Jinai ya kudanganya taarifa za Cheti cha kuzaliwa cha mtoto

Zemanda

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2021
Posts
10,999
Reaction score
23,540
Ni muda muafaka sasa kwa jamii kuliona hili tatizo ambalo linakua kwa kasi na litakuja kuwa na madhara makubwa sana siku za baadae.

Linapokuja swala la kukemea maovu tusiwe na double standards au kusema kuna uovu wenye nafuu na usio na nafuu, uovu ni uovu tu.

Nazungumzia tabia ya wanawake wa sasa kuwa na mahusiano na mtu zaidi ya m’moja,kubeba ujauzito nje ya ndoa, na kutengeneza taarifa za uongo kuhusu baba wa mtoto kwasababu zao binafsi ambazo hazina msingi wowote wala faida kwa mtoto na jamii inayomzunguka.

Mwanamke anaweza kujihusisha na wanaume zaidi ya watatu kwa wakati m’moja kwa makusudi zake na usiri kinyume na maadili ya kiafrika na kinyume kabisa na mafunzo ya kiimani. Then ikatokea akapata ujauzito atakwenda kutengeneza nakala tatu za cheti cha kuzaliwa cha mtoto zenye taarifa tofauti za wanaume hawa na kumuonyesha kila m’moja kuwa ndie baba mzazi wa mtoto huyo.

Hii tabia na hali imeanza kuzoeleka na jamii inachukulia ni jambo la kawaida tu na halina madhara yoyote bila kujua balaa au hatari ambayo tunaelekea au tunakuja kukabiliana nayo siku si nyingi kutoka sasa.

Hiki kitendo si tu kwamba ni kinyume na maadili ya kijamii na maadili ya kiimani ila pia ni kosa kubwa kisheria na ni jinai kubwa sana kwa mujibu wa sheria ya usajiri wa vyeti vya kuzaliwa na vyeti vya vifo (Cap. 108,R.E 2002) ambapo kutoa au kutengeneza taarifa ya uongo wakati wa kusajiri taarifa za mtoto au kifo ni kosa kubwa ambalo unaweza kufunguliwa kesi yenye adhabu ya fine au kifungo(miaka 2) ama vyote kwapamoja.

Kudanganya taarifa za uzazi na utambulisho wa baba mzazi wa mtoto katika cheti cha kuzaliwa kuna madhara makubwa sana na yasiyoweza kurekebika ikishatokea siku za baadae kama ifuatavyo:

Madhara kwa mama wa mtoto

Mashitaka ya uhalifu
: mzazi aliyetengeneza taarifa za uongo katika cheti cha mtoto ana risk kufunguliwa mashitaka ya uvunjifu wa sheria kwa kutenda jinai ya kufoji nyaraka ya serikali na kudanganya mamlaka ya usajiri wa nyaraka muhimu ya kiserikali(Section 23 of the Births & deaths Registration Act) na kuwekwa hatiani ikiwamo kufungwa. Na kushitakiwa kwa mashitaka ya kujipatia mahitaji na fedha kwa njia ya udanganyifu wa kufoji nyaraka muhimu ya uzazi (Fraud chargers)na kutakiwa kulipia fidia.

Kujiwekea rekodi mbaya kisheria: taarifa za kufoji nyaraka zinaweza kuja kuwa kikwazo siku za mbeleni na zikatumika kukwamisha mambo muhimu ambayo yanahitaji hati safi ya kiraia.
Kupata kesi ya kujibu mahakamani (Fraud charges): muhanga/wahanga wa kubambikiwa taarifa batili anayo haki ya kufungua mashitaka mapya mahakamani akishitaki kutapeliwa na kudai fidia ya gharama zote walizogharamika katika malezi na matunzo ya mama na mtoto ikiwa tu wataweza kuthibitisha ushahidi(risiti) wa kufanya malipo hayo ili muhusika aweze kurejesha kiasi chote kama ushahidi utakavyoonyesha.

Kujiweka hatarini kimaisha: kufoji cheti cha mtoto kunaweza kupelekea matukio ya mauwaji au kudhuriwa na muhanga kama atashindwa kuipokea taarifa vizuri na hivyo mama wa mtoto anakuwa katika hatari ya kudhurika na kushambuliwa kimwili na pengine kupoteza maisha yake.

Kuwajibika na malezi ya mtoto pekee yake: kufoji taarifa za cheti cha kuzaliwa cha mtoto kutamfanya baba mzazi kutotaka kushiriki malezi ya mtoto moja kwa moja kwa kuhofia kupewa mahitaji ya uongo lakini pia kujitoa kwa baba aliyesingizwa kutasababishwa kusitishwa kwa matunzo ya mama na mtoto na hivyo mzigo wa

Madhara kwa mtoto:

Kuharibu haki za mtoto (Child right Violation):
sheria za kimataifa (UN Convention on the child’s rights) inampa kila mtoto haki ya kuwatambua wazazi wake wote wawili na ndugu wa familia kila upande. Kufoji nyaraka na kuweka taarifa za uongo ni kumnyima mtoto haki ya kujua taarifa muhimu juu ya baba yake na ndugu zake upande wa baba yake. Hii ni violation ya haki ya msingi ya mtoto na kumnyima haki mtoto.

Urithi na mali za baba mzazi: taarifa za uongo juu ya baba mzazi katika cheti cha mtoto zinaweza kuleta madhara katika maswala ya urithi wa baba yake mzazi endapo mtoto atatakiwa kuthibitisha kwenye mamlaka zinazohusika na mirathi kuwa yeye ni biological child au anaweza kurithishwa mali za ukoo usiomuhusu wakati ndugu wa familia walistahiki kupewa mali kwasababu mwenye mali hakuwa na mtoto.

