EPISODE 13
TUNAENDELEA………….
Jumapili niliamka mapema sana nikaenda Sokoni nikanunua Jogoo mkubwa wa kienyeji aliyenona vizuri, nikanunua stake ya nyama 2kg, nikanunua maini 2kg, nikanunua matunda, nikanunua mayai ya kienyeji tray 1, nikanunua na mchele safi ule OG wa kyela 5kg, nikaelekea kwa Iryn.
Nilifika pale saa 2 asubuhi na Iryn alikua kaamka anafanya usafi wa ndani. Nikatoa vitu kwenye gari nikaingiza jikoni, alifurahi sana hii siku kama nilimsaprize na alinishukuru sana pale.
Baada ya kupata chai ile asubuhi tukaondoka kwenda kufanya shopping ya vitu. Tulikwenda moja kwa moja Mlimani city na tukaenda Shoppers.
Tulifanya shopping na hii siku alinunua vitu vingi sana vya jikoni, alinunua vyombo, na mazaga mengine mengi. Tulitoka hapo tukaingia duka la michezo akanunua vifaa vya michezo kama track, kamba za kuruka na vitu vingine vingi.
Baada ya kumaliza shopping tukaanza kurudi home. Tulirudi home na muda huo tukaingia jikoni. Nilimsaidia kumkata kata kata yule kuku vipande, na yeye alikua akiandaa vitu vingine.
Mimi kuhusu mambo ya jikoni niko vizuri sana, sasa nilikua namsaidia kazi nyingi sana mle jikoni huku tunapiga story.
IRYN: “Insider haya mambo umeyajulia wapi wewe?”
MIMI : “Mama yangu alikua ananifundisha toka nikiwa mdogo na pia nilikua najifunza mwenyewe ukubwani.”
IRYN : “Upo vizuri natamani nipate mwanaume kama wewe, mke wako atakuja kupata raha sana.”
MIMI : “Hata wewe pia naona uko vizuri sana, nilikua nakuchukulia poa ila umekamilika kuanzia uzuri, pesa, mpaka jikoni.”
IRYN : “Nataka leo nikupikie Pilau ambalo hujawai kula.”
MIMI: “Heshima yangu kwako leo imefika Nyota 5.”
IRYN: “Insider mimi sio kama wale mnaowaita slay queens tuheshimiane”
Muda huu nilikua nakataka vitunguu, nyanya, karoti na hoho, Iryn alikua ananiangalia sana huku anatabasamu. Ni kama alikua haamini macho yake mwanaume anayefanya yale mautundu ndo mimi Insider. The way tulivyokua kule jikoni akija mtu angesema sisi ni wapenzi hata Mama J angeona asinge weza nisamehe.
Muda ule tulisikia mtu akigonga mlango, Iryn alikwenda na baada ya dakika 3 alikua karudi na cake. Ni jiran ambaye alikua amezileta na zilikua tamu sana zile cake.
MIMI : “So Iryn hapa toka uhamie una muda gani?”
IRYN: “Hapa nimeamia mwaka jana mwezi june”
MIMI: “Na ulikuja lini Tanzania?”
IRYN: “Toka utokee msiba wa mama sikuwai kupanga kurudi Tanzania tena, kwa sasa ningekua zangu Ufaransa. Nimerudi Dar es salaam April mwaka jana.”
MIMI : “Chanzo cha kurudi?”
IRYN : “Insider Mama kabla ya kifo chake alinisisitiza sana nizisimamie biashara zake. Pia alinipa Diary ambayo inasiri nyingi sana, pia niligundua mama alikua ana nyumba 2 hapa Dsm alizoziacha. Pia nafatilia mafao ya mama aliyoacha kule kazini kwake, maana mama aliniandika mimi kama mrithi wake so ni pesa nyingi sana Insider. Sitaki kumuudhi mama yangu huko aliko nataka nivienzi na kuviendeleza alivyoviacha.”
Hapo ndo nikajua kumbe Iryn mama yake alimwachia urithi binti yake, pia baada ya kifo chake Iryn aliingiziwa kama 150million za rambirambi na michango kutoka kwa wafanyakazi wa Mama yake, vikundi mbalimbali na Organization. Pia mazishi ya mama yake yaligharamiwa na Organization.
