Jino lina msaada gani jeshini wandugu?

JEKI

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
4,845
Reaction score
2,957
Rafiki yangu karudishwa kutoka jeshini, kisa ana kilema, kilema chenyewe ni kuwa ana pengo, jino moja la mbele halipo, yeye anaseme alijitetea sana kwa kusema siyo pengo ila ni mwanya tu, kiukweli hata mimi sijuagi kama kweli ni pengo au ni mwanya. Lakini anasema watu wengi wamerudishwa kwa vijeraha vidogo vidogo sana, wengine kwa kuwa na kovu au kushonwa nyuzi 2 tu mguuni. Cha kujiuliza, hivi jino lina msaada gani hadi limkoseshe mtu mwenye nia njema ya kulitumikia Taifa lake katika kazi hii ngumu, kazi ya hatari, kazi ya kuweka rehani maisha yako. Binafsi majeshi ya sasa yapo modernized, kinachotakiwa ni akiri tu, nguvu tena haina nafasi.
 

Si jino tu, hata kama una unyayo ambao hauna uvungu..kuna wale watu sijui walibemendwa utotoni basi nyayo zao zinakua kama za bata! hawachukuliwi kwakua hawawezi kusimama na kutembea umbali mrefu, hata kuna aina ya kazi huwezi fanya kama una mwanya hata kama mwembamba kiasi gani, kama kua air hostes/ carbin crew etc! usishangae huyo mapengo wako kurudishwa..mpe pole!
 
elimu yangu inahusika vp hapa? Flammable
 
Last edited by a moderator:
Umenikumbusha enzi hizo Tabora boys ikiwa bado ya jeshi joining instruction ilisema kama una kilema badilisha shule, jamani kwani walipenda au watafutiwe nao jeshi litakalochukua watu wenye mapungufu fulani katika miili yao au ulemavu.
huyu jamaa si akaweke jino la bandia mjomba? au walishamchukua vidole tayari!
 
Rafiki yako atakuwa amekudanganya au kuna kitu anakuficha......hatua ya mwisho ya mchujo ambayo hufanywa na ma dr wao ni kupima afya yako, hapa wanakuwa makini sana maana unaweza kujiona upo fit kumbe una tatizo lililojificha......nimeshamshudia ndg yangu akikosa nafasi pamoja na kuwa na refarii wa maana (kakaake ni major general)
Kwa kifupi ni kuwa ma dr wao wapo makini sana kwa sababu ya kuepusha vifo vingi vinavyotokea kipindi cha mafunzo
 

huenda si kweli. JKT mujibu wa sheria huwa hawabagui huyu kilema au ana ugonjwa gani wa kimaumbile. wale wana wataalam wao na lazima watakuweka katika kundi fulani uendelee na jeshi - utakumbuka kuna wale wakiitwa MAKASHUA huenda neno hili linatokana na neno CASUALITY wanaendelea na jina hilo hadi wanakamilisha muda

Kuna jamaa mmoja wa mujibu yeye siku ya kwanzaa tu alikuwa anachecheme kama vile ana kilema - alijulikana ni kashua na aliendelea na jeshi. kwa mshangao wa kila mtu siku ya kumaliza jeshi alitimua mbio kawaida kuelekea kupanda basi lililokodishwa kuja wachukua wahitimu na kwenda nyumbani - litakua PENGO!!!
 
Dah, nimesoma hii sred nikiwa nakunywa maji.
Nimejikuta maji yote yamerukia kwenye laptop yangu.

Kuna watu mna vipaji ila mnavipotezea tu.
 
Wanaoenda kwa mujibu wa sheria wote wanapokelewa isipokua wajawazito tu..
 
Inasemekana ukiwa na pengo kuna baadhi ya #SILAHA hutoweza kuzifungua na hiyo ndo maana yake ila kuna wengi tu wanaenda!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…