Jini, Shetani na wachawi

Jini, Shetani na wachawi

KUJIKINGA NA SHARI ZA WACHAWI NA MAJINI WAO
Zifuatazo ni baadhi ya Njia za kujikinga na waovu hao:



KUSAFISHA NIA

Ibilisi alipohukumiwa kupotea kwa sababu ya kuasi kwake, aliahidi kuwapoteza viumbe wote isipokuwa wale waliosafika kikweli.

Ibilisi akasema kumwambia Allaah:

"Isipokuwa wale waja wako waliosafika kweli kweli."


Kusafisha nia (Al Ikhlas), maana yake ni kuzihusisha Ibada zote kwa moyo wote kwa ajili ya Allaah peke yake, siyo kujionyesha mbele za watu kuwa ni Mcha Mungu na unapokuwa peke yako unamuasi.

Al Junaid, mmoja katika maulamaa wakubwa wa wakati wake amesema:

"Allaah ana waja wake wenye akili, walipopata akili wakaifanyia kazi, walipofanya kazi wakaitakasa kazi hiyo na kule kuitakasa kwao kukawaingiza katika milango ya kheri yote."


KUTIA UDHU

Katika hadithi nyingi Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ametufundisha juu ya umuhimu wa kubaki na udhu kila mtu anapoweza kwa ajili ya kupata thawabu na kwa ajili ya kujikinga na kila shari.


SWALA KATIKA JAMAA

KusWali sWala za jamaa msikitini, maana Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ametufundisha kwamba mbwa mwitu (Shaytwaan) huwala kondoo wanaotembea mbali na wenzao.


SWALA ZA SUNNAH

Swala za Sunnah uziswali nyumbani, usiiache nyumba yako ikawa kama kaburi, na unaposwali nyumbani Shaytwaan hulia na kutoka nje ya nyumba yako huku akisema;

"Sina pa kulala humu, wala sina pa kula humu".




KUMUOMBA ALLAAH

Kumuomba Allaah kila mara Shaytwaan anapotaka kukuchezea na kila unapoingia mahali pachafu. Kwa mfano:

Unapoingia chooni uisome dua ifuatayo:

"Allaahumma inniy audhu bika minal khubuthi wal khabaaith). Na maana yake; (Allaah mimi najikinga kwako kutokana na majini wanaume na majini wanawake).


Kabla ya kulala usome Suratul Ikhlaas, Suratul Falaq na Suratul Naas pamoja na AyatulKursy, maana hadithi sahihi tuliyoitaja mwanzo wa darsi hii inasema kuwa anayeisoma aya hii, Allaah anaendelea kumhifadhi mpaka asubuhi anapoamka.

Ni vizuri pia kuzisoma aya tano za mwanzo za SuratulBaqarah kisha Ayatul Kursy kisha kuzisoma aya tatu za mwisho za Suratul Baqarah na Allaah Atakulinda na majini pamoja na uchawi katika siku nzima.



Kuzisoma dua mbali mbali kama vile:

(Audhu bikalimati Allaahi ttaamah min kulli shaytanin wa haammah wa min kulli aynin laammah).

Na maana yake ni;

"Najikinga kwa Allaah kutokana na kila Shaytwaan na (kila) mdudu anayesota (kama vile nge na nyoka nk. na kwa kila jicho linalodhuru).

(BismiAllaahi lladhiy laa yadhuru ma-a smihiy shayun fil ardhi walaa fiy ssamaa wahuwa ssamiyl aliym).

Unapotoka nje ya nyumba usome:

(BismiAllaah tawakkaltu ala Allaah walaa haula walaa quwwata illa biAllaah)
 
DUA ZINAMKUMBA SHAYTWAAN
Kama vile Shaytwaan anavyoweza kuwakumba wanadamu walioghafilika na kumdhukuru Allaah, Shaytwaan naye pia hukumbwa na dua za wanaomdhukuru Allaah:

Imeelezwa na maulamaa kuwa, Shaytwaan anapojaribu kumsogelea mchaMungu mwenye kumdhukuru Mola wake kila wakati kwa ajili ya kumkumba, basi dua zake humkumba Shaytwaan huyo na kumuangusha chini. Kisha Mashaytwaan wenzake hukusanyika na kuulizana:

"Amepatwa na nini huyu?"

Wenzao huwajibu:

"Amekumbwa na binadamu."


DHIKRU ALLAAH
Kwa kumaliza napenda kujikumbusha nafsi yangu kwanza na pia kuwakumbusha ndugu zangu Waislamu pia kwamba, hakuna kinga kubwa inayomkinga mtu kutokana na kila balaa baada ya Qur-aan kama kumdhukuru Allaah.



