Jini, Shetani na wachawi

Jini, Shetani na wachawi

MAJINI WANAWAOGOPA WANADAMU
Ameeleze Ibn Abi Al Dunya kwamba Mujahid amesema:

‘Usiku mmoja nilikuwa nikiswali akanitokea mfano wa mtoto mdogo mbele yangu nikamshika kwa nguvu zangu zote akainuka na kuuruka ukuta hata nilisikia kishindo cha kuanguka kwake.’ Akaendela kusema: ‘Wao (majini) wanakuogopeni kama nyinyi mnavyowaogopa."

Imepokelewa kutoka kwa Mujahid kuwa alisema:

‘Shaytwaan anakuogopeni kuliko nyinyi mnavyomuogopa akikukaribia usimregezee akakupanda, bali shindana naye na hatimae ataondoka."
 
KUWEZA KWA MAJINI KUSIKIA HABARI ZA MBINGUNI
Imepokelewa kutoka kwa Ibni 'Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba alisema:

‘Amenihadithia mmoja katika maSwahaba wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kuwa, usiku mmoja walipokuwa wamekaa pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) nyota moja ikaanguka na kun’gara. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akawauliza:

"Mlikuwa mkisemaje wakati wa ujahilia (kabla ya kuja Uislamu?"

Wakajibu:

"Tulikuwa tukisema; Usiku wa leo amezaliwa mtu mtukufu na amekufa mtu mtukufu."

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akawaambia:

"Bali haiangushwi nyota kwa ajili ya kifo cha mtu wala kwa kuzaliwa kwa mtu, lakini Mola wetu Aliyetukuka anapotoa amri, Malaika wabebao Arshi husabbih (husema Subhana Allaah), na viumbe vya mbinguni vyote humsabihi Allaah pia, kisha husabihi viumbe wa mbingu za chini mpaka habari inapofika katika mbingu ya dunia, majini huzipata habari hizo na huwatupia mabwana zao nazo ni habari za kweli, lakini wao huongeza habari za uongo juu yake.”

Kutokana na Bibi 'Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha), amesema:

"Niliuliza:

"Ewe Mtume wa Allaah, makuhani walikuwa wakituelezea baadhi ya mambo na yalikuwa ni ya kweli."

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akasema:

"Hiyo ni habari ya kweli ameipokea jini akamtupia bwana wake na kuongezea uongo mara Mia."

Imetolewa na Maimaam Al-Bukhaariy na Muslim na Ahmad na AlBayhaqiy

 
UCHAWI

NINI MAANA YA UCHAWI?
Al Azhari ambaye ni mtungaji wa kamusi maarafu ya kiarabu iitwayo “LisanulArab”amesema:

“Neno “Uchawi”, kwa kiarabu “As Sihr”, maana yake ni kitendo cha kujikurubisha na Shaytwaan na kwa msaada wake (Shaytwaan)”, na akasema pia kuwa; “Uchawi ni kulibadilisha jambo mbali na uhakika wake, nako ni kuwadhihirishia watu jambo lisilo la kweli wakaliona kuwa ni la kweli.”

Ama Swahaba Ibni 'Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema:

"Uchawi ni kuidhirisha batili katika sura ya haki."

Hayo ni katika kamusi za lugha.


Amma katika kamusi ya dini, maana ya neno Uchawi (As Sihr), kama alivyofasiri Mwanachuoni mkubwa Fakhruddin Al Razi kuwa;

"Ni kila jambo lililofichika sababu zake, linalotokeza kwa sababu zisizo za kawaida na ndani yake mna hadaa (khidaa)."

Amma Shaykh Wahiyd Abdulsalaam Bali, mwandishi wa kitabu maarufu kiitwacho 'Al Saarim Al Batar fiy muhaarabat Al Saharatul ashraar', na kitabu kiitwacho "Al wiqaya mina l jinni wa shaytan", ambaye pia ni mtaalamu maarufu katika elimu ya majini na Mashaytwaan na uchawi na ambaye pia ni katika maulamaa maarufu wanaotoa majini kwa njia ya kusoma Qur-aan, yeye anasema:

"Uchawi ni makubaliano baina ya mchawi na Jinni akishurutishwa mchawi kufanya mambo ya haramu au ya shirki, na baada ya kufanya hayo, Jinni anashurutishwa kumsaidia na kumtii mchawi huyo kwa kila anachotaka."
 
