Mbona nimesikia majini hawazeeki wanabadilisha upepo tu?MAJINI WANAKUFA?
Allaah Anasema:
"Kila kilichopo juu yake (ardhi na mbingu) kitatoweka (kitaondoka)."
Ar-Rahmaan - 26
Na Akasema:
"Hakuna aabudiwaye kwa haki ila Yeye; kila kitu kitakufa isipokuwa Yeye (Allaah basi)."
Al-Qaswas - 88
Inavyojulikana ni kwamba Iblisi yuhai mpaka siku ya Qiyaamah.
Allaah Amesema:
"Akasema (Iblisi); “Mola wangu! basi nipe nafasi (nisife) mpaka siku watakayofufuliwa (viumbe) vyote.”
Akasema (Allaah); “Hakika wewe (nimekwisha kukufanya) katika wale waliopewa nafasi.
Mpaka siku ya wakati uliowekwa (ukifika wakati huo utakufa).”
Al-Hjr - 36 -37-38
Kwa hivyo Ibilisi ataishi mpaka siku maalum anayoijua Allaah peke yake kisha atakufa, na majini nao pia wanazaliana na wanakufa kama sisi.
....apa umeacha mtyu! "malaika hawaasi" na ibilisi walikuwa waasi kabla ya kukataa kushujudu??...awali maisha yao yalikuwa adje.... EndeleaaIBILISI NI KATIKA MALAIKA?
Iblisi si katika Malaika, bali ni miongoni mwa Majinni kutokana na dalili zifuatazo:
Allaah Anasema:
"Basi wakamsujudia isipokuwa Iblisi; yeye alikuwa miongoni mwa majini."
Al Kahf -50
Na Akasema:
"Hawamuasi Allaah kwa amri zake; na wanatenda wanavyoamrishwa (yote)."
AtTahrym - 6
Kutokana na aya hii, tunapata ushahidi mwingine kuwa; Malaika hawamuasi Allaah. Kwa hivyo Ibilisi angelikuwa Malaika, asingemuasi Mola wake bali angetenda kama alivyoamrishwa. Lakini yeye alitenda kinyume na hivo. Alimuasi Allaah pale alipokataa kumsujudia baba yetu Aadam ('Alayhis Salaam), akasema:
"Akasema (Ibilisi)‘; 'Mimi ni bora kuliko yeye (Mimi) umeniumba kwa moto naye umemuumba kwa udongo."
Al Aaraf - 12
Na hapa pia tunapata ushahidi mwingi pia kuwa Iblisi si miongoni mwa Malaika, kwani Malaika wameumbwa kwa Nuru na Mashaytwaan wameumbwa kwa moto.
Katika aya iliyotangulia Iblisi alisema:
'Mimi ni bora kuliko yeye (Mimi) umeniumba kwa moto."
Angelikuwa yeye ni miongoni mwa Malaika angelisema;
“Mimi ni bora kuliko yeye umeniumba kwa Nuru".
Kwa sababu Malaika wameumbwa kwa Nuru kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) katika hadithi iliyotangulia:
"Malaika wameumbwa kwa nuru na Majini kwa ndimi za moto na Adam (ameumbwa) kwa mliyokwisha elezewa (Udongo)."
Muslim na Ahmad bin Hanbal
AINA ZA MAJINI
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
"Majini (wako) namna tatu, namna moja wana mabawa wanaruka na namna (nyengine) majoka na n’ge na namna nyengine hawaishi mahala pamoja na hupenda kuhama."
Atw-Twabaraaniy na Al-Haakim na Al-Bayhaqiy na imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy
MAHALI WANAPOISHI
Majini wanaishi katika majangwa na katika sehemu za kutupa taka, kwa sababu wao wanakula mabaki ya vyakula vya binadamu.
Zimepokelewa hadithi nyingi pia kwa njia ya Ibni 'Abbaas na Ibni Masaood (Radhiya Allaahu ‘anhum) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alikuwa akienda jangwani na kuwasemesha Majinni na kuwalingania katika dini ya Kiislamu na kuwataka wamuabudu Allaah mmoja wa kweli.
Majinni wanapenda pia kuishi vyooni, na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ametufundisha dua ya kusoma kabla ya mtu kuigia chooni, akasema:
Mmoja wenu anapoingia chooni basi aseme;
"Allaahumma inniy audhu bika minal khubuthi wal khabaaith."
Na maana yake;
“Allaah najikinga kwako kutokana na majini wanaume na majini wanawake.”
Al-Bukhaariy na Muslim.
Majini pia wanaishi katika Mashimo:
Kutoka kwa Qataadah kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
"Mmoja wenu asikojowe ndani ya shimo."
Na alipoiulizwa kuna ubaya gani mtu kukojoa ndani ya shimo akasema:
"Inasemekana kuwa Majinni wanapenda kuishi humo."
VIPI UTAWEZA KUMJUA MCHAWI
Zifuatazo ni dalili zitazokuwezesha kutofautisha baina ya mganga na mchawi. Utakapoona mojawapo ya dalili zufuatazo utambuwe kuwa huyo ni mchawi bila shaka yeyote na wala si shekhe au mganga:-
Mchawi huuliza jina la mgonjwa na jina la mama yake
Huchukua baadhi ya vitu vya mgonjwa kama vile nguo za nje au za ndani au kitambaa cha kufutia jasho n.k.
Hutaka mnyama mwenye sifa maalum au rangi maalum ili achinjwe na hapigiwi BismiLLaahi anapochinjwa
Huandika hirizi
Husema maneno yasiyojulikana
Humtaka mgonjwa aepukane na watu muda maalum na akae katika chumba kisichofikiwa na juwa
Mara nyengine humtaka mgonjwa asiguse maji muda wa siku arubaini hivi (anasema Shaykh Wahiyd Abdulsalaam Bali kwamba akikutaka ufanye hivyo ujue kwamba Jinni anayemtumikia )
Humpa mgonjwa vitu ili avifukie ardhini
Humpa mgonjwa karatasi aziunguze kisha ajifukize na moshi wake
Mara nyengine humwambia mgonjwa jina lake na mji anaoishi
Huandika maneno katika karatasi na kumwambia mgonjwa azichemshe na kunywa maji yake
UKIONA DALILI HIZI KWA MGANGA UMJUE HAPOHAPO KUWA NI MCHAWI NA UEPUKANE NAYE
Anasema Shaykh Wahiyd Abdulasalaam Bali:
"Ukiutizama uso wa mchawi utakiona kiza cha kufru kilivyotanda katika uso huo mfano wa mawingu meusi.”
Anaendelea kusema Shaykh huyo:
“Kwa wale wanaowajua wachawi, wanawaona siku zote wakiwa katika dhiki, shida, matatizo katika siha zao, matatizo na wake zao au watoto wao na siku zote hawana raha wala utulivu.”
Allaah Anasema:
"Na hakika kulikuwa na wanaume miongoni mwa wanaadamu wakijikinga kwa wanaume miongoni mwa majini kwa hivyo wakawazidishia taklifu (taabu)."
Al-Jinn - 6
Na Anasema:
"Na atakayejiepusha na mawaidha yangu basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki."
Twaahaa 124
unaweza tu imagine how jinn look like, only Allah knows jinsi wanavyoonekanaSwali, majini hatuyaoni kwa kuwa hayana mwili au yana mwili ili miili yao haionekani, je iwapo wana miili,miili hiyo ni ya namna gani