Jini, Shetani na wachawi

Jini, Shetani na wachawi

Midekoo

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2015
Posts
45,757
Reaction score
246,786
JINA LAKE
Ameitwa JINNI kwa sababu ya kutokuonekana kwake na watu, na hii ni kwa sababu kila kisichoonekana kwa jicho la binadamu katika lugha ya kiarabu jina lake hutokana (hutoholewa) na herufi mbili hizi; (Jiym) na (Nuun).

Kwa mfano; 'Bustani' huitwa 'janna' kwa sababu ya kuzungukwa kwake na majani kila upande pasiweze kuonekana ndani. Elimu ya uzazi huitwa 'Ilmul ajinna', kwa sababu ya kutokuonekana kwa kile kilichokuwemo tumboni mwa mzazi. Hata mwendawazimu naye huitwa 'majinun' kwa sababu ya kutoweka kwa akili yake. NaMajinni nao wamepewa jina hilo kwa sababu ya kutokuonekana kwao kwa macho ya binadamu.

Ukichunguza utaona kuwa maneno yote hayo; 'Janna, ajinna, majinun, jinni', yana herufi ya 'Jiym na Nuun' ndani yake.


IMANI JUU YA GHAIBU
Kuamini juu ya ghaibu (yasiyoonekana) ni katika misingi ya itikadi ya Dini.

Allaah Anasema:

"Alif Laam Miym. Hiki ni kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake.Ni uwongozi kwa wamchao Allaah. Ambao huyaamini yasiyoonekana (maadam yamesemwa na Allaah na Mtume Wake) na husimamisha Sala na hutoa katika yale Tuliyowapa".

Al Baqarah


Katika aya hizi, Allaah ametaja baadhi ya sifa za wachaji Allaah ikiwemo ikiwemo sifa hii ya kuamini Ghaibu.

Na maana ya neno 'Ghaibu', ni yale tusiyoweza kuyaona tuliyofundishwa na Allaah Subhaanahu waTaala au Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam).


USHAHIDI WA KUWEPO MAJINI KATIKA QUR-AAN TUKUFU

Katika Qur-aan Allaah Anasema:

"Na (wakumbushe) tulipokuletea kundi la majini (kuja kwako) kusikiliza Qur-aan."

Al Ahqaf - 29


Na Akasema:

"(Siku ya Qiyaamah wataambiwa) “Enyi makundi ya majini na wanaadamu! Je, hawajakufikieni Mitume miongoni mwenu kukubainishieni Aya zangu?"

Al An am 130

Itaendelea.......... .............
 
USHAHIDI WA KUWEPO KWA MAJINI KATIKA MAFUNDISHO YA MTU (SWALLA ALLAAHU ‘ALAYHI WA SALLAM) 'SUNNAH'

Katika 'Sunnah', (mafundisho ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), wameelezea Maimam Al-Bukhaariy na Muslim katika vitabu vyao vilivyo sahihi kwamba Ibni 'Abbaas (Radhiya Allaahu anhu) amesema:

"Majinni waliposhindwa kupata siri kutoka mbinguni na wakawa wanafukuzwa kwa vimondo kila wanapojaribu kuzisogelea mbingu, wakarudi makwao. Na jamii zao walipotaka kujua sababu ya kurudi kwao huko na kushindwa kwao kupata siri za mbinguni, maana kabla ya hapo walikuwa wakiweza kupata baadhi ya habari za huko, wakawajibu:

"Pamewekewa vizuizi baina yetu na baina ya (kupata) habari za mbinguni".

Wenziwao wakasema:

"Bila shaka pana jambo kubwa lililotokea, tembeeni ardhi yote Mashariki na Magharibi mtafute ni kitu gani kilichokuzuwieni msiweze kupata habari za mbinguni.”

Walipofika mahali paitwapo; “Soko la Akadha”, waislamu walikuwa wakiswali Swala ya Alfajiri, na majini hao wakaisikia Qur-aan ikisomwa, ndipo waliposema:

"Hii (Qur-aan) wAllaahi, ndiyo iliyokuzuwieni msiweze kupata habari za mbinguni."

