Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Leo mishale ya saa 7 mchana nimeona kundi kubwa la akina mama hapa Bonyokwa wakiwa wanazingira kwenye ukumbi wa Masia, katika kufuatilia zaidi kumbe mgombea ubunge jimbo la Segerea, bibie Bonnah Kamoli alikuwa amewaita ili kuungwa mkono kwa kuwapa elfu 5 na zawadi nyingine ndogondogo
Wakati bado nastaajabu akaja boda mmoja, nikawa napiga naye story, akaanza kusema mitano tena blah blah kibao, nikauliza kwanini mitano tena, akafunguka kuwa juzi Bonnah aliwaita bodaboda wa Bonyokwa katika ukumbi wa Shedafa (Shedafa garden), akawatia mpunga wa mafuta, lakini cha kusikitisha zaidi akawa anachukua namba za mpigakura kwa kila mwenye kitambulisho.
Akafunguka zaidi kuwa wakati wameitwa kwenye ukumbi, waliambiwa wasirekodi kitu chochote kwa kutumia simu janja zao, ibaki kuwa suala la ndani tu.
Nikamuuliza boda kama aliuliza taarifa zao zinazokusanywa waliambiwa zinachukuliwa kwa kazi gani au sababu nyingine akadai hajui. Nikamwambia kuwa zitatumika kupiga kura feki ndo akastuka.
Sasa TAKUKURU hizi chengachenga sijui kama wanazifahamu, mgombea anatoa rushwa ya waziwazi halafu anapiga mkwara yanayoendelea yasirekodiwe. Nitajitahidi kutafuta ushahidi wa video, sidhani kama boda wote hakuna aliyechukua tukio.
Ni hayo tu