Baadhi ya yale ambayo mchawi anatakiwa na Shaytwaan ayatende ili ajikurubishe naye ni:



 Mchawi anatakiwa auvae msahafu miguuni na aingie nao chooni

 Aandike baadhi ya aya za Qur-aan kwa damu ya hedhi.

 Miongoni mwao wanashurutishwa kuandika aya za Qur-aan penye nyayo za miguu.

 Au aiandike suratulFatiha kinyume nyume.

 Asali bila ya Udhuu.

 Wengine hutakiwa kuchinja mnyama bila ya kulitaja jina la Allaah kisha amtupe mnyama huyo mahali maalum anapoamrishwa na Shaytwaan.

 Wamo miongoni mwao wanaozungumza na nyota au kuzisujudia.

 Au hutakiwa kuandika herizi kwa maneno yenye kufru ndani yake
 
MAJINI WANAKUFA?
Allaah Anasema:

"Kila kilichopo juu yake (ardhi na mbingu) kitatoweka (kitaondoka)."

Ar-Rahmaan - 26



Na Akasema:

"Hakuna aabudiwaye kwa haki ila Yeye; kila kitu kitakufa isipokuwa Yeye (Allaah basi)."

Al-Qaswas - 88


Inavyojulikana ni kwamba Iblisi yuhai mpaka siku ya Qiyaamah.

Allaah Amesema:

"Akasema (Iblisi); “Mola wangu! basi nipe nafasi (nisife) mpaka siku watakayofufuliwa (viumbe) vyote.”

Akasema (Allaah); “Hakika wewe (nimekwisha kukufanya) katika wale waliopewa nafasi.

Mpaka siku ya wakati uliowekwa (ukifika wakati huo utakufa).”

Al-Hjr - 36 -37-38


Kwa hivyo Ibilisi ataishi mpaka siku maalum anayoijua Allaah peke yake kisha atakufa, na majini nao pia wanazaliana na wanakufa kama sisi.
Mbona nimesikia majini hawazeeki wanabadilisha upepo tu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
IBILISI NI KATIKA MALAIKA?
Iblisi si katika Malaika, bali ni miongoni mwa Majinni kutokana na dalili zifuatazo:

Allaah Anasema:

"Basi wakamsujudia isipokuwa Iblisi; yeye alikuwa miongoni mwa majini."

Al Kahf -50


Na Akasema:

"Hawamuasi Allaah kwa amri zake; na wanatenda wanavyoamrishwa (yote)."

AtTahrym - 6


Kutokana na aya hii, tunapata ushahidi mwingine kuwa; Malaika hawamuasi Allaah. Kwa hivyo Ibilisi angelikuwa Malaika, asingemuasi Mola wake bali angetenda kama alivyoamrishwa. Lakini yeye alitenda kinyume na hivo. Alimuasi Allaah pale alipokataa kumsujudia baba yetu Aadam ('Alayhis Salaam), akasema:

"Akasema (Ibilisi)‘; 'Mimi ni bora kuliko yeye (Mimi) umeniumba kwa moto naye umemuumba kwa udongo."

Al Aaraf - 12


Na hapa pia tunapata ushahidi mwingi pia kuwa Iblisi si miongoni mwa Malaika, kwani Malaika wameumbwa kwa Nuru na Mashaytwaan wameumbwa kwa moto.

Katika aya iliyotangulia Iblisi alisema:

'Mimi ni bora kuliko yeye (Mimi) umeniumba kwa moto."

Angelikuwa yeye ni miongoni mwa Malaika angelisema;

“Mimi ni bora kuliko yeye umeniumba kwa Nuru".


Kwa sababu Malaika wameumbwa kwa Nuru kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) katika hadithi iliyotangulia:

"Malaika wameumbwa kwa nuru na Majini kwa ndimi za moto na Adam (ameumbwa) kwa mliyokwisha elezewa (Udongo)."

