Jinsi Ajira Portal Ilivonipotezea kipenzi changu!!

Jinsi Ajira Portal Ilivonipotezea kipenzi changu!!

kante mp2025

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2022
Posts
631
Reaction score
1,192
Wagonga ulimbo tunapitia mengi sana maisha yanakuchapa, mapenzi yanakupiga za uso, familia inakutenga, marafiki wanakukimbia.

Katika harakati zangu za ugonga ulimbo baada ya kugraduate mimi na kipenzi changu "Fauzia" jina la uficho (comouflage)tulikuwa na mipango mingi sana.

Siku zote niliamini nitamuoa fauzia ukizingatia alikuwa binti fulani aliyefunzwa akafunzika.Japo tuliishi mbali mbali ila wote tulitokea mkoa mmoja hivo yeye alipomaliza tukasema tupambane hapa hapa mjini kutimiza malengo yetu kwa pamoja.

Mimi nikafanikiwa kujishikiza kwenye kazi ya mgahawa mjini kati ambapo nilikuwa nalipwa kitita cha laki moja mkononi.Fauzia wangu nae si haba akawa anajishughulisha na shughuli ya kupika misosi pale getho kisha kwenda kuiuza kwenye vijiwe vya boda na wakati mimi nikiwa na free time nilikuwa namsaidia hakika nilimpenda sana na niliamini ananipenda sana.

Basi nakumbuka 2020 mwezi january ndipo magamba yetu ya vyuo yalitoka baada ya kuhitimu november 2019 yeye alikuwa kozi X na mimi nilikuw kozi Y.

Hivo wakati tunaendelea na harakati za ugonga ulimbo tulikuwa tukipitia mara kwa mara website ya ajiira portal huku nikijaribu kumpa mwongozo wa kuomba ajira ukizingatia nilikuwa vizuri kiasi kwenye masuala ya mtandao yeye hakuwahi kuwa mwanamitandao kabisa.

Basi alikuwa akiitwa interview aiienda kwenye usahili nyingi alikuwa hafanikiwi nikawa namtia sana moyo nakumbuka hadi tushawahi funga kwa maombi jumapili moja ili akafanye vzuri interview yake siku ya jumatatu.

Mimi sikuwa naitwa sana kwa interview kutokana na kozi yangu kuwa nadra sana kutangazwa ajira, Niliishi nikiamini jambo la fauzia ni jambo letu sote kumbe ulikuwa UTOTO

Mungu sio Dotto Magari asee kuna siku kama zari nikiwa napitia pdf za placement nikakutana na jina la dear ex wangu fauzia asee nilifurahia sana sana nilipofika home nikampa habari hizo nae aliruka ruka kwa furaha kisha tukakumbatiana na kuugeuza usiku ule kuwa usiku wa twanga pepeta kufurahia mafanikio hayo.

Lakini nikamshauri pia fauzia katika yale mapato ya mama ntilie tusiache kutoa sadaka ya shukrani kwa jambo lile hivo tukaenda kusalimia kituo kimoja cha watoto yatima.

As a man niliwish na mimi walau ningepata kazi nikawa nimepoa kiasi fauzia akawa amenisoma akawa ananipiga piga kifuani kuwa nisiogope ipo siku nami nitapata nikafarijika sana.

Basi bhana michakato ya kuripoti kazini ikaanza hapo ndipo ajira portal ilimpeperusha njiwa wangu,Nakumbuka nilimsindikiza hadi rose migiro kwa boda ya rafiki yangu kuchukua barua yake ya kuripoti kazini siku chache zijazo.

Alikuwa kapangiwa mkoa X mbali kiasi na nilipokuwepo nikamsupport kiuanaume michakato yote ya safari ikiwemo kumkatia tiketi na kumsindikiza hadi kituoni kwake kwa kazi kuhakikisha kapolewa vema kisha nikarudi zangu kuendelea na harakati za ugonga ulimbo maana fauzia alinambia nijipe muda kiasi then atakuwa ananitembelea au laa niwe namtembelea.

