Jina langu "FATAKI" linanigharimu....!

Konakali

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
1,533
Reaction score
266
Nina umri wa miaka 36 sasa, na jina langu halisi ni "FATAKI". Sasa kutokana na matangazo yanayotolewa na taasisi mbalimbali zinazohusika na haki za binadamu, ukimwi, nk, nimeshindwa kumpata mwanamke wa kuishi naye kwa kuwa jina langu limeharribika katika jamii kutokana na matangazo haya...! Kila nikimtokea mwanadada na kujitambulisha kwa jina langu halisi, "Fataki" hushtuka na ghafla naanza kuona interests zake zinaondoka na hatimaye kumkosa....! Please Great Thinkers, help me on what should I do kwa sababu umrri unakwenda...! Je, naweza kuwashitaki taasisi hizi?
 
Kwani tangu lini katika matangazo FATAKI kafanikiwa kuibua demu?
 
Miaka 36? Bado sana....endelea kuvuta subira mkuu! Hawakukimbii kwa sababu ya jina lako, wanaukimbia umri, bado mdogo utaweza kulea familia?
 

usipate sida konakali, wapo mafataki wa kike!unaweza kuibuka na mmoja wapo.
 
mmh kwan matangazo ya fatak yameanza lin?wakat upo 33 au 34 yalikwepo ?na wakat uo pia ulishndwa kuwapata cz ya nomino yako??
labda utakuwa unaitwa ..fataki ..sasa wewe tumia jina la kwanza tu..may b JOHN..FATAK USIIITUMIE..au labda TABIA ZAKO ZIMEFANANA NA NOMINO YAKO NDO MANA WATU WANATOKA NDUKI?aujampata wa kukupenda kweli bwana jina si issue....!!!
 
Badilisha jina:A S 112:
Nimefikiria hili lakini nilidhani huenda akija kugundua baadaye kuwa nimebadilisha jina kwa lengo hili huenda akanikimbia vilevile...! Au hata asiponikimbia, lakini nikiteleza kibinadamu huenda ikawa vigumu kunielewa....! Kwa vyovyote matangazo haya yameshaniwekea mazingira magumu sana katika maisha yangu...!

Miaka 36? Bado sana....endelea kuvuta subira mkuu! Hawakukimbii kwa sababu ya jina lako, wanaukimbia umri, bado mdogo utaweza kulea familia?
Please mkuu...! This is not a joke, but I am very serious....! Do you think 36 years person is still young, provided he/she is sound mind? Please, help me...!

usipate sida konakali, wapo mafataki wa kike!unaweza kuibuka na mmoja wapo.
Mimi sio fataki kwa fani, bali kwa jina tu...! Hivyo, nisingependa niishi na fataki unayemaanisha wewe...! Tafadhali, nisaidie...!
 

Next time ukimtokea mwanamke mwambie kuwa unaitwa MCHALUKO. Ukiona jina bado linaleta tabu basi jitambulishe kwa jina la KIMEO. Ukiona maijna yote bado yanagoma nakushauri uende ukaishi China, huende kule China jina la fataki likawa na maana nzuri tu. Mfanao mzuri ni lilejina la mwanamziki KIDUMU kutoka nchi jirani. Hapa bongo jina hilo lina maana tofauti na kule kwao. Ukita kujua maana ya kidumu muulize maria roza au nyamamyao
 
kweli hata mie ungenitokea na hilo jina ningepoteza nia,kwanza mdada serious anakuona kama unamtania vile haamini kuwa hilo ni jina lako.kweli inabidi utafute jina la kujitambulisha ila pia unaweza kumwambia mdada unaitwa John mara mkiwa naye anatokea mtu anayekujua anakuita FATAKI hapo dada lazima aingiwe na hofu,kazi unayo kaka yangu.
 
Naomba mssada wako binafsi dada yangu....!
 