Muslim na Ahmad bin Hanbal
....apa umeacha mtyu! "malaika hawaasi" na ibilisi walikuwa waasi kabla ya kukataa kushujudu??...awali maisha yao yalikuwa adje.... Endeleaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Imeelezwa kwamba katika nchi ya Sham kulikuwa na mtu ambaye watu walikuwa wakimpenda na kumheshimu sana wakimdhania kuwa ni mtu mwenye makarama.

Mtu huyu alikuwa kila mwaka katika msimu wa Hajji akiwatumikia watu wa mji wake kwa kuchukua barua zao na vitu vyao na kuwapelekea watu wao waliokwenda Saudia kuhijji.

Alikuwa akipeleka na kurudi kwa muda wa siku moja au mbili tu, na watu walimpenda sana na kuamini kwamba alikuwa ni Waliy.



Siku moja mtu huyo aliumwa sana, akamuita mwanawe na kumwambia kuwa kama atakufa, basi ende mahali fulani wakati wa usiku na atamkuta ngamia wa aina fulani na ampande na kufuata amri zote atakazopewa na ngamia huyo.

Alipofariki dunia, mwanawe alifanya kama alivyoambiwa na baba yake, akaondoka peke yake wakati wa usiku na kuelekea jangwani kule alikoambiwa na baba yake kuwa atamkuta ngamia. Akamkuta ngamia kama alivyoambiwa, akampanda na alipokuwa akenda, ngamia akaanza kusema na kumtaka kijana yule ashuke na amsujudie.

Yule kijana alishtuka sana kusikia ngamia akisema na pia akashangazwa na amri zake, akamwambia:

"Vipi nikusujudie, kweni wewe ni nani?"

"Ikiwa unataka nifuate amri zako kama nilivyokuwa kwa baba yako, na nikupeleke popote utakapo duniani, basi unisujudie kama alivyokuwa akinisujudia baba yako."

Yule kijana akajibu:

"Mimi ninamsujudia Allaah peke yake, amma wewe la, siwezi kukusujudia."

Ngamia akamrusha kijana yule kutoka juu ya mgongo wake na kumwangusha chini, na kijana yule akatoka mbio mpaka nyumbani kwa mama yake na kumuelezea yote aliyoyaona na kwamba baba yake alikuwa akimsujudia Jinni ndiyo maana alikuwa na uwezo wa kusafiri kila anapotaka kwenda kwa kupaishwa na jini yule.


Kwa haya inatubainikia kuwa Jinni hamsaidii wala hamhudumii mchawi wala mtu yeyote isipokuwa naye kwa mkabala wake atumikiwe kwa kutendewa matendo ya kufru, na maulamaa wanasema:

"Kila mchawi anapokufuru zaidi, basi Shaytwaan humtumikia kwa nguvu zaidi, na mchawi akitaka apate huduma ya hali ya juu kabisa kutoka kwa masultani wa majini au kwa kiarabu wanaitwa "Maradatul Jinni", basi inambidi afanye kufuru kubwa zaidi, na kwa ajili hiyo, mchawi anapotaka nguvu juu ya wenzake inamlazimikia akufuru zaidi."

Kutokana na haya tunafahamu kwamba mchawi na Shaytwaan ni marafiki na washirika katika kumuasi Allaah.



Allaah Anasema:

"Na (wakumbushe) siku atakapowakusanya wote (akawaambia): "Enyi makundi ya majini! Hakika nyinyi mmechukua wafuasi wengi katika wanaadamu". Na marafiki wao katika wanaadamu (watagombania) waseme: "Mola wetu! Tulinufaishana sisi na wao na tumefikia muda wetu uliotuwekea". Basi (Allaah) atasema; "Moto ndio makazi yenu, mtakaa humo milele", ila apende Allaah (kuwarehemu), hakika Mola wako ndiye Mwenye hikima (na) ndiye ajuaye.”

Al-An'aam - 128
 
VIPI UTAWEZA KUMJUA MCHAWI
Zifuatazo ni dalili zitazokuwezesha kutofautisha baina ya mganga na mchawi. Utakapoona mojawapo ya dalili zufuatazo utambuwe kuwa huyo ni mchawi bila shaka yeyote na wala si shekhe au mganga:-



 Mchawi huuliza jina la mgonjwa na jina la mama yake

 Huchukua baadhi ya vitu vya mgonjwa kama vile nguo za nje au za ndani au kitambaa cha kufutia jasho n.k.

