EPISODE 40
THIS EPISODE IS SPECIAL FOR IRYN.
CONTINUE…..
Mama Janeth muda huu hata hakuwa na pingamizi kwa jinsi Iryn alivyokuwa na furaha ya kuniona asingeweza kumzuia wala kumkataza. Na muda huu Mama Janeth alionekana kuwa na furaha sana na mimi nilitumia nafasi hii kumsalimia na alinambia kwa taratibu“You have to takecare of her.”
Tuliongozana na Iryn mpaka tulikokuwa tumepark gari na tukaanza safari ya kuondoka pale Airport. Wakati tuko kwenye gari Iryn alikuwa ananiangalia sana na alikuwa na uso wenye furaha sana. Na mimi sikutaka kumwuliza jambo lolote muda huu,
MIMI: “How was your flight.”
IRYN: “Thanks God nimefika salama.”
MIMI: “Umetua na ndege gani?”
IRYN: “Qatar Airways japo tulichelewa ku-land.”
MIMI: “Haina shida cha muhimu umefika salama tu.”
IRYN: “Insider unanipeleka wapi? Naskia njaa.”
MIMI: “Nafikiri twende Mliman city ili tuongee pia.” Na muda huu nilikuwa serious kidogo.
IRYN: “Sawa haina shida.”
Baada ya kuwasili pale Mlimani city na kupark gari tulikwenda moja kwa moja mpaka instanbul restaurant ndo sehemu ambayo naonaga imetulia sana na inafaa kwa mazungumzo.
Baada ya kufika pale tulichagua sehem nzuri ya mwishoni kabisa na tukakaa na muda huu mhudumu alikuwa amefika kutusikiliza, tuli odda chakula na Iryn alikuw akiniangalia sana kama mtu anayetaka kusema jambo ila kama anasita.
MIMI: “Mbona kama una wasiwasi upo sawa kweli?”
IRYN: “Insider I’m really sorry for what all happened.”
MIMI: “Nakusikiliza kwa makini sana unambie kwanini uliamua kuondoa bila kuniaga hapo ndo nitaangalia nikusamehe au laah. Hivi unajua ni jinsi gani uliniweka kwenye wakati mgumu sana? Ilibaki kidogo sana kwenda Police kutoa taarifa hivi unafikiri mimi ningekua kwenye wakati gani?”
IRYN: “I know Insider, I am really sorry sikuu……”na muda huu Iryn alianza kutoa machozi.
Nilijisikia vibaya sana muda huu kuona akilia na ilibidi nitoe leso yangu nikaanza kumfuta machozi. Niliingiwa na huruma sana ikabidi nianze kumbembeleza nilihisi huenda Iryn alikuwa kwenye wakati mgumu sana huko alikokuwa.
MIMI: “Mummy I’m sorry na niko hapa kwaajili yako be free kunambia kilichotokea, no matter what tuko pamoja ndomana nilikuja kukupokea Airport.”
IRYN: “Insider I’m really sorry naomba utambue sikufanya makusudi kuondoka bila kukuaga ila ile siku nilipewa habari mbaya sana na Mama Janeth. Ni habari ambazo zilinikosesha raha nilijikuta na hatia sana ile siku.”
MIMI: “Kwanini unasema hivo? Ni habari gani mama Janeth alikupa?”
IRYN: “Ile siku nilikuwa chumbani nimelala nikapigiwa simu na Mama Janeth Kuwa Baba yangu amelazwa yuko hali mbaya na anahitaji kuniona haraka wakati ule. Insider unajua licha ya kuwa na uhasama na Baba yangu lakini nilikuwa bado nampenda sana.
Mama Janeth aliniambia nijiandae haraka tuondoke kwani kuna ndege imepatikana na itaondoka saa 00:30 usiku. Ilibidi niamke nianze kujiandaa haraka na kupanga nguo baadhi ya kuondoka nazo na wakati najiandaa nilipigiwa simu kuwa gari iko nje tayari inanisubiri ili tuondoke. Insider niliondoka kwa haraka sana muda huu na wakati tumeshaondoka nilikuja kugundua nimesahau simu na sikuwa na jinsi tena.
