Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Mabaki ya nyumba iliyobomolewa na lori la mizigo Friday, September 11, 2009 6:59 AM
Jinamizi la malori makubwa ya mizigo kuvamia nyumba za watu kwenye maeneo ya Kimara Mwisho limezidi kupoteza maisha ya wakazi wa eneo hilo safari hii lori kubwa lililokuwa limeegeshwa pembeni ya barabara lilivamia nyumba usiku na kuua mtu mmoja aliyekuwa amelala. Picha za ajali hiyo mwisho wa habari hii. Lori lenye namba za usajili T934 ASM lilokuwa na trela namba T885 ASM liliokuwa limeegeshwa katika eneo la Kimara mwisho usiku wa kuamkia jana liliporomoka na kuvunja nyumba iliyokuwa jirani na kuua mtu mmoja na kumjeruhi mwingine.
Aliyefariki alifahamika kwa jina la Salumu Mussa Ndete na majeruhi wa ajali hiyo alikuwa ni Hamis Salumu (28).
Gari hilo lilikuwa limeegeshwa usiku kwenye eneo hilo na dereva ambaye aliondoka zake kwenda kulala sehemu nyingine lakini cha kushangaza majira ya saa kumi na moja alfajiri gari hilo lilijiendesha lenyewe na kuvamia nyumba hiyo.
"Nilisikia mlio kama wa mabomu ya mbagala, nilipoamka na kwenda kungalia nini kilichotokea nilikuta gari kubwa limevamia nyumba yangu" alisema jirani wa nyumba zilizoathirika .
Hata hivyo matukio kama haya yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara katika eneo hili.
"Hii ni mara ya pili ndani ya mwaka huu hivyo sisi wananchi wa eneo hili tunajiuliza kuna nini" alisema mkazi wa eneo hilo, Hamisi Juma.
Wakati ajali hiyo inatokea, marehemu Salum alikuwa peke yake chumbani kwake amelala huku jirani yake Salumu naye akiwa amelala chumbani chumba cha jirani kwenye nyumba hiyo ya kupanga.
Hata hivyo waswahili wanasema mungu mkubwa, Mke wa marehemu Salum na mwanae jioni ya tukio walikuwa wamekwenda kwenye msiba wa mama yake sehemu nyingine na hivyo kunusurika maisha yao.
Ajali kama hii ni ya tano katika eneo hilo katika kipindi cha muda wa miaka 5.
Wakazi wanaoishi karibu na eneo hilo la barabara ya Morogoro wameanza kujiuliza maswali mengi bila majibu.
"Sijui kuna nini maeneo haya labda kuna mashetani" alisema mkazi mmoja wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina la John.
Mwili wa marehemu Salum umehifadhiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. GONGA HAPA KWA PICHA ZA AJALI HIYO
http://www.nifahamishe.com/NewsDeta...he.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3056846&&Cat=1