SEASON 2
EPISODE 31
βBY INSIDER MANβ
PREVIOUS:
Nilikuwa mpole ghafla hata sikuwa na usemi tena, ilinibidi nikubaliane na matokeo. Niliwaza kule gheto naishi kisera sana kuna godoro la 4x6 halafu liko chini. Nilijisemea pale, βmtoto kautaka acha niende nae tukifika huko itajulikanaβ.
CONTINUE:
MIMI: βSawa haina shida tutaenda wote kama umeridhia.β
MARY: βAu hujapenda?β Aliongea kwa sauti ya kudeka.
MIMI: βOfcourse yes.β
MARY: βHiloooo! nitakuwa na wewe mpaka niijue Dodoma yote. Ulisema una matatizo yanakusumbua, you can share with me if you want.β
MIMI: βSababu umetaka kujua matatizo yangu nitakwambia yote.β
Nilianza kumsimulia Mary mkasa mzima wa mahusiano yangu na Iryn mpaka kinachoendelea sasa. Hata baada ya kumaliza kumsimulia aliishia kunionea huruma na kunitia Moyo. Hapo sasa, ndiyo kufahamu mimi nilikuwa kwenye mahusiano na Iryn, lakini nilimsihi sana asithubutu kumwambia Jane na iwe siri yake.
MARY: βPole sana Insider ndomana umeamua kuja huku kufanya mishe zako. Na unafanya mishe gani huku sasa?β
Nilimuonesha mikono yangu na nikasimama aone jeans yangu ilivyoshika ma-oil.
MIMI: βNadhani umejua ninajishughulisha na nini tayari.β
MARY: βSema hongera kwa maamuzi uliyoyachukua naamini soon utakuwa vizuri.β
MIMI: βYeah! Kwasasa na focus na maisha yangu.β
Baada ya maongezi ya muda mrefu tuliondoka huku nimeshika bag lake mkononi na nilichukua bajaji ya kutupeleka gheto.
Dakika chache tu baada ya kuwasili nyumbani, ilikuwa saa mbili za usiku. Tulipoingia ndani ya geti, niliona dada wawili majirani wamekaa kibarazani wakipiga story. Wote walionekana kushangazwa sana kuniona nikiwa nimeambatana na mrembo.
Sikuwa na uhusiano wowote na majirani wa pale, isipokuwa Michael pekee. Ilikuwa vigumu sana kuonana na majirani, kwani niliamka asubuhi na kurudi usiku. Zaidi ya hayo, nilikuwa mtu asiyechangamana sana na wengine.
Ilikuwa kama wale dada hawakuamini kwamba kweli ni mimi niliyekuwa naingiza mrembo pale nyumbani. Nilipowaamkia, kabla hawajapata nafasi ya kujibu, Mary naye aliwasalimu, nao wakatuitikia. Kisha, nikafungua mlango wa ghetto na tukaingia ndani.
MIMI: βKaribu sana hapa ndiyo nakoishi.β
MARY: βWaow! Pazuri mbona, sijaona mazingira uliyosema hayafai mimi kukaa?.β
Mary alianza kuvua nguo pale ili akaoge, picha linaanza nakumbuka bafuni hakuna sabuni ya kuogea. Niliinuka ili nikanunue sabuni, ili nimpe na nafasi mle chumbani, ile nataka kuondoka akaniita;
βInsiderβ¦ unaenda wapi sasa?β
MIMI: βNaenda dukani mara moja mtaa wa nyuma kununua sabuni ya kuogea, soon narudi.β
Mary alicheka kidogo, kisha akaenda kuketi juu ya godoro. Wakati huo alikuwa amevaa bikini yake nyeupe pamoja na bra nyeupe juu.
MARY: βUsijali, sabuni nilitembea nayo. Halafu, unaogaje bila sabuni baby.β
MIMI: βJuzi ilidumbukia kwenye sink ndomana. Acha nikanunue sabuni kwaajili yangu, nikirudi nitakuta umemaliza.β
MARY: βTutatumia yote hii haina shida hata mwanaume anaweza kutumia pia.β
MIMI: βSawa haina shida, subiri nikuchemshie maji, huku kuna baridi sana.β
Baada ya Mary kutoka kuoga tulianza kupiga story pale na kubwa nilitaka kujua anafanya research ya nini, akasema anafanya research ya leadership.
Kwa upande wangu nilikuwa nausingizi sana pamoja na kuchoka, hivyo baada ya kutoka kuoga niliishia kulala na yeye aliendelea kuwa busy na laptop yake.
Asubuhi nilikuwa wakwanza kuamka, lakini yeye alikuwa bado kalala, hivyo nilianza kujiandaa ili niende kazini. Kwa siku za jumapili huwa siendi ofisini, lakini ilinilazimu kwenda sababu ya fundi alikuwa anakuja kutengeza vizuri mfumo wa umeme.
Nilitoka pale home saa 2 za asubuhi kuelekea mzigoni na fundi alikuwa kawasili mapema akinisubiri. Baada ya kuonana na fundi, alianza kutengeneza, nami nilikuwa nikimsubiri pale maana ilikuwa ni kazi ya masaa 2 tu.
