MwanaHaki
R I P
- Oct 17, 2006
- 2,401
- 707
Ni kweli, yu hoi matibabuni India, na tetesi ni kwamba huenda hatapona. CCM imempitisha mgombea ambaye ni MGONJWA MAHUTUTI, na kumuengua mgombea anayekubalika na mwenye uwezo mkubwa kuchaguliwa.
Ama kweli, siku ya kufa kwa nyani, miti yote HUTELEZA! CCM wamechanganyikiwa kiasi kwamba wanapoteza majimbo kwa maamuzi ya KIJINGA! Tayari wameshapoteza majimbo kadhaa kwa upande wa upinzani, hata kabla ya uchaguzi, likiwamo Masasi (ambayo ilikuwa ngome ya CCM mikoa ya kusini). Wanajinadi kwamba wana majimbo 10 ambayo wagombea wa CCM hawana upinzani. Lakini wamesahau, NEC inaweza kutupilia mbali pingamizi za CCM kwa wagombea wa upinzani, kwani kila siku rufaa zinakatwa. Tayari imeshatokea.
Kitaeleweka mwaka huu, kwani HATUDANGANYIKI!