Jini la vita limejamba EU

Jini la vita limejamba EU

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,611
Jitahidi usome mwanzo mwisho.

Mlipuko wa vita ya Russo-Ukrainian War umeiweka dunia njiapanda katikati ya chagizo linaloendelea la Uviko.

Tayari dunia imegawanyika ambapo NATO chini ya US ina ushirika mkubwa dhidi ya Urusi ambayo hadi sasa inaonekana kuwa peke yake.

US inaingia kwenye vita hii kwa sababu moja kuu ya kulipiza kisasi cha Urusi kudukua matokeo ya uchaguzi yaliyoiangusha Democrat na kuipa Republican ushindi kwa kumuingiza rais Donald Trump Ikulu ya Whitehouse.

Kwa siku moja tu Urusi imeitia kilema cha kudumu Ukraine kiulinzi ambapo maeneo 88 ya kiraia yamelengwa, raia 137 kufa, 380 vilema, 29,000 wakimbizi kwenda ndani ya Urusi yenyewe na wachache kati yao kwenda Poland lakini wakihofu kuwa Poland inaweza kuwa shabaha ya Urusi endapo NATO itapewa ardhi huko. Urusi imeshambulia tokea angani, majini na ardhini kwa wakati mmoja na imedhihiri kuwa Urusi kupigana na Ukraine ni sawa na Afrika Kusini kupigana na Swaziland.

Ukraine inadai madhara iliyopata ni kutokana na silaha zake kuharibu zile za Urusi angani na mabaki yake kuja kuangukia makazi ya watu na makambi ya Ukraine, huku ikitoa takwimu kwamba imejeruhi na kuua idadi ya wapiganaji na watumishi wa Urusi wapatao 443. Yote ni propaganda za vita za Ukraine kwa sababu kwanini hayo hayakutokea ndani ya Urusi?

Maeneo zaidi ya 100 ya ulinzi wa kimkakati yamesambaratishwa ikiwemo mfumo wa ulinzi wa kimtandao (cyber security) kiasi kwamba rais na amiri jeshi mkuu wa Ukraine Mhe. Volodymyr Zelenskyy ametangaza kuacha vita na kuitaka Urusi isitishe vita na kuondoa majeshi yake ndani ya ardhi ya Ukraine, huku EU na NATO vikiogopa na kuamua kutangaza kupitia kinywa cha rais Joe Biden wa US kuwa NATO haitapigana vita ya moto bali ya vikwazo vya kiuchumi.

Madai ya Urusi:

Ukraine inaongozwa toka nje (US)

Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine anatuhumiwa na Urusi kwa mauaji ya kimbari ya miaka 8 sasa na kwamba yeye siyo rais halali aliyechaguliwa kidemokrasia na kwamba serikali yake ni ya mpito tu.

Ukraine inajenga vinu vya Nyuklia (kama US ilizuia Iran na Korea Kaskazini kwanini yeye Urusi asiizuie Ukraine ambayo iko karibu naye kijiografia kuliko Iran na Korea Kaskazini zilivyo na US)

Ukraine iache majimbo yanayotaka kujitenga yajitangazie uhuru kamili (Crimea na Donbass/Donbas)

Urusi tangu 2014 imeunga mkono kujitenga majimbo haya ambayo yamekuwa vitani na Ukraine kwa miaka mi 8 sasa.

Umuhimu wa majimbo yanayojitenga:

Donetsk ni mji mkuu wa Donbas.

Donbas inayolala kwenye bonde la Donetsk na Luhansk ni tajiri kiuchumi, kiutamaduni na kihistoria. Inatoa makaa ya mawe kwa wingi na ina viwanda mama vingi. Ni muhimu kama ilivyo Scotland kwa Uingereza.

Crimea ambayo tayari Urusi imejiungamanisha nayo (annexed to Russia) kama ya kwake (sawa na China inavyodai kumiliki Taiwan na HongKong) ilikuwa muhimu kimataifa kwa mfumo mpya wa dunia mwaka 2014 kama ambavyo Cuba ilikuwa mwaka 1963 au Hungary mwaka 1956.

