Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 1,117
- 3,153
Hayati Rais John Pombe Magufuli ndiye mtu aliyetajwa sana katika mwaka huu 2022,penye hoja na pasipokuwa na hoja,ndiye Rais pekee ambaye atazidi kuendelea kutajwa mara nyingi kwenye awamu hii na awamu zijazo na hata kwenye uchaguzi ujao,alikuwa ni mmoja wa viongozi wachache sana wazalendo wa kweli kwa wananchi wanyonge Nchi nzima ya Tanzania.
Ni hulka ya binadamu,tunapokuwa mbele ya Watanzania,kama kiongozi nifanyeje ili nami wanione bora kama Rais John Pombe Magufuli au niwe bora zaidi yake,je nimtukane au nitende kama yeye,kwa hivyo basi Rais Magufuli amefanyika kuwa kipimio cha wengi kwa kihaya wanasema Rais Magufuli amefanyika kuwa "Measuring stick".
Kila kiongozi lazima atamtaja ili kujipima mbele za Wananchi wa Tanzania,Kila kiongozi anaetaka kukanekti na wananchi basi lazima amtaje Rais Magufuli ili kujiweka sawa kwenye uongozi na Wananchi waweze kumuelewa,bila kutaja jina la Rais Magufuli basi Wananchi hawawezi kukuelewa.
Uwe na hoja usiwe na hoja utamtaja tu,awe alikuziba mdogo au hakukuziba mdomo utamtaja tu,uwe unampenda au haumpendi utamtaja tu,sisi wauza mchicha tunasubiria reli ya Mwendokasi SGR iishe tukauze mchicha toka Dodoma na Morogoro tupeleke Dar es Salaam,sijui nauli itakuwa shilingi ngapi.
Naamini sisi wauza mchicha tutapewa 7,000 kama tulivyopewa kipaumbele na Hayati Rais Magufuli,naamini wanyonge wanamtaja kila siku wakati wa kununua mchele kilo moja 3,200 mle ugali ndugu zangu kilo 2,200 sasa shida maharage kilo 3,000 nayo imekuwa mboga ya anasa.
Hayati Rais Magufuli ameendelea kutikisa mwaka huu 2022 kwa sababu moja tu hakuna mtu mwenye sifa kama zake kiutawala,hili nalisema kama mbobezi katika masuala ya Uongozi,Rais John Pombe Magufuli alikuwa Champion katika mambo mengi na kila mwananchi analijua hilo.
Hii inawapa wakati mgumu viongozi wengi wanapokuwa mbele za Wananchi hivi sasa,useme nini wananchi wakuelewe,maana tayari Wananchi wana mfano wao wa kiongozi bora,wana performance appraisal ya kiongozi wao bora,nae ni John Pombe Joseph Magufuli.
Mtu ambae amefanya kazi na watanzania bara miaka zaidi ya 20 akiwa ni Field Public Leader tangu akiwa Naibu Waziri miaka ya 1995 kisha Waziri kamili katika wizara zaidi ya tano kwa miaka ishirini na baadaye kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Faida na hasara za kulitaja jina la Rais Magufuli.
Faida
Katika Uongozi wa Rais Magufuli tulishuhudia improvements kubwa sana katika huduma za kijamii na miundo mbinu ambayo kimsingi Watanzania wengi walikuwa wahanga wa huduma mbovu kabla yake, hivyo basi utakapo fanya jambo jema kwenye huduma za jamii au miundo mbinu na ukalitaja jina la Rais Magufuli basi Wananchi watakuelewa sana.
Hayati Rais Magufuli alileta elimu bure,aliwasaidia Watanzania wengi sana. Takwimu zinathibitisha hili baada ya wanafunzi wengi sana kuongezeka sasa,hii ni faida aliyoleta Rais Magufuli.Rais Magufuli alitatua kero za wanyonge na walioonewa ambao walishaomba msaada kwa wasaidizi wake karibu wote bila kusaidiwa,na wakakata tamaa,Wananchi walifurahi Rais Magufuli alipokwenda na kutatua matatizo yao pale pale,hiyo ilikuwa ni karama ya Uongozi aliyokuwa nayo Rais Magufuli.
Magufuli alilinda rasilimali za nchi,tulifikia wakati hadi twiga wanapanda ndege,unatarajia Watanzania wengi tungemchukia,jibu ni hapana, Watanzania walimpenda Rais Magufuli kwa sababu Wanyama waliongezeka mbugani badala ya kupungua na takwimu zinaonyesha,Rais Magufuli alijenga ukuta Mererani kuzuia kuibiwa kwa madini ya Tanzanite,hii hakuifanya kwa ajili yake bali aliifanya kwa ajili ya Watanzania,je unatarajia Watanzania wamchukie!?
Rais Magufuli aliwatetea machinga na mama ntilie, nao wakawa walau na uhuru wa kufanya biashara zao halali kwa amani ili kupata vipato vya kusaidia familia zao.je unatarajia Watanzania wangemchukia Watanzania walimpenda kwa kuwa alikuwa kiongozi bora, not kwa kuwa aliwahenyesha matajiri hapana Rais Magufuli hakuhenyesha matajiri, alihenyesha wapigaji,wala rushwa,waonea wanyonge, Mafisadi na walanchi.