Kumdhukuru unapolala, unapoamka, unapotoka nyumbani, unapositushwa na jambo, unapofurashishwa. Katika kila jambo lako jema au lisilo jema, bali hata katika kumuasi Mola wako unapomkumbuka Allaah na kukumbuka uwezo Wake juu yako na neema Zake juu yako mara utayaacha maasi hayo.



Na ukumbuke kwamba kwa msaada wake Yeye tu Subhanahu wa Taala utaweza kujikinga na kila balaa.




USIINGIZE NDANI YA NYUMBA YAKO VIFUATAVYO
Mwisho kabisa ningependa kukumbusha kuwa ndani ya nyuma yako usije ukaingiza yafuatayo;

Usitundike picha yeyote ile.

Usisikilize nyimbo.

Usiweke baraza za kusema watu au kutukana watu.

Usitizame filam za sinema nk.

Hayo yote yanakaribisha Mashaytwaan katika nyumba yako na yanafukuza Malaika.

Allaah Anasema:

"Na kama wasiwasi wa Shaytwaan ukikusumbua basi sema (AudhuBiAllaahi), jikinge kwa Allaah (na kuchezewa na Shaytwaan), Bila shaka Yeye ndiye asikiaye na ajuaye.

Hakika wale wanaomuogopa (Allaah) zinapowagusa pepesi za Shaytwaan, mara hukumbuka, tahamaki wamekweshaona njia.

Na ndugu zao (wale walioasi) wanawavutia katika upotofu (upotevu kisha wao hawaachi).”

Mwisho
Chanzo :Alhidaya
 
Kwa imani yetu wakiristo majini au mapepo ni kazi ya Shetani. Hakuna jini mzuri wala mbaya ila wote nikazi ya shetani. Aidha katika uumbaji Mungu aliumba Malaika na binadamu na wote walikuwa safi wakimtii na kumtukuza Mungu wao. Uasi uliofanywa na Ibilisi au shetani dhidi ya Mungu ndio chanzo cha dhambi na yeye pamoja na thelusi ya malaika waliomuunga mkono walitupwa na kufukuzwa kutoka mbinguni. Malaika hao waliotupwa pamoja na Ibilisi ndio majini au mapepo. Ndio maana jini au pepo lolote likisikia Jina na la Yesu Kristo mwana wa Mungu alie hai likitajwa lazima lipige kelele au kuliasana kwani wao waasi.
 
Hahaha....Ila sio siri Allah anachekeshaga sana.

😛🙂😀
 
MAJINI WANAKUFA?
Allaah Anasema:

"Kila kilichopo juu yake (ardhi na mbingu) kitatoweka (kitaondoka)."

Ar-Rahmaan - 26



Na Akasema:

"Hakuna aabudiwaye kwa haki ila Yeye; kila kitu kitakufa isipokuwa Yeye (Allaah basi)."

Al-Qaswas - 88


Inavyojulikana ni kwamba Iblisi yuhai mpaka siku ya Qiyaamah.

Allaah Amesema:

"Akasema (Iblisi); “Mola wangu! basi nipe nafasi (nisife) mpaka siku watakayofufuliwa (viumbe) vyote.”

Akasema (Allaah); “Hakika wewe (nimekwisha kukufanya) katika wale waliopewa nafasi.

Mpaka siku ya wakati uliowekwa (ukifika wakati huo utakufa).”

Al-Hjr - 36 -37-38


Kwa hivyo Ibilisi ataishi mpaka siku maalum anayoijua Allaah peke yake kisha atakufa, na majini nao pia wanazaliana na wanakufa kama sisi.
Ulishaona maiti ya Jini? makaburi yao yako wapi?
 
Kwa imani yetu wakiristo majini au mapepo ni kazi ya Shetani. Hakuna jini mzuri wala mbaya ila wote nikazi ya shetani. Aidha katika uumbaji Mungu aliumba Malaika na binadamu na wote walikuwa safi wakimtii na kumtukuza Mungu wao. Uasi uliofanywa na Ibilisi au shetani dhidi ya Mungu ndio chanzo cha dhambi na yeye pamoja na thelusi ya malaika waliomuunga mkono walitupwa na kufukuzwa kutoka mbinguni. Malaika hao waliotupwa pamoja na Ibilisi ndio majini au mapepo. Ndio maana jini au pepo lolote likisikia Jina na la Yesu Kristo mwana wa Mungu alie hai likitajwa lazima lipige kelele au kuliasana kwani wao waasi.


Imani ya kikristo inakuambia MALAIKA aliumbwa kwa kutumia nini ?
 
Hadithi zimekuwa nyingiii Sana zote ubatili mtupu Theory juu ya Theory.
 
Back
Top Bottom