Nimeona vyema nikusaidie kufahamu tu nini kilichotokea Ubungo mwaka 2005. Maana ukikuwa na ufahamu huu, utakuwa kwa uongo ambao hauna manufaa yoyote.
Ndugu yangu, matokeo ya Jimbo la Ubungo yalichelewa kutangazwa kwakuwa Mnyika na Mama Kessy waliweka pingamizi yasitangazwe, kwa kuwa walitaka kuthibitisha mara kadhaa kuwa idadi ya kura ni sahihi. Hata baada ya kuthibitisha hivyo, waliendelea kung'ang'ania kuwa kura hazikuwa sahihi. Ilibadi ilazimishwe kutangazwa baadae kwakuwa sababu zilizosababishwa yasitangazwe mapema zaidi zilikuwa hazipo tena, hata baada ya wapinzani hao kuendelea kusisitiza zisitangazwe. Nadhani nia ilikuwa kuthibitishia umma na watu kama wewe kuwa kulikuwa na wizi uliokuwa ukifanyika na ili kuwezesha kurudia uchaguzi wakihisi kuwa wangeweza kushinda endapo uchaguzi ungerudiwa. Bahati mbaya kwao hiyo haikutokea.
Mimi naamini kuwa Mnyika atakuwa Mbunge siku moja endapo ataendelea bila kuchoka kutafuta nafasi hiyo, na kama atapata support ya watu wengi zaidi na hasa mbinu ya kutafuta kura kutoka kwa wapiga kura na sio washabiki au warusha vibendera wasio na sifa za kupiga kura. Naamini kwa Mnyika kushinda Ubungo anahitaji juhudi kubwa sana kuliko zinavyoongelewa hapa. La sivyo, mwaka huu wengi watasema tena kuwa kadhulumiwa ushindi.
Msaidieni kwa nguvu zote kama mnataka ashinde.