Uchaguzi 2020 Jimbo la Morogoro mjini linamuhitaji Mbunge msomi na mwenye mikakati

Katiba inataka mbunge ajue kusoma na kuandika tu,sasa huyo msomi wewe Wa nini?
Hata kanuni za kupaa angani zinataka ndege awe na mabawa ya mifupa, manyoya na nyama.. Lakini zinatengenezwa ndege za mabawa ya chuma (Aluminium) ili ziweze kwenda kasi na kuchukua mzigo mwingi zaidi.

Mtu msomi anakuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kujenga hoja na kutatua changamoto.
 
Nawaambieni Morogoro mlianza kuwa na akili mlipowachagua CDM, sasa kama mnataka kurudi nyuma basi endeleeni kuwachagua ccm mtabaki kama mlivyokuwa zamani, yaani moja ya mikoa midebwedo nchini.
Moro Kuna nuka ccm
 
ujengaji hoja no kipawa,mbona wasomi wenu wengi hawawezi kujenga hoja,Ila hao unaowaona siyo wasomi wanajenga hoja nzuri Sana na zenye mashiko.

Kama mnataka badilisheni kifungu hicho kwenye katiba.
 
Mkuu nimekuvulia kofia na unajua mpaka unakera hongera kwa uchambuzi maridhawa nnaamin utaeleweka kwa wenye kujua, HONGERA SANA
 
Tafuteni mtu mwenye akili atawasaidia sana kuliko hawa wabeba makaratasi kwani hawatawasaidia chochote
 
Ila aboud bhn, kwenye misiba anatoa bus lililokongoroka. 😁

All in all Moro kwa Aboud huwaambii kitu. Wanampenda sana. Labda jina lake likatwe.
 
Wanakera mno yaani
Na mm kama mwana Moro nasema Aboud apewe 5 mingne. Hawa wasomi aliotaja mleta mada watatuletea figisu na maisha ya gharama. Ukishindwa kuishi Moro, ufe tu hakuna sehem utaweza.

Cha msingi serikali ituletee maji na barabara za mitaa zijengwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…