Miaka kumi iliyopita niliwahi pata tatizo la jino lilikuwa likiuma sana, nikauliza watu wakanielekeza kwa dr mmoja kkoo nikaenda.
Sasa dr ameona akasema hili ni la kutoa limeharibika vibaya hakuna namna litaweza kuzibika nikakubali.
Changamoto ilianzia nimekaa kwenye dental chair kuna sahani ilikuwa na mikasi zadi ya ishirini dr akiiweka vizuri huku akiwa bado anaweka gloves zake sawa nikamuomba niende toilet.
Niliingiwa na woga nikaamua kuondoka eneo lile haraka sana, ila sasa nilikiwa njiani maumivu yalikuwa makali sana.
Kwa kweli usiku sikulala hata kidogo kutokana na maumivu ikabidiasubuhi kulipo pambazuka niwahi pale.
Dr hakunikumbuka ila baada ya kuona jino akakumbuka kuwa jana ni mimi niliemkimbia, ilibidi nikubali tu na nilapigwa sindano za ganzi kwa taabu sana lkn zoezi likakamilika.