 Hutaka mnyama mwenye sifa maalum au rangi maalum ili achinjwe na hapigiwi BismiLLaahi anapochinjwa

 Huandika hirizi

 Husema maneno yasiyojulikana

 Humtaka mgonjwa aepukane na watu muda maalum na akae katika chumba kisichofikiwa na juwa

 Mara nyengine humtaka mgonjwa asiguse maji muda wa siku arubaini hivi (anasema Shaykh Wahiyd Abdulsalaam Bali kwamba akikutaka ufanye hivyo ujue kwamba Jinni anayemtumikia )

 Humpa mgonjwa vitu ili avifukie ardhini

 Humpa mgonjwa karatasi aziunguze kisha ajifukize na moshi wake

 Mara nyengine humwambia mgonjwa jina lake na mji anaoishi

 Huandika maneno katika karatasi na kumwambia mgonjwa azichemshe na kunywa maji yake

UKIONA DALILI HIZI KWA MGANGA UMJUE HAPOHAPO KUWA NI MCHAWI NA UEPUKANE NAYE


Anasema Shaykh Wahiyd Abdulasalaam Bali:

"Ukiutizama uso wa mchawi utakiona kiza cha kufru kilivyotanda katika uso huo mfano wa mawingu meusi.”



Anaendelea kusema Shaykh huyo:

“Kwa wale wanaowajua wachawi, wanawaona siku zote wakiwa katika dhiki, shida, matatizo katika siha zao, matatizo na wake zao au watoto wao na siku zote hawana raha wala utulivu.”

Allaah Anasema:

"Na hakika kulikuwa na wanaume miongoni mwa wanaadamu wakijikinga kwa wanaume miongoni mwa majini kwa hivyo wakawazidishia taklifu (taabu)."

Al-Jinn - 6

Na Anasema:

"Na atakayejiepusha na mawaidha yangu basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki."

Twaahaa 124
 
AINA ZA MAJINI
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

"Majini (wako) namna tatu, namna moja wana mabawa wanaruka na namna (nyengine) majoka na n’ge na namna nyengine hawaishi mahala pamoja na hupenda kuhama."

Atw-Twabaraaniy na Al-Haakim na Al-Bayhaqiy na imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy


MAHALI WANAPOISHI
Majini wanaishi katika majangwa na katika sehemu za kutupa taka, kwa sababu wao wanakula mabaki ya vyakula vya binadamu.

Zimepokelewa hadithi nyingi pia kwa njia ya Ibni 'Abbaas na Ibni Masaood (Radhiya Allaahu ‘anhum) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alikuwa akienda jangwani na kuwasemesha Majinni na kuwalingania katika dini ya Kiislamu na kuwataka wamuabudu Allaah mmoja wa kweli.

Majinni wanapenda pia kuishi vyooni, na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ametufundisha dua ya kusoma kabla ya mtu kuigia chooni, akasema:

Mmoja wenu anapoingia chooni basi aseme;

"Allaahumma inniy audhu bika minal khubuthi wal khabaaith."

Na maana yake;

“Allaah najikinga kwako kutokana na majini wanaume na majini wanawake.”

Al-Bukhaariy na Muslim.


Majini pia wanaishi katika Mashimo:

Kutoka kwa Qataadah kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

"Mmoja wenu asikojowe ndani ya shimo."

Na alipoiulizwa kuna ubaya gani mtu kukojoa ndani ya shimo akasema:

"Inasemekana kuwa Majinni wanapenda kuishi humo."

Swali, majini hatuyaoni kwa kuwa hayana mwili au yana mwili ili miili yao haionekani, je iwapo wana miili,miili hiyo ni ya namna gani
 
VIPI UTAWEZA KUMJUA MCHAWI
Zifuatazo ni dalili zitazokuwezesha kutofautisha baina ya mganga na mchawi. Utakapoona mojawapo ya dalili zufuatazo utambuwe kuwa huyo ni mchawi bila shaka yeyote na wala si shekhe au mganga:-



 Mchawi huuliza jina la mgonjwa na jina la mama yake

 Huchukua baadhi ya vitu vya mgonjwa kama vile nguo za nje au za ndani au kitambaa cha kufutia jasho n.k.

