Jino na sehemu pekee iliyobaki ya Patrice Lumumba yaibiwa Congo DRC

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,547
Reaction score
7,167
Jino la waziri Mkuu wa kwanza wa Congo limeibiwa jijini Kinshasa. Ikumbukwe waziri Mkuu Patrice Emilio Lumumba aliuliwa mwaka 1961 na Mwili wake kuyeyushwa kwenye tindikali.

Ilivyo bahati mmoja wa wauaji Askari Mbeligiji aliliondoa jino lake kwa siri bila kumfahamisha mtu yeyote. Baadae aliitoa siri hiyo na kudai amelificha nyumbani kwake Ubelgiji baada ya miaka mingi kupita.

Serikali ya Congo DRC iliwasiliana na serikali ya Ubelgiji na Askari huyo na jino kurudishwa nyumbani ikiwa ndani ya Jeneza na kuhifadhiwa eneo maalumu jijini Kinshasa mwaka 2022.

Nyumba maalumu iliyohifadhi jeneza na jino imeharibiwa usiku wa jumapili 17/11/2024 na jino kuibiwa na watu wasiojulikana.

Hata hivyo walinzi wa Rais waliliona jeneza likitoroshwa na kuliokoa huku jino halipo ndani na waporaji walishakimbia. Inadaiwa kaburi hilo halikuwa na ulinzi maalumu japo halipo mbali na Ikulu ya Kinshasa.

Awali kurejeshwa kwa jino hilo kulipokelewa kwa shangwe na wakongomani wa matabaka yote.
 
Dunia ina mambo ya kushangaza na kusikitisha.
 
Ni wapuuzi tu na wanatia aibu kwa waafrika, wanaiba jino watalifanyia nini kama si ushirikina?
 
Afrika imejaliwa mambo mengi na uhalifu pia
 
Ni wapuuzi tu na wanatia aibu kwa waafrika, wanaiba jino watalifanyia nini kama si ushirikina?
Tena jino lenyewe limeombwa lirejeshwe siku nyingi, limerejeshwa na wahuni wakaliiba.
 
Dah!....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…