Jimbo la Musoma Vijijini: Serikali Yaendelea Kuchangia Ujenzi wa Sekondari Mpya za Kata

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Serikali imetoa fedha kwa Kata mbili (2) kujenga sekondari mpya za Kata hizo.

Kata hizo ni:
1. Nyamrandirira
Sekondari itajengwa Kijijini Kasoma
2. Bukima
Sekondari itajengwa Kijijini Butata

Serikali imetenga Tsh 584,280,000.000 (Tsh 584.28m) kwa ujenzi wa kila moja!

Ushauri:
1. Viongozi wa Serikali na Chama wa Kata, Vijiji na Vitongoji wahamasishe wananchi wachangie nguvukazi ili miundombinu mingi ya elimu ipatikane kutoka kwenye fedha hizo

2. Maeneo ya ujenzi yasiwe na migogoro ya aina yo yote ile.

3. Wananchi wafuatilie matumizi ya fedha za ujenzi kwa ukaribu sana. Tumejifunza mengi kutoka Kata za Ifulifu (Kijiji cha Kabegi) na Suguti (Kijiji cha Wanyere)!

4. Ujenzi ukamilike mapema ili ifikapo Januari 2025, sekondari hizo mpya zifunguliwe

Maombi mengine (mapya) ya wananchi ya kujenga sekondari mpya kwenye vijiji vyao:

Mbunge wa Jimbo amepokea maombi kutoka vijiji vitatu (3) ya kujenga sekondari mpya:
(i) Kijiji cha Kataryo, Kata ya Tegeruka
(ii) Kijiji cha Kiriba, Kata ya Kiriba
(iii) Kijiji cha Mmahare, Kata ya Etaro

Mbunge wa Jimbo ameyakubali maombi hayo na baada ya Bunge ataenda kupiga Harambee za kuanza ujenzi wa sekondari hizo.

Sekondari zinazojengwa sasa hivi kwa nguvu za wananchi na viongozi wao ni:

(i) Rukuba (Kisiwa), Kata ya Etaro
(ii) Nyasaungu, Kata ya Ifulifu
(iii) Kurwaki, Kata ya Mugango
(iv) Muhoji, Kata ya Bugwema (Serikali imeanza kuchangia kwa kutoa Tsh Milioni 75)

Vijiji vingine zaidi ya vitano (5) vimeomba kujenga sekondari mpya lakini mipango yao haijakamilika!

Idadi ya Sekondari zinazotoa elimu, kwa sasa, ndani ya Jimbo letu lenye Kata 21 zenye Vijiji 68:

Sekondari 28: 26 za Kata/Serikali na 2 Binafsi

Lengo Kuu:
Kila Kata iwe na sekondari mbili (2) au zaidi - mfano Kata ya Nyamrandirira yenye vijiji vitano (5), ifikapo Januari 2025 itakuwa na sekondari tatu (3) - sekondari kwenye vijiji vya Kaboni, Seka na Kasoma.

SHUKRANI:
Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini tunaendelea kuishukuru Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutupatia fedha za miradi ya maendeleo, ikiwemo ya ujenzi wa shule mpya za msingi na sekondari, na uboreshaji wa miundombinu ya elimu kwenye shule zetu - ahsante sana!

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Alhamisi, 20.6.2024
 
Inacho chekesha hii serikali ni kama haina mipango sijui walio pewa madaraka uwezo wao ni mdogo sana, wanajenga shule halafu wanapunguza walimu shule ambazo bado zina uhaba wa walimu wanawapeleka shule hizo mpya badala ya kuajili walimu wapya kwenda huko,
 
Back
Top Bottom