Baada ya kufika Airport nilikutana na Mama Janeth akasema ananisindikiza mpaka South Africa afu yeye atakwenda USA ana kikao cha mwaka kule. Tulifika South Africa alfajiri na tukaenda moja kwa moja mpaka Hospital aliyokuwa Baba amelazwa Cape town. Insider nilimkuta Baba akiwa hali mbaya sana alikuwa anapumulia mashine tu alikuwa ICU. Nililia sana maana nilijua nakwenda kumpoteza baba na nina kuwa yatima.”
Na muda huu alianza kulia tena na dada alikuwa kashaleta chakula pale mezani. Na mimi niliendelea kumfuta machozi na kitambaa changu.
MIMI: “Aisee pole sana mummy ukilia hivi unaniumiza na mimi.”
IRYN: “Ahsante, Insider unajua nilianza kusali sana muda ule na nilikaa pale nje namsubiri kwa bench. Nilisema siondoki mpaka niongee na Baba, saa4 asubuhi ndo tuliitwa tuingie tena ndani tukamwone. Nilimkuta Baba kidogo afadhali na alikuwa anaongea japo kwa shida, kitendo cha kuniona ni kama nilirudisha furaha yake kwake na nilimsogelea tukaanza kulia wote pale.
Tuliondoka pale na mdogo wangu ambaye ndo mtoto wa kwanza wa mzee kwa upande wa mamdogo mpaka home na mama Janeth aliniaga anaondoka kwenda USA. Insider nilikuwa nashinda nasali tu maana mzee angekufa sidhani kama Mungu akangenisamehe maana nilikuwa na kinyongo na Baba, na toka msiba wa mama sikuwai kaa naye chini japo alikuwa akinisisitiza sana tuzungumze.”
MIMI: “Kweli kabisa Mungu asingusamehe maana sisi sote ni watenda dhambi hakuna mkamilifu.”
IRYN: “You’re right, Jumapili Baba alikuwa yuko vizuri kiafya na aliruhusiwa kwenda nyumbani, Insider baba yangu anasumbuliwa na kansa hivyo anahesabu siku za kuishi tu hapa duniani.”
MIMI: “Very sad najisikia vibaya sana kwakweli lakini nashukuru Mungu Mzee bado mzima tuendelee kumwombea.”
IRYN: “Nashukuru Mungu tumeyamaliza na Baba na nimetambua baba hakuwa na kosa alikuwa sahihi kuoa mke mdogo.”
MIMI: “Kwanini unasema sahihi wakati alisababisha kifo cha mama yako?”
IRYN: “Insider Baba alioa mke mdogo kwa siri sababu mama yangu hakuwa na uwezo wa kuzaa tena baada ya kunizaa mimi. Kwahiyo mimi ndo mtoto pekee niliyebahatika kuzaliwa kwa mama. Baba anasema kama Mwanaume asingeweza kuwa na mtoto mmoja hivyo ilimlazimu kufanya hivyo ili awe na watoto wa kuendeleza ukoo. Niliona baba alikuwa sahihi kufanya vile, mwenyewe niliwaza hakuna Mwanaume kwasasa ambaye yuko tayari kuwa na mtoto mmoja, Insider wewe ungeweza?”
MIMI: “Hapana kwakweli baba alikuwa sahihi maana wewe ukiolewa unakuwa upande wa mwanaume.”
IRYN: “Huo ndo ukweli, Insider baba anataka mimi kuwa msimamizi wa mali na kampuni zake zote zitakuwa chini yangu, maana mimi ndo binti yake pekee ambaye nina jitambua na Mzee ameona mimi nitafaa kuwa msimamizi.”
MIMI: “Kwani watoto wa mamdogo wana umri gani?”
IRYN: “Wa kwanza ni wa kike ataanza bachelor mwakahuu na wengine wawili ni wa kiume bado wadogo.”
MIMI: “Ulinambiaga mzee ana mtoto wa nje mkubwa vipi?”
IRYN: “Yule ameshaharibika Insider anatumia heroin afu ni mtoto wa nje, baba anampango wa kumsaidia kivingine. Kama pesa za mitaji kapewa lakini hakuna alichofanya cha maana mpaka sasa.”