Kumkosesha mtoto utambulisho rasmi (loss of true identity): mtoto hukuzwa akiwa na utambulisho batili na wa uongo kuhusu ukoo wake na familia ya baba yake anapotokea na hii huwa ni chanzo kikubwa cha msongo wa mawazo na sonona huko mbeleni.

Utata wa uraia na utaifa: kama baba anayetajwa katika cheti sio mzawa wa taifa husika hii inaweza kumletea mtoto migogoro siku za baadae katika maswala ya ajira, nafasi za uongozi, passport,uria halali na hata umiliki wa rasilimali kama ardhi.

Matatizo ya kisaikolojia: mtoto ambaye amegundua taarifa halisi za baba yake mzazi huweza kupatwa na trauma ya kudumu kiakili, kukosa uaminifu na mama yake na hata ndugu waliomlea na kuharibu kabisa mahusiano nao, kumfanya achukie uwepo wake duniani na kukosa utambulisho wa asili yake ya kweli yaani baba yake.

Madhara kwa mwanaume aliyesingiziwa:

Kumpa majukumu mwanaume asiyehusika: mwanaume ambaye hakuhusika na uzao wa mtoto aliyepewa atawajibika na gharama zisizomuhusu. Hii ni kinyume na haki za kiraia na kijamii kwa kubebeshwa gharama ambazo hazimuhusu hata kidogo.

Migogoro ya kifamilia: kufoji taarifa za cheti cha mtoto kunaweza kuleta migogoro katika familia ya mwanaume asiyehusika na uzazi wa mtoto aliyebambikiwa.

Matatizo ya kisaikolojia: kuna hatari ya mwanaume aliyebambikiwa taarifa za mtoto kupatwa na hasira na kufanya maamuzi ya hatari kama kushambulia mwanamke aliyemsingizia,majuto na maumivu anapogundua kuwa yeye si baba halali wa mtoto na kuwa na majuto ya kulipia gharama za muda mrefu kwa mtoto asiyemuhusu.

Kukatishwa mahusiano na mtoto aliyemlea: ukweli wa taarifa za uongo ukifahamika mtoto atarejeshwa kwa baba yake mzazi na kumuacha baba aliyesingiziwa maumivu na upweke kwa kuondokewa na mtoto ambaye alimpenda akijua ni damu yake.

Madhara kwa serikali na jamii:

kufoji cheti ni jinai (Fraud): cheti cha kuzaliwa ni nyaraka rasmi ya kiserikali kama vyeti vya chuo, hati ya Kiwanja/nyumba, kadi ya gari na zinginezo rasmi. Kufoji taarifa za hizi nyaraka ni kosa kubwa kisheria ambalo lina adhabu ya kifungo na faini likifikishwa mahakamani.

Kupungua kwa creditibility ya mamlaka ya usajiri: mamlaka za usajiri kama Brela zimeaminiwa kutoa taarifa sahihi kuhusu raia. Mwenendo na uwepo wa vyeti vyenye taarifa batili vinaweza kushusha hadhi ya mamlaka hii na kuonekana ni ya kitapeli na wanatengeneza taarifa zisizo na uhakika.

Uharibifu wa taarifa za kiserikali: mwanamke anayetengeneza taarifa za uongo na batili za cheti cha mtoto sio tu anatenda jinai ila anaongeza msururu wa takwimu za uongo katika kumbukumbu muhimu za kiserikali na kijamii.

Kuongezeka kwa migogoro ya kisheriangezeko la vitendo vya kufoji vyeti ina maanisha ongezeko la migogoro isiyo na maana siku za baadae na kuipa kazi ya ziada serikali katika kutatua migogoro inayotokana na jinai ya makusudi ya kufoji vyeti vya kuzaliwa.​

Uharibifu wa maadili na hadhi ya mama kijamii: matendo ya kufoji vyeti sio tu yanaharibu uaminifu ndani ya jamii lakini yanafanya wanawake wa kisasa kuonekana ni tatizo na kuchangia kwa sehemu kubwa kuharibu ustawi wa jamii na taasisi kuu ya ndoa. Familia zinapoteza ustawi mzuri kwasababu ya kukosekana mahusiano imara upande wa baba.

Kuhitimisha nimesema kuwa, kila mama anawajibika na taarifa anazotoa kumhusu baba wa mtoto wake na hivyo hitilafu zozote zitakazotokana na udanganyifu anaofanya ni yeye ndie atakae wajibika nazo kama chanzo na si baba wa mtoto aliyefichwa kupewa lawama yoyote. Ni wajibu wa mama kuandika taarifa sahihi na za ukweli za mwanaume aliyezaa nae mtoto kwenye cheti hata kama wamekorofishana na hawana maelewano au kuchukiana. Kinyume chake ni kutenda jinai ya makusudi na kusababisha madhara kwa jamii nzima.
 
Kama hayo angekuwa anafanya mwanaume tayari sheria ingekuwa ilishatungwa muda mrefu ili kumpiga faini na kumfunga jela.

Ila kwa kuwa ni mwanamke watasema alisababishiwa kutenda hayo.
 
😂😂😂 Umeona mzee? Tukiwachekea hawa wataanza kutuletea umarekani na maswala ya child support waanze kitufunga jela. Ni kuwa wakali tu kuanzia sasa upuuzi wao uwe na kikomo.
 
Back
Top Bottom