Jina la mdaiwa limekosewa; Je linaweza kubadilishwa na kuendelea na kesi pale ilipoishia?

Joined
Jul 8, 2020
Posts
17
Reaction score
21
Kwanza nitangulize shukrani.

Mwaka 2021 mama yangu alipata ajali sasa akafungua kesi ya madai ikaenda ikafikia mpaka hatua ya utekelezaji kabla ya kufanya utekelezaji ikagundulika kuwa jina la mdaiwa limekosewa kwahiyo ikabidi utekelezaji usimamishwe.

Nilikuwa naomba kujuzwa je inawezekana kusahihisha jina na kuendelea na utekelezaji na kama inawezekana anatakiwa afuate taratibu zipi?

Ahsante.
 
Ngoja nmstue Pascal Mayalla wakili msomi
Mkuu mwanamwana , asante sana kunishtua, japo mimi ni wakili lakini sio wakili msomi.

Jina likikosewa kwenye kesi yoyote inaitwa correctable defects, unatakiwa kitu kinachoitwa chamber summons supported na affidavit ambacho ni kiapo cha kurekebisha jina, kisha inarudi mahakamani jina linarekebishwa tayari kwa utekelezaji.

P.
 
Kwanza nitangulize shukrani.

Mwaka 2021 mama yangu alipata ajali sasa akafungua kesi ya madai ikaenda ikafikia mpaka hatua ya utekelezaji kabla ya kufanya utekelezaji ikagundulika kuwa jina la mdaiwa limekosewa kwahiyo ikabidi utekelezaji usimamishwe.

Nilikuwa naomba kujuzwa je inawezekana kusahihisha jina na kuendelea na utekelezaji na kama inawezekana anatakiwa afuate taratibu zipi?

Ahsante.
Nadhani ingekua rahisi zaidi kusaidiwa kama ungesema kesi hiyo ilikua katika mahakama gani, kwani taratibu na sheria zinatofautiana kutokana na mahakama. Anyway, mimi nitakujibu kadri nielewavyo nikiassume kesi yako ilikua either mahakama ya wilaya, hakimu mkazi ama mahakama kuu.​
Mwaka 2021 mama yangu alipata ajali sasa akafungua kesi ya madai ikaenda ikafikia mpaka hatua ya utekelezaji kabla ya kufanya utekelezaji ikagundulika kuwa jina la mdaiwa limekosewa kwahiyo ikabidi utekelezaji usimamishwe
Hujasema utekelezaji wa nini lakini naamini ulikua ukimaanisha utekelezaji wa hukumu. Hivyo basi nitakujibu kwa angle hiyo.​
Nilikuwa naomba kujuzwa je inawezekana kusahihisha jina na kuendelea na utekelezaji
Ndio inawezekana chini ya kifungu cha 96 cha Sheria ya Mwenendo wa Madai / Civil Procedure Code (CPC). Kwa mujibu wa kifungu hicho, mahakama inaweza kurekebisha makosa ya kiuandishi au kihesabu katika hukumu, maamuzi, au amri wakati wowote. Inaweza fanya hivyo yenyewe tu au kwa maombi ya muhusika katika shauri. Kwa mfano, ikiwa jina la mdaiwa limekosewa katika hukumu au amri, mahakama inaweza kurekebisha kosa hilo ili kuhakikisha haki inatendeka.​
IMG_20240620_165231.jpg

Kifungu cha 96 cha CPC
kama inawezekana anatakiwa afuate taratibu zipi?
Kama nilivyosema hapo juu marekebisho hayo yanaweza fanywa na mahakama yenyewe ama kwa maombi ya muhusika katika shauri. Kwaio kama mahakama aikugundua na kufanya marekebisho hayo, basi unatakiwa kufanya maombi mahakama hiyo hiyo iliyotoa hukumu.

Maombi hayo unayafanya kwa formal application yani Chamber Summons ikiambatana na kiapo (Affidavit) . Nadhani utafute Mwanasheria ili aweze kukusaidia suala hili kiuraisi zaidi.​
 
Mkuu mwanamwana , asante sana kunishtua, japo mimi ni wakili lakini sio wakili msomi.