Wakarudi kwa watu wao na kuwaambia;

"Enyi jamii yetu! “Hakika sisi tumesikia Qur-aan ya ajabu"

Allaah Amesema katika Suratul Jinn aya ya mwanzo:

"Sema:“Imefunuliwa kwangu kuwa kundi moja la majini lilisikia (Qur-aan) likasema; “Hakika tumesikia Qur-aan ya ajabu.”

Suratul Jinn - 1


Hizi ni dalili zilizo wazi za kuwepo kwa viumbe hawa, na kukanusha kuwepo kwao kwa sababu ya kutokuonekana kwao si hoja maana vitu vingi hatuvioni na tunakubali kwamba vipo kutokana na athari zake. Kwa mfano, joto, baridi, umeme nk. Hivi vyote hatuvioni lakini tunakubali kuwepo kwake baada ya kuona athari zake.
 
DALILI KATIKA QUR-AAN KUWA JINNI AMEUMBWA KWA MOTO
Ndani ya Qur-aan mna dalili nyingi zinazotujulisha kuwa Jinni ameumbwa kwa moto, na tutazitaja baadhi ya dalili hizo:

Allaah Amesema:

"Akasema (Ibilisi); Mimi ni bora kuliko yeye (Mimi) umeniumba kwa moto naye umemuumba kwa udongo".

Al Aaraf -12

Na Akasema:

"Na akawaumba Majinni kwa ulimi wa moto".

Ar Rahman _ 12


DALILI KATIKA MAFUNDISHO YA MTUME (SWALLA ALLAAHU ‘ALAYHI WA SALLAM) KUWA JINNI AMEUMBWA KWA MOTO
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ametujulisha pia kuwa Majini wameumbwa kwa moto, na tutataja baadhi ya kauli zake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam);

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

"Wameumbwa Malaika kwa nuru na Majini kwa ndimi za moto na Adam ameumbwa kwa mliyokwisha elezewa (Udongo)."
 
MAJINI WANAZALIANA
Allaah Anasema:

"Je! Mnamfanya yeye na kizazi chake kuwa marafiki (zenu) badala yangu hali wao ni maadui zenu? Ni mbaya kabisa kwa madhalimu badala (hii)".

Al Kahf - 50


Kauli ya Allaah katika aya hii pale aliposema 'NA KIZAZI CHAKE'. inamaanisha kwamba majini wanazaliana.


WAMEUMBWA KABLA YA BINADAMU
Allaah Anasema:

"Na tulimuumba mwanadamu kwa udongo mkavu unaotoa sauti (unapogongwa), unaotokana na matope meusi yaliyovunda.

Na majini tuliwaumba KABLA, kwa moto wa upepo wenye joto (kubwa kabisa)."

AlHijr- 26-27


Kwa hivyo majini waliumbwa kabla yetu na waliishi katika ardhi hii hata kabla ya kuumbwa kwa Aadam ('Alayhis Salaam), na hii ndiyo maana Allaah alipowaarifu Malaika kuwa anataka kuumba viumbe katika ardhi wakasema:

"Utaweka watakaofanya uharibifu humo na kumwaga damu."

AlBaqarah - 30


Malaika waliuliza suala hili si kwa ajili ya kupinga amri ya Allaah au kwa kumuonea wivu mwanadamu, bali waliuliza kwa ajili ya kutaka kuijua hekima ya kuumbwa viumbe hawa, na hii ni kwa sababu walielewa kutokana na viumbe vilivyotangulia vilivyoishi ardhini, kwamba vina sifa ya ufisadi na umwagaji wa damu.

Anasema Ibni Kathiyr (huyu ni katika maulamaa na mfasiri mkubwa wa Qur-aan) kwamba kabla ya kuumbwa kwa wanadamu, Majinni na viumbe wasiokuwa wanadamu walikuwa wakiishi ardhini na kwamba walikuwa wakifanya ufisadi mkubwa pamoja na umwagaji wa damu.

Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema:

"Majinni waliishi ardhini kabla ya wanaadamu na walikuwa wakifanya ufisadi mkubwa na Allaah akawaondoa na kuwaleta wanadamu."

Maneno kama haya pia yalisemwa na Hassan Al-Basry (Radhiya Allaahu ‘anhu), na akaongeza kusema:

"Hii ndiyo maana Malaika wakamuuliza Mola wao suali hilo."
 