 Hutaka mnyama mwenye sifa maalum au rangi maalum ili achinjwe na hapigiwi BismiLLaahi anapochinjwa

 Huandika hirizi

 Husema maneno yasiyojulikana

 Humtaka mgonjwa aepukane na watu muda maalum na akae katika chumba kisichofikiwa na juwa

 Mara nyengine humtaka mgonjwa asiguse maji muda wa siku arubaini hivi (anasema Shaykh Wahiyd Abdulsalaam Bali kwamba akikutaka ufanye hivyo ujue kwamba Jinni anayemtumikia )

 Humpa mgonjwa vitu ili avifukie ardhini

 Humpa mgonjwa karatasi aziunguze kisha ajifukize na moshi wake

 Mara nyengine humwambia mgonjwa jina lake na mji anaoishi

 Huandika maneno katika karatasi na kumwambia mgonjwa azichemshe na kunywa maji yake

UKIONA DALILI HIZI KWA MGANGA UMJUE HAPOHAPO KUWA NI MCHAWI NA UEPUKANE NAYE


Anasema Shaykh Wahiyd Abdulasalaam Bali:

"Ukiutizama uso wa mchawi utakiona kiza cha kufru kilivyotanda katika uso huo mfano wa mawingu meusi.”



Anaendelea kusema Shaykh huyo:

“Kwa wale wanaowajua wachawi, wanawaona siku zote wakiwa katika dhiki, shida, matatizo katika siha zao, matatizo na wake zao au watoto wao na siku zote hawana raha wala utulivu.”

Allaah Anasema:

"Na hakika kulikuwa na wanaume miongoni mwa wanaadamu wakijikinga kwa wanaume miongoni mwa majini kwa hivyo wakawazidishia taklifu (taabu)."

Al-Jinn - 6

Na Anasema:

"Na atakayejiepusha na mawaidha yangu basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki."

Twaahaa 124

Hicho kiza cha kufru ni kitu gani kwa hiyo kila mtu akikiona kiza cha kufru kwenye uso wa mtu basi ajue huyo mtu ni mchawi ?Naona hapa ujasaidia lolote kuhusu kumtambua mchawi
 
DALILI KUWA UCHAWI UPO, KUTOKA KATIKA QUR-AAN NA KATIKA SUNNAH (MAFUNDISHO YA MTUME (SWALLA ALLAAHU ‘ALAYHI WA SALLAM)
Katika Surat Yunus aya ya 77 Allaah Anasema:

"Akasema Musa:"Mnasema (hivi) juu ya haki ilipokujieni, (kuwa) Huu ni uchawi? (Mbona umefaulu basi) Na wachawi hawafaulu."


Hii ni dalili kwamba uchawi upo na Allaah anatufundisha katika aya hii kwamba uchawi haufaulu.

Na katika suratul Falaq Akasema:

"Na (najikinga na) shari ya wale wanaopuliza mafundoni."


Katika kuifasiri aya hii, mmoja katika maulamaa wakubwa wa tafsiri ya Qur-aan Imam Al Qurtuby amesema:

"Maana ya neno "Naffaathaat", ni wachawi wanapopuliza katika nyuzi huku wakizipiga fundo.”

Na Ibni Kathiyr katika tafsiri yake akinukuu kutoka kwa Ikrimah na Mujahid na Al Hassan Al Basry (Radhiya Allaahu ‘anhum) amesema:

"Hawa wanaopuliza mafundoni ni wachawi, na Allaah anatuamrisha tujiepushe na shari zao.”


Amma hadithi za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) zinazotufahamisha kwamba uchawi upo na kwamba uchawi ni katika madhambi makubwa sana, ni hizi zifuatazo:

Kutoka kwa Abi Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

"Jieupusheni na (mambo) saba Yaangamizayo.'

Wakasema:

'Ni yepi hayo ewe Mjumbe wa Allaah?"

Akasema:

"Kumshirikisha Allaah, Uchawi, kuiuwa nafsi iliyoharimishwa na Allaah ila kwa haki yake, kula riba, kula mali ya yatima, kurudi nyuma (kukimbia) katika vita vya Jihadi (huku ukiwaacha wenzio wanapigana), na kuwasingizia uwongo wanawake wema wasio na makosa."

