Jina la Tanganyika kupewa wilaya ni dharau kwa jina hilo tukufu

Jina la Tanganyika kupewa wilaya ni dharau kwa jina hilo tukufu

Ni bora wilaya hiyo ikabalishwa jina haraka sana. Tanganyika ni nchi, ipo haijafa kama ilivyo zanzibar. Eneo dogo hilo kulipa jina tanganyika ni kuikosea heshima nchi ya Tanganyika, hata kama kisiasa haipo lakini ipo, ndio hii inayoitwa Tanzania Bara. Ndio maana kuna chama cha wanasheria Tanganyika, chama cha madaktari Tanganyika bado vyama hivi vya kitaaluma vinatukuza Tanganyika
 
Uko Mkoa unaitwa Tanga ni kifupi cha Tanganyika na huu mkoa ndio uliozaa jina la nchi ya Tanganyika,jina Tanga(Tanja),inasemekana ni jina la asili ya Kiajemi(Iran), iikiwa na maana ya Shamba, kwa hiyo maana ya Tanganyika ni Shamba na nyika(pori).Ña pia liko.kabila mkoani Tanga,shamba wanaita Tanga.
 
Hata kule Mlimba Morogoro kuna eneo linaitwa Tanganyika Masagati. Kuna machungwa matamu balaa!! Vipi huko Tanganyika ya Katavi, kuna vitu gani vitamu?
Uko mkoa pia unaitwa Tanga,na kuna eneo ndqni ya mkoa huo,kunaitwa Tanganyika.Inasemekana neno Tanga maana yake ni shamba ni neno la kiajemi(Iran). Kwa hiyo Tanga(shamba) na nyika ni pori. Lipo kabila pia la mkoa wa Tanga, wabondei, shamba wanaita Tanga.
 
Wakuu,

Nimeshangaa hivi karibuni kujua kwamba kuna wilaya huko MKOA WA KATAVI inaitwa WILAYA YA TANGANYIKA.
Yaan, JINA TUKUFU la TANGANYIKA limedharauliwa hadi kupewa wilaya?

Ina maana tumeshamiria kabisa kuiua TANGANYIKA?

CC: Pascal Mayalla
Hakuna tatizo kabisa, tena badala ya kulaumu ulipaswa kupongeza angalau Tanganyika inasikika.

Tanganyika haiwezi kufa kwasababu ipo ina exist , eneo lipo milele, kitu ambacho hakipo ni ile status ya Tanganyika nchi, haipo, na jina tuu Tanganyika limegeuka na kuwa Tanzania Bara.
P
 
Soma historia yenu kabla ya kuanika ulivyo mweupe hapa.

Hiyo wilaya Ipo Kabla nchi yenu haijulikani kama ni nchi. Matter of fact, nchi ya Tanganyika ilikopa jina lake huko and not the other way around.

Congo kuna eneo linaitwa Tanganyika kwa sasa ni Jimbo Tanganyika ambalo lilikua linafika hadi huku Tanzania ya Leo Kabla ya mipaka ya mkoloni.

Kadhalika ziwa Tanganyika linaitwa hivyo hivyo Kabla hata wakoloni hawajafika.

Siku nyingine nitakueleza waroma walivyolikuza hilo jina na hatimaye kuwa jina la nchi kabisa.
 
Upo sawa kabisa,Na pale mtu anapotaka kuzungumza jambo kuhusu Tanzania bara ni vyema atumie Tanganyika,kama vile wenzetu hawatumii Tanzania visiwani Wanatamka Jina la nchi yao,maana kusema tanzania visiwani hata Ukerewe na ukara ni visiwa vya Tanzania..
 
Wakuu,

Nimeshangaa hivi karibuni kujua kwamba kuna wilaya huko MKOA WA KATAVI inaitwa WILAYA YA TANGANYIKA.
Yaan, JINA TUKUFU la TANGANYIKA limedharauliwa hadi kupewa wilaya?

Ina maana tumeshamiria kabisa kuiua TANGANYIKA?

CC: Pascal Mayalla
Kwani Tanganyika ni ipi?
 
Wakuu,

Nimeshangaa hivi karibuni kujua kwamba kuna wilaya huko MKOA WA KATAVI inaitwa WILAYA YA TANGANYIKA.
Yaan, JINA TUKUFU la TANGANYIKA limedharauliwa hadi kupewa wilaya?

Ina maana tumeshamiria kabisa kuiua TANGANYIKA?

CC: Pascal Mayalla
Hii nchi inafaa irudishiwe jina lake la kihistoria kabla ya ujio wa wazungu. Zenjbar = Bara la wazenji.
 
😁😁😁 umenikumbusha mbali sana, hiyo Wilaya ya Tanganyika kwanza makao makuu yake yapo Mpanda. Mwaka 2018 kuna research nilikuwa nafanya nikaenda huko, daaah pako hovyo sana kulikuwa na kambi ya wakimbizi, niliishia sehemu inaitwa Mishamo nikatembea vijiji kadhaa nikarudi maana sikuona hata lodge za kulala
 
Back
Top Bottom