UHUSIANO BAINA YA JINNI NA Shaytwaan
Shaytwaan na Jinni asili yao ni moja, hapana hitilafu baina ya maulamaa kuhusu jambo hili, isipokuwa wamekhitalafiana katika suala; “Je Ibilisi ndiye baba wa Majinni (asili yao) mfano wa Adam ambaye ni baba yetu na asili yetu ?)”

Majibu;

Iblisi si asili yao, bali yeye ni miongoni mwao.

Allaah Anasema:

"Basi wakamsujudia isipokuwa Iblisi; yeye alikuwa miongoni mwa majini."

Al Kahf -50


Kwa vile Allaah Amemtaja Iblisi kuwa ni MIONGONI mwa majini, kwa hivyo yeye ni mmoja wao na si asili yao kama mfano wa Adam ('Alayhis Salaam) alivyokuwa asili ya wanadamu.


Tulisema kuwa wameitwa 'Majinni ' kwa sababu ya kutokuonekana kwao na sisi tumeitwa 'Insaan' kwa sababu ya kusahau kwetu, kwani neno 'Insan', asili yake linatokana na neno 'Nisiyaan', na maana yake ni Kusahau.

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

"Adam alisahau na vizazi vyake vikasahau."

Ama neno 'Shaytwaan', katika lugha ya kiarabu maana yake ni 'Kila anayeasi na kupinga au kuzuwia au kushawishi viumbe wasiifuate njia ya Allaah', awe Jinni au Mwanadamu.

Allaah Anasema:

"Na nama hii tumemfanyia kila Nabii maadui (nao ni) Mashaytwaan katika watu na (Mashaytwaan katika) majini. Baadhi yao wanawafunulia wenziwao maneno ya kupambapamba ili kuwadanganya."

Al An am 112
 
IBILISI NI KATIKA MALAIKA?
Iblisi si katika Malaika, bali ni miongoni mwa Majinni kutokana na dalili zifuatazo:

Allaah Anasema:

"Basi wakamsujudia isipokuwa Iblisi; yeye alikuwa miongoni mwa majini."

Al Kahf -50


Na Akasema:

"Hawamuasi Allaah kwa amri zake; na wanatenda wanavyoamrishwa (yote)."

AtTahrym - 6


Kutokana na aya hii, tunapata ushahidi mwingine kuwa; Malaika hawamuasi Allaah. Kwa hivyo Ibilisi angelikuwa Malaika, asingemuasi Mola wake bali angetenda kama alivyoamrishwa. Lakini yeye alitenda kinyume na hivo. Alimuasi Allaah pale alipokataa kumsujudia baba yetu Aadam ('Alayhis Salaam), akasema:

"Akasema (Ibilisi)‘; 'Mimi ni bora kuliko yeye (Mimi) umeniumba kwa moto naye umemuumba kwa udongo."

Al Aaraf - 12


Na hapa pia tunapata ushahidi mwingi pia kuwa Iblisi si miongoni mwa Malaika, kwani Malaika wameumbwa kwa Nuru na Mashaytwaan wameumbwa kwa moto.

Katika aya iliyotangulia Iblisi alisema:

'Mimi ni bora kuliko yeye (Mimi) umeniumba kwa moto."

Angelikuwa yeye ni miongoni mwa Malaika angelisema;

“Mimi ni bora kuliko yeye umeniumba kwa Nuru".


Kwa sababu Malaika wameumbwa kwa Nuru kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) katika hadithi iliyotangulia:

"Malaika wameumbwa kwa nuru na Majini kwa ndimi za moto na Adam (ameumbwa) kwa mliyokwisha elezewa (Udongo)."

Muslim na Ahmad bin Hanbal
 
AINA ZA MAJINI
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

"Majini (wako) namna tatu, namna moja wana mabawa wanaruka na namna (nyengine) majoka na n’ge na namna nyengine hawaishi mahala pamoja na hupenda kuhama."

Atw-Twabaraaniy na Al-Haakim na Al-Bayhaqiy na imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy


MAHALI WANAPOISHI
Majini wanaishi katika majangwa na katika sehemu za kutupa taka, kwa sababu wao wanakula mabaki ya vyakula vya binadamu.