MIMI : “So umeweza kuzijua mali zote alizoacha mama?”
IRYN : “Yeah pia Mama alikua na kampuni ya usafi ambayo anashirikiana na rafiki yake (Mama Janeth). Hii natakiwa kuchange Director name niweke Jina langu lakini nitaacha Mama Janeth aendelee kuisimamia mimi nitakua nakwenda kwenye vikao muhimu. Pia kule Masaki kuna Saloon nyingine ambayo nayo wanashirikina na Mama Janeth sijataka kuziingilia kabisa, as long as I get my profits no problem naona Mama Janeth aendelee kuzisimamia. Mama Janeth, pia ndo kama Mama mlezi wangu kwa sasa.”
MIMI: “Kama Mama Janeth unaona ataweza zisimamia acha aendelee wewe simamia hizi ambazo mama alikua anatumia kampuni yake binafsi.”
IRYN : “Insider hata hivyo mama alikua ananipenda sana, nilikuja kujua alikua anaweka akiba ya 30% kila mwezi kwa ajili yangu. Mama kama aliona future yake.”
MIMI : “Mama kweli alikupenda, alikutengenezea njia. You have to make her proud Iryn”
IRYN : “I promise”
MIMI: “But nina ushauri, ulisema Baba anakutafuta muongee kwanini usimpe nafasi Baba yako?. Msikilize ujue anataka kukuambia nini, pia kumbuka Baba ndo only hope you have now. Naamini Baba yako anakupenda sana, na kitendo cha kutowasiliana naye atakua anajiskia vibaya sana.”
Muda huo mimi nikamsogelea yeye alikua amekaa kwenye kiti nikazunguka nyuma yake nika mshika mabega yake kama vile nayasugua.
“Iryn mtafute Baba msikilize anataka kusema nini, najua alimkosea sana mama yako mpaka kumsababishia kifo, lakini naamini alimwomba msamaha mama yako. Sisi binadamu hakuna aliyemkamilifu mbele za Mungu sote ni wakoseaji, naamini huko Mama yako aliko atakua anatamani muyamalize na Baba yako. Huu ndo ushauri wangu kwako Iryn.”
Nilivyoona amekaa kwenye kiti haongei kitu nikawaza nitakua nimemkwaza, maana Iryn mkiongelea story za mama yake alikua anabadilika sana.
“Huu ulikua ni ushauri wangu kwako kama nimekukwaza naomba nisamehe Iryn”
Muda huo nilikua nimemwacha nimeanza kwenda seblen
“Insider………”
Bhasi Iryn akasimama akaja spidi akani-hug akawa analia. Ofcoz na mimi upande wangu nilianza kujiskia vibaya sana.
“Insider nashukuru sana kwayote unajua toka nimekutana na wewe naona lifestyle ya maisha yangu inabadilika tararibu. Wewe ndo mtu pekee ambaye tunakaa tunaongea masuala ya maisha na mambo mengine mengi. Wewe ndo mtu pekee ambaye tunakua wote kwa muda mwingi, wewe ni moja ya rafiki zangu muhimu sana. Nimetokea kukuamini sana kwa muda mfupi sikutegemea kuna siku ningekua na mtu wa karibu hapa Dsm kama wewe.”
Bhasi nikamwangalia nikamfuta machozi na vidole vyangu nikaenda seblen.
Ile nimefika sebleni kucheki simu nakuta missed calls (3) za Prisca alikua pia kanitumia na message juu. Ikabidi nisome ile message na ilikua inasema:
“Insider mbona hupokei simu zangu? Toka jana tumeachana hata kunijulia hali hakuna. Unajua mimi naumwa, nataka unipeleke hospital.”
Nilikua pale kwenye coach nikajisemea kwa hii spidi ya Prisca nikimfanya mchepuko wangu atanisumbua akili sana na atakuja kuniletea matatizo kwa Mama J. Palepale nikamwandikia:
“Am sorry. Jana wakati tumeachana nilikwenda kwa mamdogo nikarudi night sana, nimemka sio muda mrefu sana na niko huku Bunju bado. Sitoweza kukupeleka Hospital kama nitawai kurudi nitakuja kukuona.”
