ubarinolutu
JF-Expert Member
- Oct 22, 2012
- 2,424
- 4,954
Ali kiba ameendelea kuleta umaskini kwa washabiki wake, na kuwapunguzia uhuru wa kupata burudani. Mashabiki wa ali kiba wanatumia nusu ya kipato chao kununua bando ilimradi waweze kuangalia video ya Seduce me 24/7 na hivyo kufanywa mazezeta, kwani bando wanaloweka ni kwa ajili ya ali kiba na si kitu kingine cha kuleta maendeleo, wengine wameenda mbali zaidi hadi kuchukua mkopo ili kupata bando la kutosha kupambana na Diamond. Pia mashabiki wake wengi wamekuwa ombaomba, kila muda kuomba vocha ya bando. Pia kwetu cc baadhi ya wanaume tunaumia sana maana wapenzi wetu(mademu ) wengi ni timu kiba na tunaombwa pesa ya bando kila siku. Kama mnavyojua washabiki wa ali kiba 90% ni kina dada mfano jokate, wema, zamaradi, wolper, uwoya so ni shida.
Jambo jingine ni la kuwa na uhuru mdogo kwa mashabiki wa ali kiba kwani hawaruhusiwi kuangalia nyimbo nyingine kabisa zaidi katika you tube yaani ni marufuku wanapaswa kuangalia seduce me huku nyimbo nyingine kali zikiwapita pembeni. Kitu cha ajabu kabisa lazima tukuze mziki wetu tuangalie nyimbo zote kwa maana zote ni nzuri.
Mwisho kabisa kuna kitu kama nimekiona Kuna kaushindani you tube kati ya Seduce me na Zilipendwa na ninaona yeyote atakayelegeza atapitwa view so inawezekana washabiki wa watu hawa hawalali wanashinda you tube muda wote, wanateseka sana na watakuja kuumwa. Diamond na alikiba mtaua vijana wa watu na dhambi mtapata na moto mtachomwa.
Pia mange amesema diamond ameshaharibika kisaikolojia baada ya kushindwa battle na kiba hiyo nakubali lakini yote haya alijitakia kumdiss mtu ambaye alikuwa kimya. Pole baba hamisa