Jina la kitabu :Jinsi ya kuendelea kuwa maskini

Sina shida na title ya kitabu na bei.Ningependa kujua maudhui yaliyomo kwa ufupi ili kuhamasika
 
Mkuu mweka mada hana maana ya kwamba uwe maskini, maana yake hivyo vitu vinavyomfanya mtu awe maskini unatakiwa uende navyokinyume!..
kitu kidogo tu mnashindwa kufikiri tukianza kuwaambia mnatumia akili mnemba mnaanza kuwa wakali...!!
Afadhali wewe umeelewa
 
Sina shida na title ya kitabu na bei.Ningependa kujua maudhui yaliyomo kwa ufupi ili kuhamasika
Kuna sababu za kukufanya eendelee kuwa maskini, madhara ya umasikini na namna ya kuukimbia umaskini
 
Mbona vile vya "Nilivyokuwa nakula nyama za watu!" mnavinunu hebu niambie hiyo tittle ni nzuri..?
muacheni kama hatauza hiyo ni juu yake!.
Mkuu, jamii inapenda stori za mapenzi, uchawi na uhalifu.

Jamii tayari ni maskini halafu kitabu chako kwa juu kinaishawishi jamii iendelee ilipoishia.
 
Yaani unataka nilipe 3,000 ili nisome jinsi ya kuendelea kuwa masikini? Title ya kitabu chako haijakaa sawa bosi wangu ila kila la heri. Naona na wewe unapambana ili kuendelea kuwa masikini!
Don't judge book for it's cover
 
Sanaa ya uandishi ni kumvutia msomaji hata kabla ya kuanza kukisoma kitabu chenyewe.

Yeye haoni magazeti yanavyopamba vichwa vya habari ili uvutike ununue, ukisoma ndani wala hayana uzito kama kichwa cha habari.

Nani anapenda umaskini?
Kuna watu wanapenda vitu tofauti
 
Don't judge book for it's cover
Acha kushupaza shingo. Kama bado kitabu kiko kwenye production, badilisha title ya kitabu hicho. Jinsi ya Kutoendelea Kuwa Masikini Inasadifu Zaidi na inamvutia mtu kutaka kujua yaliyomo.

Umepata bahati umepata sample ya wateja wako hapa. Zingatia maoni yao kama kweli unataka kuuza.
 
Mkuu mweka mada hana maana ya kwamba uwe maskini, maana yake hivyo vitu vinavyomfanya mtu awe maskini unatakiwa uende navyokinyume!..
kitu kidogo tu mnashindwa kufikiri tukianza kuwaambia mnatumia akili mnemba mnaanza kuwa wakali...!!
Kuongezea mkuu,lengo kuwafungua watu wacho dhidi ya tabia zao (za kimazoea) kuwa ndizo zinazowarudisha nyuma kufikia maendeleo.
MF.Kutojali muda (hii inaonekana kawaida ila ni njia ya Jinsi ya Kuendelea Kuwa Masikini)
 
Wazo lako nimelichukua mkuu maana katika maisha kitu muhimu ni kuzidi kuwa Bora πŸ™
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…