Al-Bukhaariy na Muslim


Ndugu yangu Muislamu, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) aliposema kuwa mambo hayo 'Yanayomuangamiza', maana yake ni kuwa yanamuangamiza mtu katika moto wa Jahannam.

Ukirudia kuisoma tena hadithi hiyo utaona kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ameutanguliza uchawi kabla ya dhambi ya kuuwa, ingawaje kuuwa ni dhambi kubwa sana, na Allaah Anasema katika Suratu Nnisaa aya ya 93:

"Atakayemuuwa Muislamu kusudi, basi jaza yake ni Jahannam atakuwa humo milele na Allaah Ataghadhibika naye na Atamlaani na amemtayarishia adhabu kubwa."


Juu ya ukubwa wa dhambi hiyo ya kuuwa, lakini Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu alayhi wa sallam) ameipa uzito zaidi dhambi ya Uchawi kwa kuiweka nafasi ya pili baada ya Shirki na kabla ya dhambi ya kuuwa.

 
SOMA BAHATI YAKO (NYOTA YAKO) LUCKY STARS
Katika hadithi ifuatayo iliyosimuliwa na Abu Dawood na Ibni Majah hadithi ambayo Shaykh Al-Albaaniy ameitaja kuwa ni "hadithi njema", na hadithi hii pia ni dalili kwamba elimu ya kutabiri kwa nyota ambayo huandikwa katika magazeti na watu hupenda kusoma kwa kutaka kujua bahati zao, kitendo hiki ni haramu na yeyote atakayesoma nyota yake, basi swala zake hazikubaliwi kwa muda wa siku arobaini, hii ikiwa anasoma na huku haziamini, amma akisoma na huku anaziamini, basi anaingia katika hukumu ya aliyemuendea mtabiri na kumuuliza jambo, na anakuwa amekwisha kufuru yote aliyoteremshiwa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam).

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

"Atakayejifunza sehemu ya elimu ya nyota (utabiri) amejifunza sehemu ya uchawi, akiongeza atakachoongeza (katika uchawi au nyota)."


Na hii ni kwa sababu wanaosoma elimu ya nyota (utabiri) wanaamini kwamba katika nyota wanaishi majini ambao ni masultani na wakuu, na wanaitakidi kuwa mambo yetu yote husababishwa na harakati za nyota hizo kila zinapotaharaki kutoka mahali kuelekea pengine. Kwa ajili hiyo wao huzingoja nyota hizo masaa mengi ya usiku ili wapate kuandika talasimu zao, na huku ni sawa na kuziabudu nyota hizo.

(Pana tofauti baina ya elimu ya anga za juu (Astronomy) ambayo haina ubaya wowote ndani yake, na elimu ya nyota (Astrology) - utabiri - ambayo ni haramu).

Ushahidi Mwengine unapatikana katika hadithi iliyosimuliwa na Umran bin Hussain (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliyesema kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

“Hayuko pamoja nasi mwenye kuamini juu ya nukhsi (waarabu walikuwa wanapotaka kusafiri humrusha ndege na akielekea upande wa kulia basi husafiri, amma akielekea upande wa kushoto huamini ni ukorofi na kuivunja safari yake), na pia hayuko pamoja nasi mwenye kupiga ramli au mwenye kupigiwa, na atakayemuendea mtabiri na akamsadiki asemayo basi kesha kufuru yale aliyoteremshiwa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)."

Al-Bazaar.


Katika hadithi hizi Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) anatukataza tusiwaendee wachawi wala watabiri wa aina yoyote ile kwa kuwauliza juu ya jambo lolote lile, hata kama atajibadilisha na kujiita AlHajj Fulani au Shaykh Fulani au Maalim Fulani au Mganga Fulani na hii ni kutokana na kufru zao wanazozifanya kwa kuwasujudia majini na kuridhishana nao ili wawatumikie.



Na hii ni dalili kwamba uchawi upo, maana kama haupo, basi Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) asingetukataza kufanya kisichokuwepo.