Urusi inadai kuwa wakazi wa Rasi ya Crimea kwa asilimia kubwa sana wanaongea lahaja ya Kirusi.

Urusi inahitaji majimbo hayo kwa uchumi wake, Ukraine nayo inahitaji majimbo hayo kwa uchumi wake, majimbo hayo nayo yanahitaji uhuru kamili (sovereignty) lakini yakitumia Urusi kama daraja la kufikia ndoto yao hiyo.

Vikwazo:

Kumeibuka mashindano ya kuwekeana vikwazo kati ya washirika wa NATO na Urusi ambapo maeneo yaliyoishaguswa hadi sasa ni sekta za fedha, safari za anga, mabenki, uhamiaji, biashara (matajiri 5 wakubwa wa Kirusi waliowekeza UK mitaji yao imeshikiliwa (assets frozen)) kupitia tangazo la Mhe. Boris Johnson PM wa UK.

Katika kujibu mapigo, Urusi imefunga viwanja 12 muhimu vya ndege za kiraia, imepiga marufuku ndege za UK na washirika wa NATO kuingia Urusi na kutotumia anga la Urusi.

Urusi inategemewa na dunia kwa uzalishaji mkubwa sana wa ngano, gesi asilia, silaha na vileo vya kiwango cha juu duniani, hivyo dunia inaihitaji Urusi kuliko inavyoihitaji Ukraine. Hiki ndicho kinachompa Urusi kiburi na jeuri.

Changamoto:

US enzi ya rais Boris Yeltsin wa Urusi (baada ya kupokea Urusi iliyosambaratika mikononi mwa rais Gor Bachev kupitia sera yake ya mageuzi ya kiitikadi aliyoiita Perestroika) ilikula njama kuua WARSAW PACT ikabakisha NATO. Poland ambayo US inaomba kutumia ardhi yake kwa ajili ya vita hii ilikuwa mshirika wa Urusi kwenye WARSAW PACT, leo Poland imejiposa kwa NATO.

NATO ina washirika EU na Americas, Urusi haina washirika US na EU kwahiyo hivi sasa US kupitia NATO inatumia majirani wa Urusi kuiminya Urusi.

NATO imejitafakari na kuona bora vikwazo kuliko vita vya moto kwa sababu ukimya wa China, Iran, Korea Kaskazini, Syria vimeipa homa kali kwamba huenda wakajiunga na Urusi ambapo tayari ndani ya saa 24 rais Nicolás Maduro Moros wa Venezuela hakuvuta subira bali alitangazia dunia hadharani kwamba yuko upande wa Urusi kwenye vita hii ya RUSSO-UKRAINIAN WAR.

US ni mteja mkubwa sana wa mafuta ghafi na bidhaa za petroli toka Venezuela. Katika mwaka wa 2021 US iliagiza mafuta kwa kiwango ambacho ni mara tatu ya kile kilichoagizwa na Urusi, sababu inaweza kuwa kwamba Urusi inatumia gesi zaidi ya mafuta kwa sababu inaongoza dunia kwa uzalishaji wa nishati ya gesi asilia.

Aidha, kama Iran ikiungana na Urusi ni wazi kwamba wanachama wa OIC hawatakaa kimya kuona NATO ikilipa kisasi kwa Iran na kwamba itabidi OIC wote wawe upande wa Urusi kupitia ndugu yao Iran.

Hofu kuu ya OIC kukaa upande wa Urusi kupitia Iran ni kwamba uamuzi huo unaweza kumuibua Muisrael ambaye atataka amuunge mkono US na kwamba kwa kitendo hicho, ndani ya himaya ya OIC Uarabuni hakutakalika kwa sababu Israel itataka kuipunguzia OIC nguvu humo humo ndani kabla ya kuvuka mipaka kwenda Ukraine kuisaidia Urusi na labda Iran.