Zimepokelewa hadithi nyingi pia kwa njia ya Ibni 'Abbaas na Ibni Masaood (Radhiya Allaahu ‘anhum) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alikuwa akienda jangwani na kuwasemesha Majinni na kuwalingania katika dini ya Kiislamu na kuwataka wamuabudu Allaah mmoja wa kweli.

Majinni wanapenda pia kuishi vyooni, na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ametufundisha dua ya kusoma kabla ya mtu kuigia chooni, akasema:

Mmoja wenu anapoingia chooni basi aseme;

"Allaahumma inniy audhu bika minal khubuthi wal khabaaith."

Na maana yake;

“Allaah najikinga kwako kutokana na majini wanaume na majini wanawake.”

Al-Bukhaariy na Muslim.


Majini pia wanaishi katika Mashimo:

Kutoka kwa Qataadah kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

"Mmoja wenu asikojowe ndani ya shimo."

Na alipoiulizwa kuna ubaya gani mtu kukojoa ndani ya shimo akasema:

"Inasemekana kuwa Majinni wanapenda kuishi humo."
 
WANAKULA NA KUNYWA

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

"Mmoja wenu anapokula, basi ale kwa (mkono wa) kulia na anapokunywa anywe kwa (mkono wa) kulia, kwa sababu Shaytwaan anakula kwa kushoto na kunywa kwa kushoto."



Na akasema:

"Mtu anapoingia nyumbani akasema; 'BismiAllaah', na anapokula (akasema BismiAllaah), Shaytwaan husema; 'Hatuna makazi humu (ndani ya nyumba hii), na hatuna chakula cha usiku'. Ama anapoingia asiseme; 'BismiAllaah', Shaytwaan husema; 'Tumepata makazi humu', na asiposema BismiAllaah pale anapokula, basi (Shaytwaan) husema; 'Tumepata makazi na chakula".
 
WANA UWEZO WA KUJIGEUZA
Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alinipa jukumu la kulinda (chakula cha) zaka ya Ramadhani, akaja mtu akawa anaiba katika chakula kile, nikamkamata na kumuambia kwamba nitampeleka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), akasema: 'Mimi ni muhitaji na nina watoto wengi na shida nyingi."

Anasema (Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu):

"Nikamuacha aende zake, na asubuhi yake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akaniuliza:

“Ewe Abu Hurayrah umefanya nini na mfungwa wako jana?"

"Akasema:

"Nikamwambia:

"Ewe Mtume wa Allaah, alinisikitikia shida zake na watoto wengi nikamuonea huruma nikamuacha."

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akasema:

“Ama huyu amekudanganya na atarudi.”

Nikajuwa kwamba atarudi kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema hivyo. Nikamtegea, akaja tena siku ya pili kuiba chakula, nikamkamata, nikamuambia nitakupeleka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Akaniambia:

“Mimi ni muhitaji na nina watoto wengi sitorudia tena.”

Nikamuacha aende zake, na asubuhi yake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akasema:

“Ewe Abu Hurayrah umefanya nini na mfungwa wako jana?”

Nikamuambia:

"Ewe Mtume wa Allaah, alinisikitikia shida zake na watoto wengi nikamuonea huruma nikamuacha."

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akasema:

"Ama huyu amekudanganya na atarudi."

Nikamkamata mara ya tatu akiwa anaiba (tena) chakula, nikamuambia:

"Nitakupeleka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na hii ni mara ya tatu na kila mara unasema hutorudia kisha unarudia."

Akasema:

"Niache nikufundishe maneno Allaah atakufaa nayo."

Nikamuuliza;

“Maneno gani hayo?"

Akasema:

“Unapokuwa juu ya tandilo lako soma Ayatul Kursy - Allaahu laa ilaaha illa huwal hayyul qayuum - mpaka mwisho na itaendelea kukuhifadhi aya hii na hatokukaribia Shaytwaan mpaka utakapoamka.”

Nikamuacha aende zake.

Asubuhi yake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akaniuliza:

“Amefanyaje mfungwa wako jana?”

Nikamuambia:

"Ewe Mtume wa Allaah amejidai eti amenifundisha maneno ambayo Allaah Atanifaa nayo, basi nikamuacha huru."

Akaniuliza;

“Ni maneno gani hayo?”