Ofcourse ile show nilompelekea tena ya kibabe na hasira, nilijua kwa mtoto laini kama yule ambaye hajaizoea mikiki lazima angepata homa tu.
Muda ule niko seblen, Iryn alikua ameshaanza kuandaa chakula mezani na mimi nikatoka kwenda kumsaidia kukata matunda.
Hii ndo siku ya kwanza naonja mapishi ya Iryn kiukweli lile pilau lilikua ni tamu sana, pilau lilikua na mixer ya maini afu kuku walikua wa kuroast. Kile chakula kilikua kitamu sana, kweli nikaamini Iryn hata kwenye mapishi yuko vizuri sana. Na muda huo nakula alikua ananiangalia kama mtu ambaye akisubiri nitoe neno.
MIMI: “Mama upo vizuri sana nilikuachukulia poa ila nimekunyooshea mikono.”
IRYN : “Si ulikua unanidharau?, mimi sijaamua tu kuingia jikoni.”
MIMI: “Ulijifunzia wapi haya mapishi maana hili pilaua ni tamu sana.”
IRYN: “Nimejifunzia chuo mapishi mengi sana hasa ya Ufaransa kama hili pilau nimelipika kifaransa. Wakati niko chuo nilijiunga na CLUB za Catering, Dancing na Gardening. Na nilipata Certificates kwenye CLUB zote pale chuoni.
MIMI : “So hizo CLUBS ni kama short course au?”
IRYN : “No tuseme ni kama Extracurricular activities. Pale chuoni kulikua na CLUBS nyingi sana wewe unaamua ujiunge na zipi na ilikua hutakiwi kujiunga zaidi ya 5. Na zote mnaingia darasani mnafundishwa na mnafanya practical, mfano kama mapishi najua kupika mapishi mengi sana na yote nilifaulu. Najua kupika mapishi mengi ya Europe, pia upande wa Gardening tumefundishwa jinsi ya kuandaa garden, kupamba maua na kumbi za sherehe. Hapa Tanzania sijaona garden ilopambwa vizuri labda kwa Masaki na Oysterbay kidogo atlist. Kuna mbinu za kutengeneza Garden Insider, na plan mbeleni huko kuanzisha kampuni yangu ya upambaji na utengenezaji wa Garden naamini nitapata sana hela.”
Muda huo akawa ananionesha picha za Garden walizokuwa wanatengeneza chuo na zile za Mapishi.
MIMI: “Vipi kuhusu Dancing”
IRYN : “Dancing tumejifunza dancing nyingi sana especially za Europe mfano minuet, Tarantella, Ballet, waltz dance nknk “. Na hizi Dance zinatumika sehemu tofauti kulingana na mazingira. Na ninajua dance zaidi ya 20.”
MIMI: “Mwalimu naye anakua anajua kucheza kabisa?”
IRYN : “Ndio mwalimu lazima ajue kucheza na pia kuna clip videos ambazo tunakua tunaangalia class. Yaani kama kukata mauno unafundishwa stage kwa stage, tofauti ya mauno ya Africa na Europe ni kwamba wadada wa Europe mauno yao ni ya mapozi yale ya taratibu ila Waafrica anazungusha kama pia. Wazungu wanasema ni uchafu na fujo, kiuno kinatakiwa kuzungushwa taratibu huku unashuka chini kwa mapozi huku umelegeza macho.”
MIMI : “Aah aisee ni noma, wazungu wameendelea sana haya mambo Bongo vyuoni hakuna kabisa.”
IRYN : “Wenzetu vyuo vyao vinakufundisha na ujasiriamali kama hapo ukimaliza chuo unaweza kwenda kuajiriwa hata na Restaurant au Garden yoyote ile na ukapata hela. Tanzania hawatoi elimu za ujasiriamali kwa vitendo.”
MIMI: “Tanzania bado tunasafari ndefu sana.”
IRYN : “Mimi nimesoma International Business Administration lakini tumefundishwa jinsi ya kubehave as Managing Director, tunafundishwa jinsi ya kudress, jinsi ya kuongea na customers au wafanyakazi na viongozi wa nchi nknk. Na tulikua tunafanya practical, ukizingua course una carry. Unafundishwa pia jinsi ya kuwa confident unavyokuwa kwenye vikao, vyombo vya habari na jinsi ya kutuma mails na kuongea kwenye simu. Insider kama unataka mtoto wako apate elimu bora mpeleke akasome nje.
