Inck
New Member
- Sep 8, 2021
- 2
- 2
Je, umewahi kujiuliza ni kwanini watu wengi wanaamini kuwa bila kwenda kwa mganga huwezi fanikiwa? Bila shaka umewahi kujiuliza, lakini je, ulishawahi kwenda mbele kidogo na kujiuliza ni kwa namna gani hawa waganga huwafanya watu kuwa matajiri? Ni watu wachache hujiuliza swali hili. Basi dhamira ya andiko hili ni kukufahamisha kwa ushahidi yakinifu wa namna gani hasa waganga huwawezesha baadhi ya watu kufanikiwa kiuchumi.
1. Hitaji la dhati la muhusika kutaka kuwa tajiri
Ni dhahiri kuwa mpaka mtu anaamua kwenda kwa mganga kutafuta utajiri, basi mtu huyo anayo nia ya dhati ya kufanikiwa. Basi kwa kigezo hicho tu, mtu huyo anakuwa ameshafaulu katika hatua ya kwanza ambayo ni "kuwa na nia ya dhati ya kufanikiwa". Kwahiyo sasa, kitakachompelekea mtu huyo kufanikiwa sio nguvu ya mganga bali ni utayari na uthubutu wake katika kutaka kufanikiwa.
2. Masharti ya waganga hujikita katika nidhamu ya pesa na kujituma katika kazi
Masharti kama; Huruhusiwi kulala kitandani, Hakikisha unaamka saa kumi na moja kila siku, huruhusiwi kushiriki kingono na mwanamke tofauti na mkeo, huruhusiwi kuwa na watoto na mengineyo mengi. Ukiyachunguza Masharti haya kwa umakini utagundua yote yanalenga katika kumfanya muhitaji kuwa na nidhamu ya pesa (Financial discipline) pamoja na hardworking spirit (Kufanya kazi kwa bidii).
Kwa kumzuia mtu kulala kitandani no dhahiri kuwa mtu huyo atakuwa akiamka mapema kutokana na uchovu wa kulala chini na hivyo kumfanya aanze kazi mapema. Sharti lingine ambalo ni kumtaka mtu aamke mapema, saa kumi au saa kumi na moja, pia linalenga kumfanya mtu husika kuanza biashara au kazi zake mapema. Pia hutoa sharti la kumzuia muhusika kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke tofauti na mkewe. Sharti hili humafanya muhusika kujiupusha na moja ya sababu kubwa zinazowafanya wanaume wengi kutokufanikiwa ambayo ni "wanawake".
3. Uwezekano wa kufanikiwa kiuchumi hutegemea uwezo wa kufuata masharti
Mwisho
Andiko hili limejikita katika tafakuri binafsi ya mwandishi. Naweza kuthibitisha hili kwa kukuuliza swali lifuatalo:
Kwanini watu husingizia kuwa kila aliyefanikiwa ni mshirikina ilihali wao pia wanataka kufanikiwa kwa gharama zozote lakini hawajafanikiwa?

Hili ni dhahiri kuwa si mganga anayemfanya mtu husika kuwa tajiri bali ni uwezo wa mtu huyo kuzingatia masharti aliyopewa ambayo huwa ni nidhamu ya fedha na kujituma katika kazi.Mwisho

Upvote
1