MIMI: “Aisee! Huyo mamdogo wako amekubaliana na mawazo ya mzee hajaonesha sign yoyote mbaya?”
IRYN: “No she is very happy na amefurahi sana mimi kuyajenga na Baba, kampuni zote zitakuwa za familia but under my watch. Na ninavyoongea na wewe hapa Baba amenikabidhi documents zote muhimu za kampuni na password za account za kampuni.”
MIMI: “Aisee hongera sana huku mama kule Baba na kote unahitajika itabidi ufocus now.”
IRYN: “No way na October nitarudi South Africa kusoma Masters, naenda kule ili niwe karibu na baba na pia ndo nitakabidhiwa rasmi madaraka na Baba.”
MIMI: “Utaweza kumanage South Africa na huku?”
IRYN: “Insider unasahau kama nina bachelor ya Business Administration? kitu kidogo hiko kinishinde?, kuna mpango nauandaa nitakushirikisha.”
MIMI: “Kwahaya yote mimi nimekusamehe pole sana kwa yote.”
IRYN: “Insider nilikuwa kwenye wakati mgumu sana hata kukumbuka kuna Insider naanzaje wakati baba ana hali mbaya?. Hivi unajua namba yako nimeipataje? Ile Jumapili ambayo tumerudi na Baba kutoka hospital nilianza kukumbuka wewe, maana nilijua utakuwa unanitafuta sana. Japo sikufikiria kama ungewaza kwenda Police.”
MIMI: “Tulianza kuogopa maana kuna mlinzi wa Jiran alisema aliiona Noah nyeusi imepark getini nje na ilitoka kwa spidi sana. Sisi mawazo yetu umetekwa maana baada ya kufungua mlango tuliona simu kitandani na imezimwa na baada ya mlinzi kusema hayo tulipagawa sana.”
IRYN: “Maskini poleni sana simu ilikuwa haina chaji afu ile iliyonifuata ni Mercedes Van nyeusi ina muundo kama wa Noah tu, ila kwa mbali mtu angesema ni Noah.”
MIMI: “Si unajua wabongo? So uliipataje namba yangu?”
IRYN: “Dada yule Agent ulikochukua mizigo ndo alonisaidia kupata namba yako. Baada ya kumtafuta Mama Janeth hakuwa online na nikapata wazo la kumtafuta yule dada Agent mpya. Nilikuwa na history ya kuchat nae kupitia email na nilijua lazima tu angekuwa na namba zako. Baada ya kumtext huwezi amini alirespond within 30mins na akanitumia namba yako unajua sikuaamini Insider.”
MIMI: “Daah ulitumia akili sana, unajua nilikwenda mpaka ofisini kwa Mama Janeth na niliambiwa hayupo? Lakini niliwapa details zangu wamtumie mama incase akizipata anirudie lakini mpaka leo kimya.”
IRYN: “Pole sana Insider mama Janeth alikuwa busy sana maana baada ya kwenda US ilibidi aende Ukraine si unajua masuala ya Social Protection? Kuna Research walikuwa wanafanya kule.”
MIMI: “Ina maana hata ujumbe wangu hakuupata?”
IRYN: “Aliupata, Jumatatu alinitafuta akanambia amepata ujumbe wako kuwa umtafute, so yeye alinitafuta mimi ndo nikamwambia niliondoka bila kukuaga ila nimesha kucheki tayari. Insider kitendo cha kwenda mpaka ofisini kwake Mama Janeth amekuelewa na kukubali sana, amenambia wewe ndo rafiki mwema, thank you so much for everything.”
MIMI: “Wewe kama mtu wangu wa karibu ilibidi nifanye vile. Na imekuwaje tena mmerudi wote?”
IRYN: “Aliomba nimsubiri aje amwone Mzee afu turudi wote Dar es Salaam, pia tulikuwa na mazungumzo ya pamoja.”
MIMI: “Sawa anakujali sana, tuondoke zetu nikupeleke mapema ukapumzike utakuwa umechoka sana.”
IRYN: “Insider mimi siendi kwangu nataka twende kwako na hii week nitalala kwenu sawa?”
MIMI: “Sawa karibu pale ni home tu hata usiwe na wasiwasi.”