Tuliongea mambo mengi na hapo nikajua kumbe Iryn ana Bachelor ya International Business Administration, zaidi ya hapo pia ana ujuzi mbalimbali.
Baada ya kumaliza kula nilimshukuru kwa chakula na mimi nikatoa vyombo mezani na kupeleka jikonii na palepale nikaanza kuviosha.
Iryn aliniaga anakwenda kulala na mimi muda huo nikasema nimpigie simu mama J. Nilipiga simu lakini hakupokea, nikasema acha nimwache mwanamke ukimlazimisha atakusumbua acha atanitafuta mwenyewe.
Mzee pia alinipigia simu kupitia “Whatsapp call” na tuliongea sana, moja ya maongezi yaliyonifurahisha ni pamoja na Mzee kunambia ameshachora ramani ya nyumba. Baada ya mazungumzo haikuchukua sekunde akanitumia ile ramani. Niliipenda ile ramani sababu mzee alikua ameidizaini vizuri sana, licha ya kujenga hizo nyumba 2 za vyumba viwili bado kuna eneo kwa juu ningeweza kujenga chumba na sebule hapo baadae. Pia kulikua na sehem ya kujenga tank la maji na parking ilikua kubwa.
Nililala pale kwenye coach, Iryn ndo aliyekuja niamsha na muda huo ilikua tayari saa 1 kasoro usiku. Hii siku Iryn alipanga nimpeleke Kidimbwi akasafishe macho na alitamani sana kufika eneo hili.
IRYN : “Insider amka kajiandae bhasi”
MIMI : “Wewe uko tayari?”
IRYN : “Bado kuvaa tu.”
Kama mnavyojua wanaume hatunaga mambo mengi, nilikwenda kwenye gari nikatoa kibag changu, nikatoa pamba zangu. Ndani ya muda mfupi nilikua niko tayari nikimsubiri yeye.
Haikuchukua muda na yeye akawa ametoka tukaondoka kuelekea Kidimbwi. Tulifika pale kwenye saa2 na tulipark gari sio mbali sana na geti la kuingilia ndani. Palepale Masai sijui alitokea wapi akaja kugonga upande wangu.
MASAI: “Bossy usipark gari hapa, kuna mtu anakuja kupark”
Iryn akadakia maongezi yetu…
IRYN: “Masai huyo mtu yukowapi? Mbona simwoni”
MASAI : “Amenipigia simu anakuja nimwekee parking.”
IRYN : “Bhasi utamtafutia eneo lingine sisi tunapark hapa. Na anakulipa sh. ngapi?”
MASAI : “Ananilipaga 3,000”
IRYN : “Ok mimi nitakupa 10,000, pia naomba uilinde hii gari, sawa?”
Muda huu tulikua tumeshashuka sasa mimi nina lock mlango wa gari.
MASAI : “Sawa haina shida Bossy”
Masai akanambia bro una demu mzuri sana wewe ni noma, dizaini kama Iryn alisikia yale maneno ya Masai, japo masai alikua akiongea kwa sauti ya chini. Nlimpiga jicho Iryn aliishia kutabasam na kutingisha kichwa cha kusikitika.
Tulivyoingia ndani ya eneo la tukio walionekana watu wakiwa wamekaa kaunta, wengine kwenye viukuta, wengine wakitoka na kuingia, kwa mbele kaunta zilionekana screen watu wakiangali mpira, mambo ya EPL.
Wakati tunasogea kuna dada akawa ameshakuja kutuwahi
“Karibuni guys mmependeza sana”
IRYN : “Thank you. Nataka tukae sehem ambayo imetulia lakini ina vibe”
“Sehemu nyingi zimechukuliwa na zingine ziko reserved.”
MIMI : “Dada najua huwez kosa sehemu ya kutuweka, wewe fanya mambo tutakufurahisha sana.”
