Jina la "Utopolo" linapotea kwa kasi mtaani

We ndio unazidi kulipromote
 
Kwanza wengi wanaolishangaa jina la makolo ni washamba tu.

Watoto wa mjini wanapowaingiza mjini wakuja baada ya kupigwa wale waliopigwa huwa wanaitwa makolo,uliza matapeli hilo ni neno walilolitumia tangu na tangu na hadi sasa.Washamba wa mjini wanaliona ni neno jipyaaaaaa na kulishadadia wakati ni neno la zamani sana.

Washamba wa mjini hasa wa utopolo wanadhani hilo neno limeletwa na msukule.

Teh teh teh tehhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh
 
Nikupe tofauti ya Makolo na Utopolo?

UTOPOLO: Ni Jina lililotokana na Mwanayanga kindakindaki lililotamkwa kwa hisia dhidi ya Uwezo wa Timu ya Yanga. Jina hili limekuwa ni msamiati mpya kwenye Lugha ya kiswahili kwani hata wasiofatilia mambo ya Mipira unapofanya jambo lisiloeleweka watakwambia "HEBU WACHA UTOPOLO WAKO".

MAKOLO: Ni Jina la kulazimisha lisilotokana na Mwanasimba bali Yanga kuwalazimisha Simba walipokee. Hili Jina halijabeba hisia yoyote zaidi ya kuforce likubalike.

Hivyo UTOPOLO ni Jina litakaloishi kizazi na kizazi likifuatiwa na Vyura FC, Gongowazi na Ndala. Majina mengine kama Chaneta FC, Lialia FC, Wakimataifa, Manyani FC, Misukule FC, Vibwengo FC, CAS FC, KARIA FC, IRIZAR FC, WAMADIMBWINI FC, GSM FC n.k. haya yote yamepotea na yatapotea.
 
Umesahau Mama Jay FC
 

Mbona lipo sana hadi Google na Wikipedia?

 
Sasa hapa jf naamin kuwa tuna share mawazo na watoto wa juzi ,neno kolo kwa watu waliozaliwa chini ya 1995 kwao sio geni Ila kwa wale wa 2000 kuja 2021 wataona ni kitu kigeni .

Kuna maneno Kama kolo, sakala ,dunya,na mengine kibao ni maneno yaliopitwa na wakat yalishatumika Sana huko mwanzoni.

Ila neno utopolo kamwe halitakuja futika kwanza mlijipa wenyewe alafu ni neno la kihehe yaan kibantu pure so mtaishi nalo Sana , niamin mm neno kolo ndio linaenda kufa kifo Cha mende ,kwanza Wana simba hawajawah lichukia Zaid na wao wanajiita wazwaz maana wanajua halina madhara na soon linaenda kufa kifo heavy
 
Ulivyokuwa mtopolo hata hujui kwa thread hii ndiyo unazidi kulikoleza. UTOPOLO OYEEEEEEE!!!!!
 
Mke wangu shabiki wa utopolo
Cha ajabu tuna mtoto mdogo jana kajikojolea mama ake akamwambia

Heeee mbona unamambo ya utopolo mwanangu

Nilicheka sanaaa ndgu zangu
Hilo jina halichuji limekaa mahala pake
 
TURUDI NYUMA: Kuna timu ILIJITOA UFAHAMU NA KUJIFANYA NI YA KIZUNGU NA KUDHARAU ASILI YAKE KWA KUJIITA" SUNDERLAND". SERIKALI IKAPIGA MARUFUKU UJINGA HUO NA KUTAKA MAJINA YENYE ASILI YETU, NDIPO TIMU HIYO IKATOKA USINGIZINI NA KUBADILI JINA KUWA SIMBA. WAKATI HUO, TIMU NYINGINE ILIRINGIA ASILI YAKE KWA KUJIITA "VIJANA CHIPUKIZI WA KIAFRIKA WA DAR ES SALAAM ( DAR es Salaam Young Africans). NI AIBU TIMU KUFUNDISHWA NA SERIKALI KURINGIA ASILI YAKE!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…