Nilifanya malipo na tukaondoka pale Mlimani city kurudi home na njiani story zilikuwa zimekolea sana.
MIMI: “Hivi unajua una kesi za kujibu kwa Mama Junior?”
IRYN: “Kesi gani hiyo?”
MIMI: “Si aliziona zile picha za kule Zanzibar ujue.”
IRYN: “Insider umezidi sana uzembe picha kama zile ulishindwaje kuzihide au kuzifuta? Au hujui jinsi ya kuhide picha nikufundishe?. Huo ni uzembe mkubwa sana unaweza kuwa serious kwenye vitu vikubwa ukapuuzia vidogo na ndo vikakufelisha. Hivi unanitengenezea mazingira gani kwa Mama Junior? hata kama hatuna mahusiano kwa Mke hawezi kukuelewa even to me siwezi kukuelewa kabisa.”
MIMI: “Kweli nilizingua sana kwa hili, ujue toka tumetoka Zanzibar sikukaa chini nikatulia na suala lako lilinipa sana stress. Na aliziona baada ya kumpa simu Junior aangalie Cartoon ndo alipata chance ya kukagua.”
IRYN: “Insider unajua Mama J wako ana wivu sana na wewe, na pia anakupenda, inatakiwa hili ulitambue. Ilinde simu yako kama uhai wako wewe ni Mwanaume unawasiliana na watu tofauti usipokuwa makini itakucost siku kama nilivyokwambia awali.”
MIMI: “Uko sahihi this time nitakuwa makini sana, ila alielewa mpaka leo hajawai kuulizia tena.”
IRYN: “Uzuri nilimwambia kwamba tuko wote Zanzibar hili nalo limesaidia, nisingemwambia na akaona hizo picha ingekuwaje?. Mama Junior nilishamsoma mapema sana na nitaendelea kumweka sawa taratibu.”
MIMI: “Sawa bhana ngoja nione reaction yake akikuona.”
Tuliwasili pale home nikatoa mabag yake na nikamkaribisha ndani na muda huu dada alikuwa katoka nje kunipokea.
“Dada peleka haya mabag chumbani kwako.”
Tulikaa pale seblen na Iryn alikuwa busy sana na Junior maana alionekana kum-miss sana. Na muda huu aliomba bag lake kubwa aletewe na baada ya dada kulileta alilifungua bag na lilikuwa limejaa mazawadi tu.
Kwa upande wangu alikuwa ameniletea zawadi za viatu, nguo, saa na laptop ya Macbook Air mpya kabisa.
IRYN: “Insider hii Laptop itakusaidia kuandaa kazi zako na report za kampuni.”
MIMI: “Thank you Mummy.”
Ukweli sikutegemea kama Iryn angeniletea zawadi ya Macbook na niliifurahia sana hii zawadi. Kwa upande wa Junior alikuwa kamletea Ipad ya kuchezea, nguo za kutosha na viatu.
IRYN: “Hizi za Mama Junior wewe hazikuhusu ataangalia mwenyewe badae, dada rudisha bag ndani. Dada wewe nimekusahau sorry nitakupa hela ukafanye shopping.”
DADA: “Ahsante Dada.” Dada Junior alionesha kufurahia baada ya kusikia atapewa hela akafanye shopping.
IRYN: “Insider mimi si nipo hapahapa kesho tutakwenda naye Sinza au unaonaje?”
MIMI: “Sawa haina shida itapendeza zaidi.”
IRYN: “Vipi kuhusu maendeleo ya ofisi?”
MIMI: “Salama kabisa nikiwa na Lucy na Sumaiya mambo yanakwenda vizuri kabisa.”
IRYN: “Kesho tutakwenda wote kuangalia maendeleo.”
MIMI: “Sawa haina shida mummy.”
Tulikaa pale tukiendelea na mazungumzo yetu na jioni Mama Junior alirudi kutoka chuo na baada ya kuingia ndani na kumwona Iryn alikwenda mbio na wakakumbatiana.
TO BE CONTINUED
“Sorround yourself with People that love you for you and love them back. Because love is the one thing in this world that’s worth fighting for.”
Week hii sitakuwepo tukutane Jumapili [emoji120]