Nikupe tofauti ya Makolo na Utopolo?
UTOPOLO: Ni Jina lililotokana na Mwanayanga kindakindaki lililotamkwa kwa hisia dhidi ya Uwezo wa Timu ya Yanga. Jina hili limekuwa ni msamiati mpya kwenye Lugha ya kiswahili kwani hata wasiofatilia mambo ya Mipira unapofanya jambo lisiloeleweka watakwambia "HEBU WACHA UTOPOLO WAKO".
MAKOLO: Ni Jina la kulazimisha lisilotokana na Mwanasimba bali Yanga kuwalazimisha Simba walipokee. Hili Jina halijabeba hisia yoyote zaidi ya kuforce likubalike.
Hivyo UTOPOLO ni Jina litakaloishi kizazi na kizazi likifuatiwa na Vyura FC, Gongowazi na Ndala. Majina mengine kama Chaneta FC, Lialia FC, Wakimataifa, Manyani FC, Misukule FC, Vibwengo FC, CAS FC, KARIA FC, IRIZAR FC, WAMADIMBWINI FC, GSM FC n.k. haya yote yamepotea na yatapotea.