Uchaguzi 2020 Jimbo la Moshi Mjini lachukuliwa na CCM kwa mara ya kwanza tangu Uasisi wa mfumo wa Vyama Vingi nchini

Uchaguzi 2020 Jimbo la Moshi Mjini lachukuliwa na CCM kwa mara ya kwanza tangu Uasisi wa mfumo wa Vyama Vingi nchini

Kuna kitu nakiona hakijakaa sawa. Either ni hapa JF au ni tume ya uchaguzi.

Nafatilia hapa JF nione matokeo. Naona yanatoka yale wapinzani wakuu tu walikobwagwa. Mbowe, Sugu, Moshi hapo. Kwani mbona hatupati huko kwingine?! Mbona kama matokeo yanatoka style ya kutuumiza tuumie kwanza?!?? What's not right here?
Karibia nyuzi zoote ni hao tu wapinzani wakubwa. Sasa tatizo hii propaganda ni tume ya uchaguzi au ni JF. Maana JF nayo siku izi nna mashaka nayo sana sijui kwa nn.
Sugu, Mbowe...chali, kifo cha mende, ndembe, ndembe...kwa sauti ya Lipumba!
 
Halijachukuliwa, limeporwa na TISS wakawapa CCM.
 
Jimbo la Moshi Mjini lililoko Moshi mkoani Kilimanjaro limekuwa chini ya CHADEMA kwa muda wa miaka 20, kuanzia mwaka 1995.

Katika Uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995 Antony Komu alishinda Jimbo hilo kupitia NCCR-Mageuzi na kuwa mbunge hadi mwaka 2000. Komu alihamia CHADEMA.

Kuanzia mwaka 2000 hadi 2015 lilikuwa chini ya Philimon Ndesamburo kupitia CHADEMA. Uchaguzi Mkuu wa 2015 ulimfanya Japhary Michael kuwa mbunge wa jimbo hilo hadi mwaka 2020.

Katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, Priscus Tarimo kupitia CCM amelichukua Jimbo hilo na kufanya Jimbo hilo kuwa la CCM kwa 2020 – 2025.
Mbunge wa kwanza moshi mjini baada ya vyama vingi kurudishwa alikuwa Mtui
 
Duh ila twende mbele turudi nyuma Zanzibar ni wala Urojo ila wanajua kukaza...huku Bara buana tuendelee kuwa Wanaume wa Bara tishio kidogo tuu tumefyata mikia tunasubiri Karma itende kazi yake hata Kenya wakitudharau ni sawa asee, duuh Ushindi wa sasa ni maandalizi ya kupita 2025......

Sababu Mbowe,Mbilinyi,Mdee,Heche wote Out tutabakia kuwa wasikivu na wenye Amani ya kudumu yenye walakini ndani yake mpaka ukamilifu wa Dahari...Hahahahaha
Wewe umekaa nyuma ya keyboard unapiga kelele unataka nani akupiganie
 
Back
Top Bottom