Kama Zimbabwe ilivyokuwa mwanachama wa Madola, Israel nayo ni mjumbe kwenye OIC (asiye na kura, bali tu kwa sababu dini ya Kiislamu ni ya pili kwa ukubwa Israel nyuma ya ile ya Kiyahudi Jewish); lakini kimkakati wa ulinzi (kijasusi), kwahiyo Israel ikiungana na US na NATO kupitia mgongo wa Ukraine kuwashambulia majirani zake wa OIC wa Uarabuni ambao ina uadui nao; itakuwa imehujumu ujumbe wake wa OIC kwa kisa tu cha kuzitetea US na NATO.

Kitu pekee ambacho dunia inatakiwa imuombe Mungu kwa bidii kumaliza vita hii ni kwamba Urusi ina teknolojia ya kutengeneza silaha za kibaiolojia za hali ya juu (ambayo US na NATO hawana) alizowahi kumuuzia Iraq; na chanjo ya virusi hivyo anayo yeye pekee duniani (ni siri kali ya kiulinzi), hivyo katikati ya janga la dunia la Uviko-19, kama Urusi ikiamua kutumia silaha hizo za kibaiolojia (virusi) ni dhahiri kwamba dunia itakuwa imefika kusiko. Hii inaweza kuwa ni moja ya sababu za NATO kuahirisha kupigana vita ya moto na kuchagua vita ya vikwazo vya kiuchumi.

Tayari Urusi inadukua mawasiliano ya Ikulu na Idara zote za Ulinzi na Usalama za Ukraine. Ukraine sasa iko mikononi mwa Urusi kwa 100%. NATO inaogopa kuunganisha Ukraine kwenye mfumo wake wa ulinzi na pia ule wa kiserikali (zikiwemo Ikulu za NATO) kwa kuhofia Urusi kudukua. Hivyo Urusi inadhibiti mfumo wa mawasiliano yanayoingia na kutoka Ukraine na kufanya NATO kukata mawasiliano na Ukraine. Vita ni mawasiliano kwa sababu ndiko amri za kivita zinakopatikana.

Afrika imeshikwa pabaya kwenye gogoro hili kwa sababu ni kama vile EU iliota kwamba lazima Mrusi ataishambulia Ukraine; ikajiwahi kufanya mtaguso na AU (#EUAU) wiki iliyopita kutoa furushi (package) la fursa za uwekezaji ndani ya AU (Blackmail) hivyo Afrika italazimika kufunga kinywa chake kwenye vita hii kama Bi. Harusi.

Ni dhahiri sasa kwamba viongozi wa Afrika wamepata kisingizio kingine cha pili baada ya Uviko-19; cha vita ya Urusi na Ukraine; cha kuegemezea madai yao ya kushindwa kukuza chumi zao na kushindwa kutekeleza ilani zao za uchaguzi, wanashindwa kujuwa kuwa changamoto ni mtaji pia.

UN iko wapi kwenye hili?

Namna gani nzuri ya kumaliza fitna ya kihistoria kati ya Urusi na US

Ili kuondoa mvutano kati ya Superpowers wawili wa dunia (US na Urusi) ni kwa Urusi kuamua kuwa mwanachama wa EU, hii itasawazisha (neutralize) nguvu za US kwa sababu ndani ya EU kuna wanachama wa NATO pia hivyo US inapoitishia Urusi kwa kutumia NATO basi wanachama wa EU ambao pia ni washirika wa NATO hawatamkubalia US badala yake watalazimika kumtetea Urusi ambaye ni mwana EU mwenzao (japo siyo mwana NATO)

Kati ya wanachama 27 wa EU, 21 pia ni wanachama wa NATO. Wana-NATO wengine wanne ni waombaji wa uanachama wa EU ambao ni Albania, Montenegro, Macedonia Kaskazini, na Uturuki. Wengine wawili Iceland na Norway wamechagua kuwa nje ya EU, hata hivyo wanashiriki kwenye soko la pamoja la EU.

