Sisi tunaitana majina yetu ya kwanza, na watoto siku wakitaka "kukata kiu" utasikia wanakuita jina lako...... huwa tunacheka tu.
Ila sasa wazazi huwa hawajisikii vizuri tunapoitana majina yetu mbele yao. nakumbuka kuna siku mama yangu aliwahi kuniuliza kwa nini namwita mume wangu kwa jina la kwanza, nikamjibu ndo nimezoea hivyo, akasema sio vizuri. mama mkwe wangu pia aliwahi kumwambia mume wangu kuwa mimi nina watoto, kwa hiyo aniite mama fulani, akamjibu hawezi. kwa hiyo inabidi watuvumilie tu