Jina likikosewa kwenye kesi yoyote inaitwa correctable defects, unatakiwa ku saini document inaitwa affidavit ambacho ni kiapo cha kurekebisha jina, kisha inarudi kwa hakimu, inatoka an addendum ya hiyo hukumu yenye jina sahihi na utekelezaji wa hukumu unaendelea.

P.
Nadhani hujaelewa concern yake msomi.
 
Nadhani ingekua rahisi zaidi kusaidiwa kama ungesema kesi hiyo ilikua katika mahakama gani, kwani taratibu na sheria zinatofautiana kutokana na mahakama. Anyway, mimi nitakujibu kadri nielewavyo nikiassume kesi yako ilikua either mahakama ya wilaya, hakimu mkazi ama mahakama kuu.

Hujasema utekelezaji wa nini lakini naamini ulikua ukimaanisha utekelezaji wa hukumu. Hivyo basi nitakujibu kwa angle hiyo.

Ndio inawezekana chini ya kifungu cha 96 cha Sheria ya Mwenendo wa Madai / Civil Procedure Code (CPC). Kwa mujibu wa kifungu hicho, mahakama inaweza kurekebisha makosa ya kiuandishi au kihesabu katika hukumu, maamuzi, au amri wakati wowote. Inaweza fanya hivyo yenyewe tu au kwa maombi ya muhusika katika shauri. Kwa mfano, ikiwa jina la mdaiwa limekosewa katika hukumu au amri, mahakama inaweza kurekebisha kosa hilo ili kuhakikisha haki inatendeka.​
View attachment 3021520
Kifungu cha 96 cha CPC

Kama nilivyosema hapo juu marekebisho hayo yanaweza fanywa na mahakama yenyewe ama kwa maombi ya muhusika katika shauri. Kwaio kama mahakama aikugundua na kufanya marekebisho hayo, basi unatakiwa kufanya maombi mahakama hiyo hiyo iliyotoa hukumu.

Maombi hayo unayafanya kwa formal application yani Chamber Summons ikiambatana na kiapo (Affidavit) . Nadhani utafute Mwanasheria ili aweze kukusaidia suala hili kiuraisi zaidi.​
kesi ipo mahakama ya wilaya temeke na ni utekelezaji wa hukumu mkuu
 
Ahsa

asante mkuu kwa majibu na ushauri mzuri🙏
 
asante mkuu kwa majibu je hiyo affidavit inapatikana wapi?
Mkuu mwanamwana , asante sana kunishtua, japo mimi ni wakili lakini sio wakili msomi.

Jina likikosewa kwenye kesi yoyote inaitwa correctable defects, unatakiwa kitu kinachoitwa chamber summons supported na affidavit ambacho ni kiapo cha kurekebisha jina, kisha inarudi mahakamani jina linarekebishwa tayari kwa utekelezaji.

P.
 
Mkuu mwanamwana , asante sana kunishtua, japo mimi ni wakili lakini sio wakili msomi.

Jina likikosewa kwenye kesi yoyote inaitwa correctable defects, unatakiwa kitu kinachoitwa chamber summons supported na affidavit ambacho ni kiapo cha kurekebisha jina, kisha inarudi mahakamani jina linarekebishwa tayari kwa utekelezaji.

P.
NB: Jina la hiyo kampuni daiwa lilikosewa tangu kesi inaanza na ilikosewa herufi moja tu na ile nadhani ni summons(kama sijakosea) iliyopelekewa hiyo kampuni daiwa ilikuwa na makosa hayo. je kwa hapo inawezekana kuendelea na utekelezaji wa hukumu maana makosa hayo yalitokea tangu mwanzo wa kesi mpaka mwisho ndio ikagundulika kosa hilo la jina?...asante
 
Basi nimeshakujibu.

Hukumu ilisha toka?
 
Kisheria, kunapotokea kosa lolote dogo, linarekebishwa bila kuathiri hukumu.

Kukotokea kosa kubwa, defective plant, kesi inatupwa kwa technicalities
P
 
Back
Top Bottom