Wanachama waanzilishi wa NATO ni Ubelgiji, Canada, Denmark, Ufaransa, Iceland, Italia, Luxembourg, Uholanzi, Norway, Ureno, Uingereza na Marekani. Ukraine siyo mwanachama wa EU wala NATO lakini imeshiriki operesheni nyingi za NATO (Urusi naye siyo mwanachama wa EU wala NATO). Aidha, zipo taarifa kwamba Bosnia na Herzegovina, Georgia na Ukraine wameomba kujiunga NATO.

Case Study ya Israel ambayo Urusi ingeiiga.

Hadi mwaka 2021, wanachama sita pekee kati ya ishirini na wawili wa Arab League wameitambua Israel: Egypt, Jordan, United Arab Emirates, Bahrain, Sudan na Morocco. Mauritania ilivunja uhusiano na Israel. Pia dini ya Uislam ni ya pili (19%) kwa kubwa Israel baada ya ile ya Jewish 75%, hii inampa Israel nafasi OIC ili taasisi hii ya kimataifa ya kiislamu iweze kusimamia maslahi ya Uislamu ndani ya Israel ambako kuna uhuru mkubwa wa kuabudu kikatiba. Fursa hii inaiangukia Israel kwa kuwa mshiriki OIC asiye na kura, pia Arab League Israel ana fursa, japo ndani ya moyo wa Israel fursa hizi anazitumia kimkakati ya kijasusi kwa ajili ya ulinzi na usalama wake (kujuwa anavyojadiliwa huko).

Urusi ilitakiwa ijifunze hili toka kwa Israel; kwa kujiunga EU ili iweze kusawazisha (ku-neutralize) nguvu za NATO. Badala yake Urusi ilibuni taasisi ya Eurasian Economic Union (EEU) ambayo ina wanachama 5 ambao ni Jamhuri za Kisovieti za iliyokuwa USSR i.e. Russia, Kazakhstan, Belarus, Armenia na Kyrgyzstan.

©Douglas Majwala,
United Republic of Tanzania,
February 25, 2022.

1645791889423.png

Picha ya juu: Kwa wakati mmoja manowari, ndege-vita na vifaru vya Urusi vikiichakaza Ukraine.

1645791993629.png

Taswira kwa hisani ya google.
 
Urusi wakipigwa msilalamike
Tayari Urusi inadukua mawasiliano ya Ikulu na Idara zote za Ulinzi na Usalama za Ukraine. Ukraine sasa iko mikononi mwa Urusi kwa 100%. NATO inaogopa kuunganisha Ukraine kwenye mfumo wake wa ulinzi na pia ule wa kiserikali (zikiwemo Ikulu za NATO) kwa kuhofia Urusi kudukua. Hivyo Urusi inadhibiti mfumo wa mawasiliano yanayoingia na kutoka Ukraine na kufanya NATO kukata mawasiliano na Ukraine. Vita ni mawasiliano kwa sababu ndiko amri za kivita zinakopatikana.
 
Tayari Urusi inadukua mawasiliano ya Ikulu na Idara zote za Ulinzi na Usalama za Ukraine. Ukraine sasa iko mikononi mwa Urusi kwa 100%. NATO inaogopa kuunganisha Ukraine kwenye mfumo wake wa ulinzi na pia ule wa kiserikali (zikiwemo Ikulu za NATO) kwa kuhofia Urusi kudukua. Hivyo Urusi inadhibiti mfumo wa mawasiliano yanayoingia na kutoka Ukraine na kufanya NATO kukata mawasiliano na Ukraine. Vita ni mawasiliano kwa sababu ndiko amri za kivita zinakopatikana.
Mrusi huyo ndani ya Tanzania..😂
 
Tuondolee mahaba na hisia zako, Leta chanzo cha habari tujisomee
 
Tayari Urusi inadukua mawasiliano ya Ikulu na Idara zote za Ulinzi na Usalama za Ukraine. Ukraine sasa iko mikononi mwa Urusi kwa 100%. NATO inaogopa kuunganisha Ukraine kwenye mfumo wake wa ulinzi na pia ule wa kiserikali (zikiwemo Ikulu za NATO) kwa kuhofia Urusi kudukua. Hivyo Urusi inadhibiti mfumo wa mawasiliano yanayoingia na kutoka Ukraine na kufanya NATO kukata mawasiliano na Ukraine. Vita ni mawasiliano kwa sababu ndiko amri za kivita zinakopatikana.
Yes is clear and logical, why NATO not picking any call from Ukraine .
 
