Jina la kitabu :Jinsi ya kuendelea kuwa maskini

Wang chung

Member
Joined
Oct 26, 2024
Posts
26
Reaction score
36
Kitabu cha "Jinsi ya Kuendelea Kuwa Masikini" kinatoa mifano na ushauri kuhusu tabia na maamuzi yanayoendelea kuwafanya watu kubaki kwenye umasikini. Hiki ni kitabu kinachokosoa mtindo wa maisha, ufikiriaji, na maamuzi ambayo mara nyingi huwafanya watu kushindwa kufanikiwa kiuchumi. Kinahimiza watu kuepuka tabia kama vile kutotaka kujifunza, kufanya kazi kwa juhudi kidogo, kuwa na mtazamo finyu kuhusu fedha, na kutojiwekea malengo madhubuti. Katika hali ya jumla, kitabu kinachunguza vikwazo vya kimawazo na kimazingira vinavyoshindwa kuvunjwa na wengi, na jinsi ya kutokomeza vikwazo hivyo ili kufikia mafanikio.

Utakipata kwa bei ya tsh 3000/=
 
Yaani unataka nilipe 3,000 ili nisome jinsi ya kuendelea kuwa masikini? Title ya kitabu chako haijakaa sawa bosi wangu ila kila la heri. Naona na wewe unapambana ili kuendelea kuwa masikini!
 
Yaani unataka nilipe 3,000 ili nisome jinsi ya kuendelea kuwa masikini? Title ya kitabu chako haijakaa sawa bosi wangu ila kila la heri. Naona na wewe unapambana ili kuendelea kuwa masikini!
Mkuu mweka mada hana maana ya kwamba uwe maskini, maana yake hivyo vitu vinavyomfanya mtu awe maskini unatakiwa uende navyokinyume!..
kitu kidogo tu mnashindwa kufikiri tukianza kuwaambia mnatumia akili mnemba mnaanza kuwa wakali...!!
 
KENZY huyo ni mfanyabiashara, anatakiwa kuuza mawazo yake kupitia kitabu alichoandika, unafikiri kwa kichwa hicho kitawavutia wangapi?
 
KENZY huyo ni mfanyabiashara, anatakiwa kuuza mawazo yake kupitia kitabu alichoandika, unafikiri kwa kichwa hicho kitawavutia wangapi?
uandishi ni kazi ya sanaa na sanaa ni ubunifu!, mimi sijaona shida kwenye hiyo tittle labda uwe hufikirii tu!
 
uandishi ni kazi ya sanaa na sanaa ni ubunifu!, mimi sijaona shida kwenye hiyo tittle labda uwe hufikirii tu!
Ni sawa, lakini kwa mawazo yangu hiyo sanaa yake angecheza nayo ndani ya kitabu.
Angekuwa amelenga kama kitabu cha kufundishia mashuleni kusingekuwa na tatizo, lakini lengo lake ni “biashara” na wateja wake ni jamii nzima, asiyejua sanaa ya uandishi na anayejua sanaa ya uandishi.

Sawa, nimekatiza mtaani mimi nisiyejua sanaa nikakiona, kichwa cha habari tu kitanikimbiza kwasababu sipendi kuendelea kuwa maskini.
 
Mbona vile vya "Nilivyokuwa nakula nyama za watu!" mnavinunu hebu niambie hiyo tittle ni nzuri..?
muacheni kama hatauza hiyo ni juu yake!.
 
Mkuu mweka mada hana maana ya kwamba uwe maskini, maana yake hivyo vitu vinavyomfanya mtu awe maskini unatakiwa uende navyokinyume!..
kitu kidogo tu mnashindwa kufikiri tukianza kuwaambia mnatumia akili mnemba mnaanza kuwa wakali.!!!
Kutumia akili mnemba nalo limekuwa tusi siku hizi? Ni wapi ulipotuambia kuwa tunatumia akili mnemba tukawa wakali? ☹

Kwa vile hii siyo kazi ya kifasihi, wewe umefikiaje mahitimisho hayo hata kabla ya kukisoma kitabu?

➡️➡️➡️ Anyway, mimi nilikuwa namzingua tu maana hiyo title kwa mtu mwingine kusema kweli haijakaa poa hata mmtetee namna gani. Ningekuwa publisher/mhariri wake nisingekubali kitabu kitoke kikiwa na title hiyo!
 
Ndiyo pointi yangu hiyo pia. Hii siyo kazi ya kifasihi. Huyu ni motivesheno spika na hana nafasi ya kupoteza katika kukamata shauku ya hadhira yake. Ndiyo maana nikasema hiyo title haijakaa poa. Ingekuwa ni riwaya, wala kusingekuwa na tatizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…