-Hasara
Unapotaja jina la Rais Magufuli kwa chuki binafsi za udini,ukabila au itikadi hii ni hasara kwako,adui yako si Magufuli,kwa wapinzani adui yenu ufisadi, uongozi mbovu,mfumuko wa bei kwenye bidhaa,na kutotumia vyema rasilimali za Tanzania kuinufaisha Tanzania.
Mpinzani wenu ni CCM kama itafanya vibaya mbele za Wananchi,Kosa hilohilo lilifanywa na Chadema ambao waligombana na Zitto na Dkt Slaa huku adui yao akiwa ni CCM ambayo ilionekana kuanza kukataliwa kwa Wananchi,
Kwa sasa tuna tatizo kubwa la mfumuko wa bei vitu vinavyowagusa Wananchi moja kwa moja badala yake Zitto Mambo ya mwaka 2017 na anamtaja mtu aliyekufa!! Sasa ataamka aje akurekebishie mfumuko wa bei uliopo hii leo!!?
Tukiwa kwenye mfumuko wa bei hakuna atakayemsema Hayati Rais Magufuli akapata Faida yoyote Ile, zaidi nawaona wanaomkosoa hasa viongozi kama akina Zitto wakipata uharibifu mkubwa na kujenga chuki mioyoni mwa wananchi wa hali ya chini, masikini ambao daima walimuona Rais Magufuli mkombozi wao.
Wakati huu wa maisha magumu vitu vinapanda bei ukimshambulia Rais Magufuli, Kwa namna mbalimbali,ni kujimaliza kisiasa,kifikra,kiutamaduni na kimaendeleo.
Kundi la Wananchi masikini walioneemeka au kupata ahueni kijamii,kiuchumi na kisiasa katika awamu ya Rais Magufuli daima watamchukia mtu ambae anamsema Rais Magufuli ambae kwao alikuwa mkombozi.
Kitendo cha Rais Magufuli kuleta nidhamu serikalini tayari ni neema maana watu watahudumiwa ipasavyo na hakika watu walihudumiwa ipasavyo, Umeme ulikuwa stable na Umeme usipokatika unatumika na watu wote na ukiwa stable faida twapata sote.
Aliwaachia wamachinga uhuru wa kutengeneza vipato vyao vya halali na wakapata hela kwa kazi za halali kwa hakika Wamachinga walimpenda Rais Magufuli kwa hilo,na kwa ujumla hatuwezi kusema hakuna alieneemeka kiuchumi!
Rais Magufuli alijenga Reli ya Umeme kwa faida ya Watanzania,Rais Magufuli alijenga masoko Kila Wilaya Tanzania mzima kwa faida ya Watanzania,sio kwa faida yake,Rais Magufuli alijenga Bwawa la Umeme la Mwalimu Julius Nyerere kwa faida ya Watanzania,Rais Magufuli alihamisha makao makuu ya Nchi kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa faida ya Watanzania.
Leo atanangwa juu ya covid lakini twende ndani turudi nje mzee alifanya maamuzi sahihi juu ya lile suala,hilo gonjwa la corona tutaishinalo kama mafua na ukimwi tu hata huko nje sasa wanaishinalo.
Rais Magufuli hakukataa chanjo ila alitaka uhakika wa chanjo hizo kama ni salama kwanza,hii ni kwa faida ya Watanzania,yeye kama mkemia nae alitaka kujiridhisha,sio kupokea tu.
Kinachofanyika sasa ni kutoa ile imani ya utendaji wa Rais Magufuli ndani ya akili za Watanzania!,maana watu wanaamini ule utendaji wake kama ndio kiongozi anavyopaswa kuwa na waliusubiri uongozi kama huo kwa muda mrefu.
Sasa viongozi wa sasa wanajua tutawahukumu kwa kumtumia magufuli kama mfano!..Mfano suala la upatikanaji wa umeme lilivyoanza kusuasua ni mashahidi tosha watu walianza kupiga kelele!,na hii ni kwa sababu tulishazoeshwa huduma hii kutokuwa ya kusuasua katika Uongozi wa Rais Magufuli.
Nimalizie kwa kusema kwamba kuna watu wanachanganya kati ya Uzalendo na Uchawa,Uchawa siyo Uzalendo japo una tabia za kufanana. Awamu ya Tano kulikuwa na wazalendo wengi unaweza ukarejea viongozi kama Balozi Humprey Polepole na wengineo ila hivi sasa kuna chawa wengi.
Unaweza kufanya utafiti wako binafsi,Pumzika kwa amani Rais John Pombe Magufuli,Mzeee JPM apumzike kwa amani,kuna wahuni wanatembelea barabara zako ulizojenga,wengine wanapanda ndege zako ulizonunua na bado wanasema haukufanya chochote.
Enzi zako baba unga wa dona uliuzwa tsh. 800 kwa kilo moja,hivi sasa unga dona ni tsh 1800 hadi 2,200 kwa kilo moja,kazi inaendelea ila ikiendelea hivi kwenye uchaguzi ujao tutafika tumechoka, nimalizie kwa kusema,Uwe na hoja usiwe na hoja utamtaja tu Rais Magufuli,awe alikuziba mdomo au hakukuziba mdomo utamtaja tu,uwe unampenda au haumpendi utamtaja tu,niwatakie heri ya mwaka mpya 2023.
Nikiishia hapa, mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.
Recent Publication;-
-Assessment on the effect of Micro-Financing on Poverty Reduction.