Nikasema:

"Ameniambia:

“Unapokuwa juu ya tandiko lako soma Ayatul Kursy mpaka mwisho na Allaah ataendelea kukuhifadhi nayo na hatokukaribia Shaytwaan mpaka utakapoamka."

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akasema:

"Ama yeye amesema kweli ingawaje ni muongo. Unamjua nani uliyekuwa ukizungumza naye siku tatu hizi ewe Aba Hurayrah?"

Nikajibu:

"La simjuwi".

Akasema:

“Yule ni Shaytwaan.”

Al-Bukhaariy


Kwa vile Shaytwaan huyu aliyekuwa akiiba alikuwa akimjia Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwa sura ya binadamu, basi hii ni dalili kwamba majini wanao uwezo wa kujibadilisha umbile lao.
 
WAMO MIONGONI MWAO WANAWAKE NA WANAUME
Katika hadithi niliyoitaja hapo juu Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alisema:

"Anapoingia mmoja wenu chooni, basi aseme:

“Allaah najikinga kwako kutokana na majini wanaume na majini wanawake




WANAOWA?
Majini wanaoana na kuzaliana, na ushahidi umo ndani Qur-aan katika kauli Yake Subhanahu wa Taala Aliposema:

"Je! Mnamfanya yeye (Ibilisi) na kizazi chake kuwa marafiki (zenu) badala yangu hali wao ni maadui zenu? Ni mbaya kabisa kwa madhalimu badala (hii)."

Al Kahf - 50


Hata hivyo Maulamaa wengi hawakubali majini waowane na wanadamu.

Pana kisa cha mwanamke mmoja kutoka Yemen alikuwa akidai kwamba anajiwa na jinni na kwamba jinni huyo anataka kumuowa. Alipoulizwa Imam Malik kuhusu jambo hili akasema:

“Sioni kifungu chochote cha sheria kinachoharamisha, isipokuwa nakuogopeeni fitna (Mitihani).”


Maulamaa wamesema kuwa kauli ya Imam Malik hii inatujulisha juu ya hofu yake, kwani mwanamke yeyote anaweza kujipatia mimba kwa njia zisizo za halali, kisha akasema kwamba ameolewa na jinni na kwa njia hii uhuni utazidi na fitna zitaenea.

Maulamaa wengine wamekataa kabisa fikra ya kuoana baina ya majini na wanadamu wakiegemea kauli ya Allaah Isemayo:

"Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mupateutulivu kwao."

Ar-Ruwm - 21


Na Akasema:

"Na Allaah amekuumbieni wake katika jinsi yenu na akakujaalieni kutoka kwa wake zenu watoto na wajukuu."

An-Nahl - 72


Katika aya hizi Allaah anatufahamisha kwamba ametuumbia wake zetu katika jinsi yetu, wakati Majinni si katika Jinsi yetu.

Na akasema; “Ili mupate utulivu kwao", wakati mwanadamu hawezi kupata utulivu kwa jinni, maana siku zote mtu hupata utulivu kwa kiumbe aliye mfano wake na majini si mfano wetu.

 
MAJINI WANAKUFA?
Allaah Anasema:

"Kila kilichopo juu yake (ardhi na mbingu) kitatoweka (kitaondoka)."

Ar-Rahmaan - 26



Na Akasema:

"Hakuna aabudiwaye kwa haki ila Yeye; kila kitu kitakufa isipokuwa Yeye (Allaah basi)."

Al-Qaswas - 88


Inavyojulikana ni kwamba Iblisi yuhai mpaka siku ya Qiyaamah.

Allaah Amesema:

"Akasema (Iblisi); “Mola wangu! basi nipe nafasi (nisife) mpaka siku watakayofufuliwa (viumbe) vyote.”

Akasema (Allaah); “Hakika wewe (nimekwisha kukufanya) katika wale waliopewa nafasi.

Mpaka siku ya wakati uliowekwa (ukifika wakati huo utakufa).”

Al-Hjr - 36 -37-38


Kwa hivyo Ibilisi ataishi mpaka siku maalum anayoijua Allaah peke yake kisha atakufa, na majini nao pia wanazaliana na wanakufa kama sisi.
 
mashallah nzur sana endelea dada etu

never mistaken kindness with weakness
 
Back
Top Bottom