Jina la mtoto...

ila wanaonekana kama ni waislamu, si vibaya mkamwita Mariamu,Fatma,Khadija.sometimes majina yanakua ni chanzo cha tabia ya mtu
 
washauri kuwa jina linakuja kuwa na athari huko mbele katika mafanikio ya mtoto believe you me!...Hilo jina la Mwajabu sijui maana yake..lakini ajabu zaidi ni hilo la Preta.... wanajua maana yake? je wameshaona akina Preta ni watu wa namna gani?

Nakubaliana nawe Veracity, jina huwa lina-impact kubwa sana katika maisha ya mtu. Kuna mtu alimpa jina mtoto wake wa kiume "Ikabodi" lenye maana ya utukufu wa MUNGU umetoweka (wasomaji wa Biblia mnafahamu habari hii kwa watoto wa Kuhani Eli) na mtoto huyu akakua na akawa kama zezeta maana utukufu wa MUNGU umetoweka.

Wakati nikiwa Sekondari kulikuwa na wasichana wawili darasa langu la nyuma (shule yetu ilikuwa mchanganyiko as I am a male) waliokuwa na akili sana na tabia njema pia, na mtoto wa kaka yangu mmoja nikampa jina la mmoja wa hao wasichana na impact nimeiona huyu mtoto is also so bright.

Kwahiyo unapochukua jina mahali fulani na kumpa mtoto wako ni vyema kuangalia tabia za huyo mtu japo kunaweza kukawa na tofauti kidogo toka kwa mtu na mtu wenye jina sawa.
 
Hakuna kuzaa mtoto mpaka mhakikishe mnaweza kukubaliana angalau jina.
 
Watu wengine wanapenda kujitafutia matatizo kwenye ndoa zao. Waachane na hayo majina mawili, kila mtu aandike majina matatu anayoyapenda katika karatasi wayachanganye na mmoja wao achague kikaratasi chenye jina moja katika hivyo vikaratasi sita na jina likalochaguliwa la kwanza ndiyo liwe jina la mtoto.
 

hahaha yako hii kali
 
kwani mwajabu maana yake ni nini? labda wale waislamu watuelezee

Je, kama angeitwa Wonder (Wanda), ingelikuwa jina baya?

Anyway kimsingi kwa watu wenye upeo mzuri huhakikisha wanawarithisha watoto wao au vizazi vya tamaduni zilizopo ndani ya mila zao. Kati ya hizo tamaduni ikiwa ni pamoja na jinsi ya kuwapatia watoto majina, jinsi ya kupika vyakula vya kiasili nk.
Ukitaka kujua athari ya kukosa urithi wa utamaduni nenda kawaangalie wale wamarekani weusi ambao wanahangaika kutafuta asili zao.
 


charity???
si ndio atakuwa anagawa mpaka basi...
ha ha ha.
 

Hili laweza kuwa jawabu kwa tatizo lao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…