Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,430
JIMBO LA NAMTUMBO: BILIONI 3.3 ZATUMIKA UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA RUVUMA
Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma, unaendelea kutekelezwa kwa awamu ambapo hadi sasa, kiasi cha Shilingi Bilioni 3.3 kimetumika katika ujenzi pamoja na kukamilisha jengo la huduma za mionzi pamoja na kusimikwa kwa mashine za kisasa za CT scan na Digital X-Ray zikiwa zimeanza kutoa huduma.
Akijibu swali la Mbunge wa Namtumbo, Mhe. Vita Rashid Kawawa, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, amesema kuwa ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) unaendelea na kwamba Serikali imetenga Shilingi Bilioni 2 kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ili kuendeleza ujenzi huo.
“Mradi huu unatekelezwa kwa awamu na unatarajiwa kukamilika katika awamu ya tatu ifikapo mwaka wa fedha 2025/2026,” ameeleza Dkt. Mollel wakati wa kikao cha Bunge.
Hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali kuboresha huduma za afya katika mikoa ya pembezoni na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na za kisasa karibu na maeneo yao ya makazi.