Mbona unakomaa tuu bila hata kaushahidi ka website au screen shot?
 
Yes is clear and logical, why NATO not picking any call from Ukraine .
Baada ya Ukraine kukosa mawasiliano toka US na NATO kuanzia usiku wa jana (kwa saa za EA), rais mpweke wa Ukraine amelihutubia taifa lake kuiambia Moscow kuwa Ukraine haitapigana vita hivyo anaitaka Moscow kuondoa vikosi vyake toka ardhi ya Ukraine.
 
Mbona unakomaa tuu bila hata kaushahidi ka website au screen shot?
Uchambuzi siyo lazima kila kitu copy paste, baadhi unatumia pursuits zako kupata logic na sense bila kuathiri maana. Kwenye Journalism inaitwa Critical Thinking.

Sources:-
RT
ALJAZEERA
BBC
CNN
DW
REUTERS
AFP
XINHUA

Kwanini vyanzo hivyo vyote na siyo kimoja? Kwenye Journalism kuna kitu kinaitwa balance of story/report. Unasikiliza/unasoma kote alafu unatafuta right balance.
 
Umechambua vizuri lakini hapo uliposema eti Urusi ina Siraha za Kibiolojia ambazo USA na NATO hawana hapo ndipo nikasituka nikajua huyu ni Team Putin kwahiyo hakuna uchambuzi wowote ule zaidi ya mahaba.

Yaani unaizungumzia Hii hii USA ambayo ilitengeneza Magonjwa yafuatayo ambayo mpaka Sasa yanaitesa Dunia na hakuna taifa lenye Tiba mahususi zaidi ya USA yenyewe?

Anthrax, Polio,Small Pox,HIV Mansoil,TB, Rift Valley Flue.

Wewe jamaa Nenda kasome tena. Yaani hata wewe umejisitukia kabisa eti (ni Siri kubwa) harafu wewe wa kwa Mtongole unaijua.
 
Ukraine bye bye... Tuliwaambia lakini.

Hitler mwenyewe alikuwa amekaribia kuiteka dunia yote ila alipoambiwa wanajeshi wa Urusi wapo hapa Ujerumani ikambidi adumbukie kwenye pipa la asidi 😬😬
NATO inaogopa vita na Mrusi kipindi hiki cha msimu wa baridi kali na virusi vya Corona vinavyoshamiri kwenye ubaridi.

In Northern and central parts of Russia winter starts in early November and stretches all the way to the end of April.

Urusi ni mjuvi pekee duniani mwenye uwezo wa kipekee wa kupigana kwenye ubaridi mkali.

Enzi ya vita kuu ya dunia, Warusi hawakuishi kwenye eneo waliloko leo, waliishi maeneo ya Yugoslavia, baada ya Hitler kuwaua kwa uwingi waliamua kukimbilia juu zaidi karibu na Northern Pole ya dunia kwenye ubaridi mkali ambapo vikosi vya Ujerumani vilikufa kwa baridi kali tu hata bila silaha na ndipo Mrusi akaanza kustawi kwenye eneo hilo na kubuni vileo vikali vinavyohimili ubaridi na hivyo kujijenga kimedani dhidi ya Ujerumani na kuwashinda vita.
 
Umechambua vizuri lakini hapo uliposema eti Urusi ina Siraha za Kibiolojia ambazo USA na NATO hawana hapo ndipo nikasituka nikajua huyu ni Team Putin kwahiyo hakuna uchambuzi wowote ule zaidi ya mahaba.

