Jinsi ATI walivyotaka kuwadhoofisha wamililiki wa Hospital Binafsi

Jinsi ATI walivyotaka kuwadhoofisha wamililiki wa Hospital Binafsi

MwanaAfya

Member
Joined
Jan 17, 2019
Posts
6
Reaction score
1
ATI ni Association of Tanzania Insurers.

ATI waliweka tangazo kwenye magazeti mbalimbali wakitaka wamiliki wa hospital binafsi wawe wanachama wao ili waweze kufanya kazi na mashirika ya bima ya afya bila hivyo watakosa fursa Hiyo.

Sasa najiuliza si makubaliano ya kufanya kazi na bima husika yanakuwa ni ya hospital na bima husika? ATI wanaingiaje hapo??

Mara ngapi tumesikia Hospital binafsi wakiwadai bima hizo mamilioni ya fedha kwa mda mrefu na mpaka wengine wanasitisha huduma kwa baadhi ya bima?? Ebu ATI acheni mchezo huo.

Ninaona kama tangazo lenu lina nia ya kudhoofisha shughuli za afya za sekta binafsi.

Tunaomba pia TIRA waingilie hili maana kuna mchezo hapa unafanyika.

Ahsante.
IMG-20190110-WA0025.jpeg
IMG-20190122-WA0001.jpeg


Fedha ni Pesa
 
Back
Top Bottom