenda mbunge wetu sababu ukifiwa anajitolea gari kupeleka makaburini wakati huohuo Hana maji miaka nenda rudi. Vimisaada vya kijinga meno yote nje
 
Alipogombea Profesa, mkamletea mizengwe ya udini na ukabila...mkamchagua mhindi kisa anatoa basi lake kwenye misiba...kaeni na huyo muhindi wenu anawatosha kwa akili zenu
Hapo kwenye kutoa gari kwa ajili ya msiba ndio naonaga watu wa morogoro bure kbs. Mtu huna maji miaka nenda rudi ila kamsiba kwa mara moja kwa miaka mitano mtu kakuletea gari ndio umeona mfalme wenu. Hv hata mkichanga msibani miatano tano huyo marehemu hapelekwi makaburini. Vipo vitu vya kutupumbaza lakini hiyo staili ya kudanganya walio na upeo mdogo sn
 
Hamna hata aibu watu wa Morogoro. Hivi kweli Aboud ni mwakilishi wa wananchi wa hali ya chini wa Morogoro? Jaribu kwenda India uone kama utapata hata uwenyekiti wa mtaa....#Gabachori
Wakati wa nyerere majaji walikuwa mpaka wahindi na wazungu Acheni ubaguzi

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Mnakosea sana kufikiri haya.

Kwanza inaelekea wengine tunajiandikia tu huku hata hatujui kazi ya "mbunge" ni nini

Mbunge ni mpeleka mawazo tu ya watu anaowawakilisha kutoka katika eneo linaloitwa "jimbo la uchaguzi" katika baraza ama mkutano mkuu wa taifa wa wawakilishi wote wa majimbo yote katika nchi yote....

Mkutano ama baraza kuu hili linaitwa "BUNGE"...

Ndani ya mkutano huu wa " BUNGE", zipo pande mbili. Upande huu ni "wananchi" kupitia "wawakilishi wao - wabunge". Upande wa pili huu ipo " serikali kuu - Rais na mawaziri wake"....

Bunge ndiyo wananchi wenyewe. Bunge ni "supreme power" dhidi ya serikali. Bunge (wananchi) ndiyo wameipa serikali mamlaka ya kuamua kwa niaba yao. Bunge linakuwa pale kuidhibiti serikali isiende nje ya mstari...

Serikali kupitia vyombo na taasisi zake ndiyo ina jukumu la kukusanya kodi na kuzipangia matumizi yake. Ili matumizi hayo yawe "legal" ni sharti yawe approved na wanachi kupitia chombo chao - Bunge...

Unapofika wasaa huu wa kupitisha matumizi ya serikali kwa nchi nzima, ndipo kila mbunge anapotoa mahitaji ya watu wake ktk locality (jimbo) lake....

Kwamba jimboni kwangu wananchi wanahitaji 1, 2, 3, 4.....nk. Sasa Tanzania nasikia ina majimbo zaidi ya 250...

"Mbunge" huyu si mwamuzi wa kile watu waliomtuma wanataka kiwe;

Mfano kama waliomtuma wanataka wajengewe barabara ama shule ama kitu hiki ama kile. Kiuhalisia yeye hana uamuzi wa kusema watu wa jimbo la Morogoro mmenituma kupeleka ombi la mjengewe barabara ama shule ama stendi, basi mmepata tayari...

Hana uamuzi huo asilani hata awe msomi wa kiwango cha juu chochote duniani..!!!!

Kupeleka mawazo ya unaowakilisha kama mbunge na kupokelewa ni jambo moja. Lakini maombi/mawazo kufanyiwa kazi ni jambo jingine kabisa. Na hapa ndipo palipo na shida....

Kufanyiwa kazi kwa mawazo ya watu anaowakilisha mbunge kunategemea mambo mengi;

å Allocatiin ya bajeti/rasrimali fedha ya nchi
å Utashi wa kisiasa wa wenye maamuzi na mamlaka
å Vipaumbele vya kibajeti (budgetary priorities) vya nchi
å Nani anahitaji zaidi kuliko mwingine ama jimbo gani linahitaji zaidi kitu hicho hicho...
å Nk nk nk..

Kwa kuzungatia jukumu ama kazi ya mbunge, mtu yeyote anaweza kuwa mbunge ili mradi ana akili timamu, msikilizaji mzuri, anajali, ana uwezo wa kujenga hoja na kueleweka, mbunifu, mhamasishaji (mobilizer & motivator) mzuri wa anaowakilisha nk nk....

"Usomi" wa mbunge wa kiwango chochote "it's just an added advantage" lakini hakiwezi kuwa kigezo cha jimbo fulani kuwa guaranteed kupiga hatua kubwa za kimaendeleo kijamii na kiuchumi eti kwa sababu lina mbunge msomi...!!

Na kwa taarifa na faida ya wasomaji, wengi wa "watu wasomi wana sifa hizi; wana viburi, watafuta vyeo tu kwa kutumia usomi wao, si wanyenyekevu, wana maringo kwa sababu ya elimu yao na tabia zingine zinazofanana na hizi....

Hawa kwa ujumla wengi wao hawafai kuwa wakikilishi wa watu kwenye nafasi kama ya ubunge, udiwani nk.....

Kinacholeta tatizo ktk nchi yetu ni mfumo wetu wa kiutawala kikatiba na kisheria kuwa na matundu ama matobo tobo mengi....

Walioweka kigezo kikuu cha mwakilishi (mbunge ama diwani) kuwa na sifa ya KUJUA KUSOMA na KUANDIKA tu ba kiwango cha elimu ya drs la VII ama form IV tu, walikuwa sahihi sana kwa kuwa walizingatia jukumu/kazi ya mwakilishi huyu ni nini.

As time went on na kutokana mfumo wa utawala wa nchi ukaondoka katika lengo lake kuu yaani kuhudumia wananchi na kuwa kujinufaisha viongozi kwanza kwa gharama ya wananchi (wapiga kura).

Wasomi wengi wakaiona fursa hii. Wengi wakawa wanaacha taaluma zao na kuingia kwenye siasa na kuanza kusaka nafasi za uongozi wa kisiasa kama uDC, uRC, uWaziri, ubunge nk nk

Watapitia wapi? Ni huko kwa wananchi kwa kuwarubuni na usomi wao kwa ahadi kuwa watatumia usomi wao kuwandolea kero ya umasikini wao hawa wananchi huku ukweli ukiwa ni kuwa wanaenda kujikwamua wao na familia zao kutoka kwenye umasikini....!!

Kwa hiyo tusidanganyane hapa....
Ukweli mtupu. Watanzania walio wengi hawajui ni nini kazi ya mbunge.
 
Back
Top Bottom