“Sawa nisubirini hapa nikawaandalie sehem nakuja kuwachukua”
Muda huo Iryn macho yote yalikua yakiitizama hili eneo kwa umakini sana. Kwa upande mwingine tulikua tukipigwa sana macho na watu mbalimbali. Na sisi tulikua tumekaa kwenye kiukuta pembeni ya kaunta.
IRYN : “I love this place, watu kuwa wengi hivi kutanifanya nisiipende.”
MIMI: “Wewe ni certified ANTISOCIAL siwezi kukushangaa”
Akanipiga na kibao cha pajani
Na muda huo dada alikua kafika kutuchukua na kutupeleka kwenye meza yetu. Ilikua ni meza ya duara iliyounganishwa na mlingoti na viti virefu vya kukaa, na pale kulikua na viti vinne vya mzunguko.
“Mtakaa hapa kuna wengine watakuja watakaa na nyinyi kwa upande huu”
IRYN: “Hapa nimepapenda pia pako karibu na DJ nitavibe. Insider ulishawai kutumia Moet?”
MIMI : “Hapana but naskia ni sweet”
Muda huu dada waiter alikua akitabasamu sana..
IRYN : “Ni kama champagne ila ni nzuri sana. Dada naomba tuletee ile Moet Imperial Rose.”
MIMI : “Usisahau maji ya kunywa chupa kubwa na pia usilete Moet na yale mataa yenu, hatuko kuuza sura hapa.”
“Sawa haina shida msijali”
Hivi viwanja vikubwa ukinunua vinywaji vya gharama huwa vinaletwa na watu special wameshika mataa yao, sikuhizi wanaandika na jina la mnunuaji.
Baada ya muda mfupi dada alikua kaleta vinywaji na tukaanza kupeleka taratibu maana ilikua mapema sana na eneo halikua na watu kihivyoo. Muda ule tuliendelea na story taratibu
IRYN : “Insider Kuna jambo inatakiwa ulifahamu”
MIMI : “Jambo gani hilo?”
IRYN: “Ipo hivi kuna jambo sikukwambia Insider nataka leo nikuweke wazi. Grizz mwakajana December alinipa pesa ndefu tu ninue gari, sasa mimi sikutaka kuikataa pesa yake. Mimi kama unavyoniona sina mpango wa kununua gari kwa sasa naona itaniletea shida tu, hata ningenunua ningeishia kuipark sina mpango na gari kwa sasa. Nilivyoona gari yako nzuri na inavutia ndo nikapata wazo niwe nakutumia kama my driver. Grizz anajua hilo gari ni yangu na anajua wewe ni dereva wangu nimekuajiri.”
MIMI: “Mimi sina shida kabisa Bossy wangu.”
IRYN : “Ile siku ambayo hatukwenda wote, Grizz aliniuliza nakulipaje mshahara nikamwambia kama tulivyokubaliana kwa mwezi 1,200,000/= (Tulikubaliana na Iryn kwa weekend ni 300,000). Na yeye aliuniuliza nimeshakulipa kiasi gani, nikawambia nimeshakulipa miez 2 tayari ambayo ni 2.4 million. Grizz akasema suala la mshahara wako litakua chini yake na akasema atanirudishia pesa niliyokuwa nimekulipa na atatoa pesa ya mwezi huu. Alivyonipa ile bahasha kuhesabu zile pesa zilikua ni Euro 1,500 lakini mimi sikutaka kutoa kiasi chochote pale niliamua kukupa.
MIMI : “Thank you lakini ulikua ushanilipa kwanini usingetoa? Ungeacha hata ya mwezi huu, mimi nilijua ni zawadi kutoka kwa Grizz.”
IRYN : “Insider natambua wewe pia unamajukumu sana japo bado hujaniweka wazi kuhusu maisha yako, lakini mimi nikikutizama naelewa. Hiyo pesa kwangu sio ya kuni fanya nikakosa ubinadamu. Kwa muda ambao tumefanya kazi na wewe nimeingiza pesa nyingi sana, na pia huwa najiskia vibaya unavyonisubiri usiku hata kama ni kazi yako lakini umejitoa kwangu.
MIMI: “Niseme tu Ahsante sana kwa yote, niseme ukweli toka nikutane na wewe umekua ukinijali sana. Unanifanya niendelee kuvimba hapa mjini, naomba usinilipe mpaka thamani ya hii pesa itakapotimia.”
