Texas wanatumia sana umeme wa windmills, ni jimbo la kwanza kutumia umeme wa windmills. Zaidi hata ya California.
Sasa na hili arctic chill lilivyopiga na kumwaga snow windmills zimeshindwa kufanya kazi. Hii ni moja ya sababu kumekuwa na matatizo ya umeme.
Jana kuna mtu nilikuwa naongea naye kazini, yuko huko. Anasema hajawahi kuona hali hii.
Miaka 15 iliyopita nilienda kumtembelea dada yangu huko, nimetoka zangu New York kipindi cha baridi. Nimevaa makoti yangu ya baridi. Kufika Texas ikawa joto kama nimefika Dar!
Watu wa Texas hawajazoea snow.
Unaweza kukuta mtu katoka Texas kaja New York mara ya kwanza anashangaa snow sawa na mtu aliyetoka Tanzania.