Yaani unaizungumzia Hii hii USA ambayo ilitengeneza Magonjwa yafuatayo ambayo mpaka Sasa yanaitesa Dunia na hakuna taifa lenye Tiba mahususi zaidi ya USA yenyewe?

Anthrax, Polio,Small Pox,HIV Mansoil,TB, Rift Valley Flue.

Wewe jamaa Nenda kasome tena. Yaani hata wewe umejisitukia kabisa eti (ni Siri kubwa) harafu wewe wa kwa Mtongole unaijua.
The Russian Federation is known to have possessed three types of weapons of mass destruction: nuclear weapons, biological weapons, and chemical weapons. It is one of the five nuclear-weapon states recognized under the Treaty on the Non-Proliferation of Nuclear Weapons. The nation possesses approximately 6,400 nuclear warheads—the largest stockpile of nuclear weapons in the world.[4] More than half of the world's 14,000 nuclear weapons are owned by Russia.[5] Russia's predecessor state, the Soviet Union, reached a peak stockpile of about 45,000 nuclear warheads in 1986.[6]

The Soviet Union ratified the Geneva Protocol—prohibiting the use of biological and chemical weapons—on April 5, 1928 with reservations that were later dropped on January 18, 2001.[7] Russia is also party to the 1972 Biological Weapons Convention and the 1993 Chemical Weapons Convention.[8][9] The Soviet biological weapons program violated the Biological Weapons Convention and was the world's largest, longest, and most sophisticated program of its kind.[10] At its peak, the program employed up to 65,000 people.[10] In 1997, Russia declared an arsenal of 39,967 tons of chemical weapons.[11][12]

Source: Wikipedia.

The United States biological weapons program began in 1943 and was discontinued in 1969.

The program officially began in spring 1943 on orders from U.S. President Franklin Roosevelt. Research continued following World War II as the U.S. built up a large stockpile of biological agents and weapons. Over the course of its 27-year history, the program weaponized and stockpiled the following seven bio-agents (and pursued basic research on many more):

Source: Wkipedia

Sasa angalia haya:
Urusi (Soviet Union) ilisaini Itifaki ya kuachana na silaha za kibailojia April 5, 1928. Ina maana iliishakuwa nazo kabla ya mwaka 1928 (kabla ya hata vita ya pili ya dunia)

US ilianza kujenga silaha za kibailojia kwa mara ya kwanza mwaka 1943 (baada ya Soviet Union kusaini Itifaki ya Geneva) na kuachana na matumizi yake mwaka 1969. Inaaminika US ilishindwa kuzidhibiti kiteknolojia na kibajeti jambo ambalo lilifanya PENTAGON kusitisha uzalishaji, matumizi na kuziharibu zenyewe ili kukwepa isije kujipatia madhara yenyewe. Ukimwi et al vilishinda US na zikachomoka na kusambaa duniani.

Urusi ndiyo nchi pekee duniani iliyowahi kuwa na mzigo mkubwa wa silaha za kibaiolojia (zaidi ya nusu ya silaha za dunia ilikuwa nazo Urusi pekee)

Katika vita za Iraq na US miaka ya 1989 na ile ya 2003 - 2011, inaaminika Iraq ilitishia kutumia silaha za kibaiolojia ilizopata toka Urusi, ina maana Urusi bado kumbe inazo kwa siri hata baada ya kusaini Itifaki ya Geneva ya mwaka 1928, na ndiyo maana kwenye vita hizo US ililalamika Urusi kuvunja Itifaki hiyo, kama US ilikuwa nazo basi isingelalamika maana nayo ingezitumia za kwake pia dhidi ya Saddam Hussein.

Always research before you go public.
 
Tayari dunia imegawanyika ambapo NATO chini ya US ina ushirika mkubwa dhidi ya Urusi ambayo hadi sasa inaonekana kuwa peke yake

Nimeishia kusoma hapo tu.

Hivi unafatilia mambo kweli maana inaoneakana kama yote uliyoandika humo umesimuliwa.
 
Back
Top Bottom