IRYN : “Insider sisi tushakua familia tayari, ni muda muafaka wa kuniweka wazi kuhusu maisha yako. Sijui historia yako, najua unaishi Mbezi lakini sikujui kwako, wewe unakuja kwangu mimi kwako sikujui what Kind of friendship do we have?”
Palepale nikawaza sijui nimwambie ukweli kama nina mke na mtoto. Nikaona kama mapema sana, lakini nikapata wazo siku nitamsaprizi nitamleta kwangu.
Na muda huo dada alikua amekuja kutuuliza kama tunahitaji chochote, bhasi tukaagiza portion 2 za mbuzi choma.
MIMI: “So Grizz alishaondoka?”
IRYN: “Alishaondoka,unajua Grizz anakukubali sana Insider.”
MIMI : “Kwanini unasema hivo?”
IRYN: “Ile siku ambayo tulikwenda kule Oysterbay na ukaanza kuchoma nyama na kujichanganya nao, bhasi Grizz anasema ni Waafrica wachache ambao wanajiamini kama wewe.”
MIMI: “Hahaaha unajua Iryn haya maisha sometimes ni kujitoa ufahamu tu, siku ile niliona hawajui kuchoma nyama ikabidi niwasaidie.”
IRYN : “Sasa Grizz hapo ndo alipokukubali na alisema next time akija tutafanya party ya kuchoma nyama tu.”
MIMI : “Mimi sina shida tena hio siku nitawaonesha mautundu yangu yote”
IRYN : “Unajua ile siku uliyolala home wakati tumetoka Samaki samaki tulikua tumelewa. Mimi hata sikuwa nimelewa I was just pretending. Hata tulivyofika home ukanipandisha kitandani nilikua na akili zangu zote, ukanivua koti nilikua nakuangalia tu. Baada ya kutoka pale ulirudi seblen baada ya dk15 mimi nilitoka kukuangalia nikaona umelala na mimi nikarudi kulala. Nilikufanyia makusudi ili nijue wewe ni Mwanaume wa aina gani na toka siku ile unaona ukaribu wangu kwako umeongezeka.
MIMI: “Aisee yaani kumbe yale yote nililokuwa nafanya ulikua unaoana.”
IRYN: “Yes, nilitaka kujua wewe ni Mwanaume wa aina gani ila nikajua wewe ni More than Gentleman. Insider Kitendo cha kunywa pombe na kutokunifanya chochote nili realize wewe sio mtu mwenye tamaa na ni wanaume wachache sana wenye tabia kama yako.
MIMI : “Hata ile siku ungenitaka kimapenzi nisingekukubalia kabisa”. (Nilimjibu hivo kuonesha uzuri alionao hauni babaishi)
IRYN : “I’m proud of you. Jumanne tutakwenda kwa Mama Janeth Masaki kuna mambo natakiwa kuongea naye.”
MIMI : “Sawa haina shida utanambia tu muda wa kwenda.”
Hapa ndo nikajua kumbe nilikua nimewekewa mtego kama ningekua natabia za kifisi kama wale wazee wa kula Kimasihara bhasi kibarua kingeota nyasi.
IRYN : “Insider I need your company nataka kwenda washroom, huko njian nitasumbuliwa sana.”
Na mimi hata sikutaka kumgomea na pale kwenye table alikuwepo jamaa na dem wake tukaomba watuangalizie. Na muda huo watu walikua wengi sana ilikua saa4 tayari na watu walizidi kumiminika pale.
Nilimpeleka Iryn mpaka washroom na mimi nikazama upande wa “Gents” kupunguza mafuta. Nilitoka nikawa namsubiri kwa pale nje, na baada ya dakika kadhaa akawa ametoka. Sasa ile tunarudi macho ya mafisi yalikua yakimwangalia sana Iryn na macho ya madem yalikua kwangu.
Tulirudi kwenye meza yetu kuendelea na vinywaji na muda huo dada alikua ameshaleta zile portion za mbuzi. Iryn akaagiza Moet nyingine kama ileile kwa dada. Moet ina kilevi cha 13% ndomana mademu wanazipenda sana afu pia ni sweet.