Pia hadithi hizi zinatufahamisha kwamba mambo haya ni haramu na atakayeyatenda anakuwa amekwishayakanusha yale aliyokuja nayo Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kwa sababu aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ni kwamba hapana aijuwae ghaibu isipokuwa Allaah Subhaanahu wa Taala.

Hadithi ziko nyingi sana, lakini hizi pamoja na aya zilizotangulia zinatosha kuwa ni dalili kwamba yote hayo yametajwa katika Qur-aan na katika mafundisho ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam).
 
UCHAWI UMEANZA ZAMA ZA NABII SULAYMAAN?
Wachawi wanaposoma talasimu zao huwadanganya watu kwa kuanza kusoma baadhi ya aya au sura ndogo ndogo za Qur-aan na kulitajataja jina la Nabii SULAYMAAN na utawasikia daima wanamnasibisha Mtume huyu ('Alayhis Salaam) na kufru zao hizo ili wajinga wanaowafuata wadhani kwamba hayo yamo katika dini.

Uchawi haujaanza zama za Nabii Sulaymaan kama wachawi wanavyozuwa na kumsingizia Nabii Huyu wa Allaah, bali ulikuwepo kabla yake kwa miaka elfu nyingi.

Uchawi ulikuwepo tokea zama za Nabii Saleh ('Alayhis Salaam) aliyekuja kabla ya Nabii Sulaymaan kwa miaka elfu nyingi.

Allaah Anasema:

"Wakasema: (kumuambia Nabii Swaalih); "Hakika wewe ni miongoni mwa waliorogwa."

Ash-Shu'araa - 153
 
UCHAWI NI KUFRU
Wachawi na wafuasi wao hupenda kumsingizia Nabii SULAYMAANi kwa kuinasibisha na kufru yao hiyo na Mtume huyu mtukufu ambaye Allaah alimpa ufalme ambao hajaupata mwengine baada yake kwa kumpa uwezo wa kuwatiisha majini, upepo, na uwezo wa kujua lugha za wanyama n.k.

MwenyezMungu Anasema:

"Basi tukamtiishia upepo unaokwenda pole pole kwa amri yake, anakotaka kufika (unamfikisha).

Pia tukamtiishia Mashaytwaan, kila ajengaye na azamiaye (lulu).

Na wengine wafungwao minyororoni (wanapokhalifu amri zake).”

Swaad - 36-38


Katika tasfiri yake, Ibni Kathiyr amenukuu kauli ya Ibni 'Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa amesema:

"Asif - alikuwa mwandishi wa Nabii Sulaymaan na alikuwa akilijuwa jina tukufu la Allaah (Al ismul aadham), na alikuwa akiandika kila kitu katika daftari kwa amri ya Nabii Sulaymaan na kulificha daftari hilo chini ya kiti cha Nabii Sulaymaani. Alipofariki Nabii SULAYMAAN, majini wakayatoa maandishi hayo wakachanganya na kuandika baina ya kila mistari miwili uchawi na kufru yao, kisha wakawaambia watu wao kuwa hayo ndiyo maandishi ya Nabii Sulaymaan na ndiyo aliyokuwa akiyatenda, na Mayahudi wakayasadiki maneno hayo, wakawa wanamtangazia Nabii huyu kuwa ni mchawi.

Mpaka alipokuja Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na kuteremshiwa aya ya 102 katika Suratul Baqarah:

Allaah Anasema:

"Wakafuata yale waliyoyafuata Mashaytwaan (wakadai kuwa yalikuwa) katika ufalme wa (Nabii) Sulaymaan; na Sulaymaan hakukufuru (Kwa sababu uchawi ni kufru) bali Mashaytwaan ndio waliokufuru wakiwafundisha watu uchawi (waliokuwa wakiujua wenyewe tangu zamani) na (uchawi) ulioteremshwa kwa Malaika wawili Haruta na Maruta katika (mji wa) Babil (Babylon). Wala (Malaika hao) hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie "Hakika sisi ni mtihani (wa kutazamwa kutii kwenu); basi usikufuru. "Wakajifunza kwao (Mashaytwaan) ambayo kwa mambo hayo waliweza kumfarikisha mtu na mkewe (na mengineyo) Wala hawakuwa wenye kumdhuru yeyote kwa hayo ila kwa idhini ya Allaah. Na wanajifunza ambayo yatawadhuru wala hayatawafaa.