Hapo ndipo mauza uza yalianza mwanzo fauzia alikuwa ni mtu wa kunitafuta kila akirudi kazini baada ya miezi miwili hiyo ikafa nikawa nikituma meseji najibiwa niko kwa kikao siku zilivoenda nikawa sijibiwi kabisa, Nikimpigia fauzia ananijibu kiufupi sana baadae akaacha kabisa kunijibu roho wa bwana akanena nami kuwa hapo parapanda ishalia maana kuna siku alinambia ukweli kuwa niache kumsumbua yupo na mume wake

Fauzia kwa sasa ana watoto wawili na kaoelewa na bwana mwenye mipesa mimi bado nipo na harakati zangu za ugonga ulimbo huku nikimngojea bwana maana na mimi kwa mara ya kwanza nimefanikiwa kuingia oral ajira portal.

Nilichojifunza Wanawake Ni Opportunist, Asante Yesu Sikujinyonga Nakesha Kuendesha Boda kama mpumbavu.
 
Pole Mkuu..!!!
umenikumbusha mbali sana, Siku nililala Hostel za UDOM, wanyewe wanapaita CBSL nikiwa Ghorofani naziona ofisi za PSRS usiku nzima nawaza barua yangu ya kuripoti kituo cha kazi.
Yale maeneo nayamiss sana.
 
Pole Sana ,mlango mmoja unapofungwa milango mingine inafunguka usikate tamaa kupitia Fauzia Naamini kuna jambo ulilojifunza
 
Pole Mkuu..!!!
umenikumbusha mbali sana, Siku nililala Hostel za UDOM, wanyewe wanapaita CBSL nikiwa Ghorofani naziona ofisi za PSRS usiku nzima nawaza barua yangu ya kuripoti kituo cha kazi.
Yale maeneo nayamiss sana.
natamani na mimi nkafwate barua yangu siku moja
 
😅Nimecheka kifala babu, we share same story am also a bajaji driver mzee holding bachelor degree in business administration mkuu, also a driver sometimes six car gear especially land cruiser, if I get green pastures sometimes

Also, the loml after she seduced by a man with three keys, I was ghosted mzee

So manigger let's pushing we still young and energetic
 
one day yes ma brodah, bado kiumbe wa Mungu nina imani tele
 
Usije ukaacha kutimiza ndoto zako eti unapoteza nguvu zako kupambania ndoto za mtu mwingine ili akifanikiwa aje nawewe akuvushe huo ni upumbavu,

Achilia mbali rafiki hata ndugu yako usijaribu labda kama ni mama yako mzazi ndio akipata atakukumbuka.
Binadamu tumeumbwa kusahau na mtu anapopata upenyo anaenda kukaa na wenzake wenye hadhi kama yake.

Kikubwa ni kupigania ndoto zako wewe kama wewe bila kulaumu mtu ufike unapopataka wewe, ukifanikiwa wataanza kurudi utashangaa hata na huyo X wako ataanza kukutafuta tena.
 
Pole mkuu huu ni ukweli mtu but usife moyo Mungu atakuona na haya yote yatabaki kua simulizi tu
 
Usije ukaacha kutimiza ndoto zako eti unapoteza nguvu zako kupambania ndoto za mtu mwingine ili akifanikiwa aje nawewe akuvushe huo ni upumbavu,

Achilia mbali rafiki hata ndugu yako usijaribu labda kama ni mama yako mzazi ndio akipata atakukumbuka.
Binadamu tumeumbwa kusahau na mtu anapopata upenyo anaenda kukaa na wenzake wenye hadhi kama yake.

Kikubwa ni kupigania ndoto zako wewe kama wewe bila kulaumu mtu ufike unapopataka wewe, ukifanikiwa wataanza kurudi utashangaa hata na huyo X wako ataanza kukutafuta tena.
Ulikuwa utoto nishajifunza mkuu
 
😅Nimecheka kifala babu, we share same story am also a bajaji driver mzee holding bachelor degree in business administration mkuu, also a driver sometimes six car gear especially land cruiser, if I get green pastures sometimes

Also, the loml after she seduced by a man with three keys, I was ghosted mzee

So manigger let's pushing we still young and energetic
Hii ni lugha gani wakuu?
 
Back
Top Bottom