JEKI
JF-Expert Member
- Aug 16, 2013
- 4,845
- 2,957
Rafiki yangu karudishwa kutoka jeshini, kisa ana kilema, kilema chenyewe ni kuwa ana pengo, jino moja la mbele halipo, yeye anaseme alijitetea sana kwa kusema siyo pengo ila ni mwanya tu, kiukweli hata mimi sijuagi kama kweli ni pengo au ni mwanya. Lakini anasema watu wengi wamerudishwa kwa vijeraha vidogo vidogo sana, wengine kwa kuwa na kovu au kushonwa nyuzi 2 tu mguuni. Cha kujiuliza, hivi jino lina msaada gani hadi limkoseshe mtu mwenye nia njema ya kulitumikia Taifa lake katika kazi hii ngumu, kazi ya hatari, kazi ya kuweka rehani maisha yako. Binafsi majeshi ya sasa yapo modernized, kinachotakiwa ni akiri tu, nguvu tena haina nafasi.