Muda ule nilikua nawaza jinsi ya kumuingia Iryn kuhusu suala la Muajemi, lakini nikasema acha kwanza moet imkolee. Na muda huu DJ alikua kashaanza kuchanganya mangoma, dizaini kama vibe lilianza kupanda.
DJ aliipiga ngoma ya “Ruger-bounce” na palepale Iryn alitoka kwenye kiti akaanza kukatika taratibu, yaani ni alikua anakata kiuno kwa mapozi, taratibu alikua anashuka chini kwa beat na kupanda. Nilipigwa na butwaa maana nilikuaga namchukulia simple sana, hata jamaa na dem wake ilibidi wawe wanamwangalia.
Majirani wa karibu walianza kuyaelekeza macho kwake jinsi alivyokua akikata kiuno kwa mpangilio. Nafikiri walishangaa sana kuona mrembo mzuri kama yule anajua kukata mauno, na muda huo dada alikua ameleta moet tayari.
Kilikua ni kitendo cha dakika lakini was amazing, kiliweza kuteka attention ya watu pale. Nikamwambia naona umeamua kuniprove wrong, sina cha kusema tena. Niseme tu nakuongezea nyota zingine 5 ziwe 10.
Hii siku Iryn alikua na furaha sana maana vibe alilokua nalo ni hatari. Aliendelea kucheza na mimi nilikua nikimsapoti kwa kumshika kiuno na kumbambia.
IRYN: “Insider unajua ni muda sana sijatoka out kama hivi, last time kuenjoy hivi ilikua ni Ufaransa.”
MIMI : “Mara moja moja inatakiwa uwe unatoka unafurahia maisha. Unajua kukata mauno asee sikupatii picha kwa bed.”
IRYN : “Pombe zimeanza kukuingia eeh.”
MIMI : “Unakumbuka hata kule Coral unikazia namba ya yule mzungu ulisema nimelewa.”
IRYN : “Kumbe husahau tu..”
MIMI: “Kuna jambo nataka nikwambie kuhusu yule Mwarabu wa siku ile unamkumbuka?”
IRYN: “Yeah. Kwani mnawasiliana naye?”
MIMI : “Exactly, alichukua my number that day. Hata hivyo sio Mwarabu ni Muajemi.”
IRYN : “Nakusikiliza , Go on”
MIMI : “Alinipigia simu akaomba tuonane, nikamwelezea Iryn mkanda mzima wa siku ile. Muajemi ana connection nyingi sana anaweza kukusaidia hasa kwa dubai anaonekana sio mtu wa kawaida. Yeye alikua anaomba muonane tu, sijui anataka muongee nini.
IRYN : “Do you trust him?”
MIMI : “Ofcourse, he can be strusted”
IRYN : “Ok will discuss about this”
Muda huu aliomba nimpe tena company anakwenda toilet, nikampeleka nikamsubiri tukarudi mezani. Ofcourse kwa yale mazingira angekua anakwenda peke yake angesumbuliwa sana na wahuni. Na Iryn ni kinda ya mwanamke ambaye hapendi sana kusumbuliwa au kusimamishwa anaonaga kama ni dharau.
Tulikaa pale mpaka saa8 tukaamua tuondoke, alikuja dada na bill, nakumbuka bill ilikua 573,000/= Iryn alilipa na akampa dada 50,000 ya huduma yake. Dada alishukuru sana ni kama hakuamini na akaomba next time tuwe tunamtafuta yeye alitutajia jina. (Huyu dada ni rafiki yangu mpaka sasa navyoandika hapa, nikienda pale Kidimbwi huwa ananipa huduma yeye).
Tulivyofika pale getini Maasai baada ya kutuona akaja chap, sababu niliskia muda ule Iryn anasema atampa elfu 10, bhasi nikatoa nikampa. Masai alifurahi sana na Iryn akamwambia next time nikija ole wako ulete uswahili.
Nikamshukuru Iryn kwa out then nikawasha gari tuondoke tukalale, wakati tumevuka geti la Kidimbwi kuna gari ilikuja kwa spidi sana na ikatugonga “BOOM”. Ilisikika sauti ya Iryn “Mamaaaa…….”.
TO BE CONTINUED……….
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu