Uchaguzi 2020 Jimbo la Moshi Mjini lachukuliwa na CCM kwa mara ya kwanza tangu Uasisi wa mfumo wa Vyama Vingi nchini

Uchaguzi 2020 Jimbo la Moshi Mjini lachukuliwa na CCM kwa mara ya kwanza tangu Uasisi wa mfumo wa Vyama Vingi nchini

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Jimbo la Moshi Mjini lililoko Moshi mkoani Kilimanjaro limekuwa chini ya CHADEMA kwa muda wa miaka 20, kuanzia mwaka 1995.

Katika Uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995 Antony Komu alishinda Jimbo hilo kupitia NCCR-Mageuzi na kuwa mbunge hadi mwaka 2000. Komu alihamia CHADEMA.

Kuanzia mwaka 2000 hadi 2015 lilikuwa chini ya Philimon Ndesamburo kupitia CHADEMA. Uchaguzi Mkuu wa 2015 ulimfanya Japhary Michael kuwa mbunge wa jimbo hilo hadi mwaka 2020.

Katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, Priscus Tarimo kupitia CCM amelichukua Jimbo hilo na kufanya Jimbo hilo kuwa la CCM kwa 2020 – 2025.
 
NI UDANGANYIFU MKUBWA ULIOFANYIKA HAWA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI WOTE NI MAKADA WA CCM WALIOSHINDWA KWENYE UCHAGUZI WA 2015
NI UKIUKWAJI MKUBWA WA DEMOKRASIA NA HAKI ZA WALIOPIGA KURA POLENI SANA WOTE MLIOPIGA KURA KWANI
YALIOTANGAZWA SIO MATOKEO HALISI BALI NI MATOKEO YA KUPIKWA NA WASIMAMIZI MAKADA WA CCM
 
Kule Tarime nako, Jonh Heche out!!!

Siju sasa Jimbo gani CHADEMA wanauhakika nalo
 
Kuna kitu nakiona hakijakaa sawa. Either ni hapa JF au ni Tume ya uchaguzi.

Nafatilia hapa JF nione matokeo. Naona yanatoka yale wapinzani wakuu tu walikobwagwa. Mbowe, Sugu, Moshi hapo. Kwani mbona hatupati huko kwingine?! Mbona kama matokeo yanatoka style ya kutuumiza tuumie kwanza?!?? What's not right here?
Karibia nyuzi zoote ni hao tu wapinzani wakubwa. Sasa tatizo hii propaganda ni tume ya uchaguzi au ni JF. Maana JF nayo siku izi nna mashaka nayo sana sijui kwa nn.
 
Kifo ni Siri ya ya muumbaji.
Anaweza kushinda uchaguzi na akafa vilevile Kama ambavyo anaweza kufa baada ya kushindwa Uchaguzi.

Kushinda au au kushindwa hakuathiri so ujio wa siku ya kifo cha binadamu.
Labda kufa kwa msongo kwa mshindwa au furaha iliyopitiliza na kusababisha uzembe ukamuuwa mshindi.
Mbona unasema 2020-2025 anaweza kufa pia asifike hiyo 2025.
 
Duh ila twende mbele turudi nyuma Zanzibar ni wala Urojo ila wanajua kukaza...huku Bara buana tuendelee kuwa Wanaume wa Bara tishio kidogo tuu tumefyata mikia tunasubiri Karma itende kazi yake hata Kenya wakitudharau ni sawa asee, duuh Ushindi wa sasa ni maandalizi ya kupita 2025......

Sababu Mbowe,Mbilinyi,Mdee,Heche wote Out tutabakia kuwa wasikivu na wenye Amani ya kudumu yenye walakini ndani yake mpaka ukamilifu wa Dahari...Hahahahaha
 
Hili ndilo tatizo la kuacha Mzungu Robert Amsterdam kuwa kampeni meneja wa Lisu.

Mbowe hakutaka hata mara moja kuwa sehemu ya kampeni ya mgombea wake wa Urais,

Wala hakumkemea mzungu kuchafua image ya Chama,

Tulionya hapa hamkusikia.

Haya sasa kunyweni katika kikombe chenu.
 
Mashindano kwa wakuu wa mikoa Wakuu wa Wilaya Wakurugenzi kuiba kura kumuonyesha mungu mtu ili wapate sifa. Wamejitaidi maelekezo waliyapata toka mda mrefu.

NIKUPE MSHAHARA, NIKUPE NYUMBA, NIKUPE GARI, ALAFU UMTANGAZE MPINZANI MSHINDI.

waTanzania tupeane polee kwakuwa na Raisi Aina ya Magufuli.

Waumiaji kiuchumi Ni wengi wanufaika makada wachache wanakula mema ya inchi.
 
Back
Top Bottom