Jinsi AI Inavyoharibu Maisha Yako Kimya Kimya

Jinsi AI Inavyoharibu Maisha Yako Kimya Kimya

Ngoja wataalam wa graphics design waje
Kwa mfano ningekuwa bado natafuta hela kwa njia ya picha wenyewe wanaozihitaji wanaita picha za kubadili mazingira ningepiga hela sana. Kila siku nisingekosa kuanzia 100,000/= kwa msaada mkubwa wa bwana ChatGPT.

Hakuna kuhangaika na liphotoshop au kwenda photo studio kutengeneza picha hizo. Ni kumpiga picha mhusika, Kisha unaprompt kulingana na mhusika wa picha anataka aonekane, ndani ya dakika picha yake tayari, unamwonyesha anatoa hela.
 
Nakubali mkuu ni nzuri sana lakini je muafrika anaitumiaje? hapo ndipo mjadala ulipo.
Hatupo serious na technologia mkuu, sisi majungu mengi, kutekanatekana kijinga, kushinda kanisani na msikitini kila dakika.

Ebu angalia hizi website, ni ndogo tu lakini inaonyesha wazi technlogia inakuja kwa speed sana

1. IntelBase

2. Base44
 
Unakumbuka maisha kabla ya Google au calculators watu walisema nini?

Watu walisema hivi hivi kwamba tutakuwa wajinga, lakini ndio kwanza tumekuwa wabunifu zaidi. AI inafanya zile kazi za kishamba na za kuchosha ili sisi tubakiwe na muda wa kufanya high level thinking, inatupa nafasi ya kufikiria mambo makubwa zaidi!
 
Ikitumika vizuri hakuna shida na wala sijasema haifai ila Kuna watu AI Ina watawala badala wao waitawale AI
 
Mkuu dunia inaenda mbele hairudi nyuma. Nakumbuka mwaka 2014 kuna mwalimu mmoja mhitimu wa UDSM alikuwa anaona watsapp kama kitu cha kihuni. Ukimwambia nitumie list ya vitu unavyotaka nisupply anakujibu andaa kalamu na karatasi nikupigie simu uwe unaandika. Mkuu AI ndo kwanza iko mwanzoni sana.. bado ni dhaifu. Siku zijazo itasababisha ajira kama za uigizaji filamu kupotea.
 
Hivi Photoshop na wenzake bado ana maringo kama livyokuwa anatulingia miaka ya 2013 kushuka chini baada ya ujio wa AI?
yaani toleo la adobe 2026 iko friendly mno, yaani ina kila kitu sasa hivi, na no hidden tools
 
Back
Top Bottom