Na kwa yakini wanajua kwamba aliyekhiari haya hatakuwa na sehemu yoyote katika Akhera. Na bila shaka ni kibaya kabisa walichouzia (starehe za) nafsi zao (za Akhera). Laiti wangalijua, (hakika wasingefanya hivi)."



Katika aya hii Allaah anatufahamisha pia kuwa uchawi ulikuwepo kabla ya Nabi Sulaymaan kwa miaka mingi, tokea zama za ustaarabu wa Babiloni walipoteremshwa Malaika wawili, Haruta na Maruta ili kuwaonyesha watu na kuwafahamisha nini uchawi, wapate kuujuwa mara watakapouona na wasiufuate, na hii ni kwa sababu uchawi ni kufru.



Watu waliacha kufuata nasaha za Malaika hao na wakajifunza yale ambayo yatawadhuru na wala hayatawafaa, ingawaje walikuwa wakijuwa kuwa aliyekhiari haya hatakuwa na sehemu yoyote katika Akhera.



Wachawi mpaka hivi sasa wanajaribu kuunasibisha uchawi wao na Nabii Sulaymaan pamoja na Malaika hawa wawili.



Tatizo kubwa hupatikana pale wachawi wanapofanya uganga wao pale wanaposema maneno yao ya kichawi. Wao huchanganya maneno hayo na baadhi ya aya za Qur-aan na wanaofanyiwa uganga hudhania kwamba Qur-aan ndiyo inayosomwa na kwa ajili hiyo na kutokana na ujinga wao, huhadaika na kujiingiza nao katika shirki.
 
mashallah nimefurahia sana darsa lako.Mods naomba msiupoteze huu uzi tafadhalini sana!allah akujalie kheri mleta uzi uzidi kuleta suala hili la kheir

never mistaken kindness with weakness
 
Swali, majini hatuyaoni kwa kuwa hayana mwili au yana mwili ili miili yao haionekani, je iwapo wana miili,miili hiyo ni ya namna gani
unaweza tu imagine how jinn look like, only Allah knows jinsi wanavyoonekana
 

Attachments

  • CE_2VmvUkAEjr3X.jpg
    CE_2VmvUkAEjr3X.jpg
    38.7 KB · Views: 76
Kwenye Biblia yanaitwa mapepo na tunayavurumusha kwa jina la Yesu!
 
HUKUMU YA UCHAWI KATIKA DINI YA KIISLAMU
Anasema Imam Maalik (Rahimahu Allaah) katika kitabu chake AlMuwata:

"Mchawi anayefanya uchawi mwenyewe, hukumu yake ni kuuwawa, ama yule anayemuendea mchawi, huyo hauwawi."


Ibni Qudama naye anasema;

"Hukumu ya mchawi ni kuuawa."


Hukmu kama hizi pia zimepokelewa kutoka MaSwahaba mbali mbali kama vile Umar, Uthmaan, Ibni 'Umar na wengine (Radhiya Allaahu anhum).


Hukumu hii ya kuuwawa kwa mchawi pia ameitamka Imam Ahmed bin Hambal (Rahimahu Allaah).



Na imepokelewa kutoka kwa maSwahaba mbali mbali kwamba Umar bin Al Khataab (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliwaandikia maSwahaba kuwaamrisha wamuuwe kila mchawi mwanamke au mwanamume. Anasema mmoja katika maSwahaba kwamba baada ya kupata maandishi hayo waliwakamata na kuwaua wachawi watatu."



Amma Imam Shafi (Rahimahu Allaah), yeye anaona kuwa mchawi asiuliwe isipokuwa akikiri mwenyewe kwamba ameuwa kwa uchawi wake.



Kutokana na yaliyotangulia infahamika kwamba MaSwahaba (Radhiya Allaahu ‘anhu) pamoja na maulamaa wengi wanaona kwamba hukumu ya mchawi ni kuuliwa, isipokuwa Imam Ash-Shaafi'y (Rahimahu Allaah), yeye anaona kuwa auliwe tu ikiwa mchawi huyo atakiri kwamba ameuwa kwa uchawi wake.

 
Back
Top Bottom