Naomba mssada wako binafsi dada yangu....!

msaada upi zaidi ya huo niliokupatia.
huo ndio msaada niliojitahidi kukupatia ukijumlisha na ya wengine unaweza kupata japo nusu ya suluhisho la tatizo lako.
kama huna tabia za kifataki itakuwia rahisi kidogo kusolve issue
 
Konakali
Pole kwa hicho kisanga,lakini kama walivyotangulia kusema wengine badilisha jina, kwakuwa naamini una majina mawili au matatu tumia mojawapo,vinginevyo ni ngumu sana mtu kukuamini hata kama amekupenda coz halisound vzr kutokana na maudhui linayofikisha thru media.
 
Queen;
Kila anayekutokea huwa unajenga nia naye, assuming jina lake siyo Fataki?
 

mimi siitwi FATAKI queen.
 

Pole sana Konakali... Hujampata tu anayekupenda ki ukweli hasa ikiwa tabia yako ni tofauti sana na tafsiri halisi ya FATAKI.

Kubadilisha jina haitasaidi, ila ukiaza mahusiano tumia majina yako mengine kwa muda kisha baada ya penzi lenu kukomaa waweza mwambia kuwa hilo pia ni jina lako.
Kwakuwa atakwisha ijua tabia yako, hawezi fanya maamuzi kutokana na jiana ila na mwenendo wako mzima.

Uumri wala usikuogopeshe....Usijeangukia pabaya.
 
Mbona mahakama bado zipo Tanzania, kwazo waweza kubadilisha jina. Vilevile waweza kuiomba mahakama kulazimisha hiyo taasisi kutotumia jina hilo katika matangazo kama utathibitisha kihalali kuwa utumiaji wa hilo jina katika matangazo unakuathiri katika jamii. Wapo wanasheria wa kujitolea kama huna uwezo wa kufungua kesi kwa kutumia wakili. Kama unahitaji nitumie email via indumeyene@jamiiforums.com
 
msaada upi zaidi ya huo niliokupatia.
huo ndio msaada niliojitahidi kukupatia ukijumlisha na ya wengine unaweza kupata japo nusu ya suluhisho la tatizo lako.
kama huna tabia za kifataki itakuwia rahisi kidogo kusolve issue
Waweza kujitolea kunizibia gepu hili mamy....!

What if yeye akaanza kujua jina langu lililojificha kabla mimi sijamsimulia kisanga hiki; mfano nikipishana na wanaonifahamu, then wananitaja FATAKI...!

mimi siitwi FATAKI queen.
Mkuu mbona unataka kunizibia riziki yangu? Hahahah......! Kumbe mafataki wa fani wapo.....! Lakini mimi ni kwa jina tu...!

Well noted...! Lakini hapo kwenye red, unadhani ni kwa muda gani naweza kuficha jina hili? Je, ikitokea kwa namna moja ama nyinigine akajua kabla sijaweza kumweleza ukweli, atanichukulieje?

Asante, lakini jamii si bado wataendelea kunitaja kwa jina hili? Hasa watani nitakabiliana nao kivipi? Aidha, msaada wako huenda ukaleta matunda, japo kwa muda mrefu...! Hapo kwenye red, nitadhibitishaje?

Kweli wewe FATAKI hadi leo bado hujampata?
Kwani kuchelewa ndio ufataki mkuu? Kwa kweli sikuelewi...! Aidha, mimi niko :confused2:.
 
What if yeye akaanza kujua jina langu lililojificha kabla mimi sijamsimulia kisanga hiki; mfano nikipishana na wanaonifahamu, then wananitaja FATAKI...!

Konakali,
mwanzoni unavyomwaproach ni vyema ukamweleza ukweli halisi na jinsi unavyojiskia kwa sasa kuhusu jina lako,naamni solution pekee ni ukweli maana utakuweka huru,na kama anakupenda atakuamini.Otherwise,kila la kheri:A S thumbs_up:
 
Naomba mssada wako binafsi dada yangu....! .

Mmh.Ngashituka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…