Nilimtumia message Mary kumpa taarifa nimetoka mara moja na nitawahi kurudi ili tukale lunch, sababu muda naotoka alikuwa bado kalala.
Michael alinipigia simu na ile kuona ni yeye nilipokea simu kwa haraka sana;
MICHAEL: βKaka salute asee! naona umeamua kuachia makucha yako.β
MIMI: βHahahaa! Kwanini kaka?β
MICHAEL: βOyaa huyu dada anayeanika nguo hapa nje ndo shem wetu nini?β
MIMI: βHahahaha! Kaka nakuja soon tutaongea.β
MICHAEL: βKaka nimeshindwa kuvumilia, imebidi nikupigie simu.β
MIMI: βKwani anafua nguo?β
MICHAEL: βPicha linaanza namuona anatoka magetoni, halafu sasa ana confidence zote, kaka kama mwanamke unaye asee.β
MIMI: βKaka relax nitakucheki soon.β
Niliwaza pale ina maana Mary anafua nguo? Ninakumbuka nina nguo chafu mle gheto atakuwa kaamua kuzifua.
Saa sita mchana niliachana na fundi baada ya kumaliza kazi na wakati narudi nilipitia mgahawani, nikanunua chips kuku sahani mbili, nikaendelea na safari yangu ya kurudi home.
Nilipoingia pale uwanjani, niliona nguo zangu zote zimefuliwa, hata boxer zilikuwa zinang'aa. Nilijikuta nikiwa nimeishiwa maneno, maana sikutarajia kabisa Mary kufanya hivi. Nilisimama kwa muda nikitafakari, kisha nikaingia ndani, ambako nilimkuta akiwa amelala kitandani.
MIMI: βMummy pole! Mbona unajipa majukumu ambayo sio yako?β
MARY: βNitakuwa mwanamke wa ajabu kukubali kukaa na nguo chafu ndani.β
MIMI: βThat was not your job, hujaja hapa kwaajili ya hili.β
MARY: βUnasahau kwamba mimi ni mwanamke na sifa yangu ni usafi?β
MIMI: βSawa yaishe mummy, nimekuletea chakula ule.β
Niliachana na Mary, kisha nikaenda kuonana na Michael pale kwake na nilimkuta amekaa seblen;
MIMI: βBrother mambo vipi, naona umetulia.β
MICHAEL: βKaka hapa nina stress kwanza, hizi kazi za serikali ni za kikuda sana.β
MIMI: βShida ni nini kaka.β
MICHAEL: βMwanangu si nimepigwa transfer hapa, natakiwa kwenda Mtwara huko.β
MIMI: βDuh! Pole sana mzee baba, lakini mtwara ni kuzuri mzee.β
MICHAEL: βNasikia hivyo, sema maisha ni popote nitaenda no way.β
MIMI: βLini unakwenda huko?β
MICHAEL: βUkishapewa barua unatakiwa kwenda kuripoti kituo kipya, hapa nimechukua likizo kwanza halafu huko nitaendaga.β
MIMI: βUkiondoka hapa si nitapata shida maana wewe ndo mtu pekee ambaye tunakaa na kupiga story kama hivi.β
MICHAEL: βUsiwaze kaka, simu zipo tutaendelea kuwasiliana. Kaka yule dada ndiyo shemeji nini? Maana ni mzuri balaa, nimeamka naona anaanika nguo, nikajisemea huyu dada mbona sijawahi muona, ghafla naona anaingia kwako.β
MIMI: βHuwezi amini kaka huyo dada ni mshikaji wangu na hapa Dodoma kaja ana masuala yake tu, usiniwazie vibaya.β
MICHAEL: βKaka yaani mlale wote halafu usimguse?.β
MIMI: βAmini kwamba kaka.β
MICHAEL: βHili nakupinga lazima mlane tu. Kwanza unapata wapi jeuri ya kumuacha mwanamke kama yule, labda uwe na matatizo.β
MIMI: βHahahaa! Kaka wacha nikukimbie tutachekiana badae bhasi.β
MICHAEL: βBadae tutoke out tukapate hata dinner.β
MIMI: βHaina shida maana niko na mgeni lazima iwe hivyo.β
Baada ya kuachana na Michael nilirudi gheto, lakini cha ajabu nilikuta Mary hajala eti alikuwa ananisubiri mimi ili tule wote.
Wakati tunakula nilianza kumuuliza anipe ratiba zake za kesho akasema hana ratiba yoyote na ataondoka na mimi kwenda mzigoni, pia aione na ofisi yangu.
Saa moja usiku tuliamua kutoka kwenda kupata chakula cha jioni pamoja na Michael, na tukachagua Golden Fork. Wakati tukiwa pale, Michael, kama kawaida yake, alianzisha ucheshi wake kwa Mary kwani ni mtu wa maneno sana. Mary alionekana kufurahia sana ucheshi wake.
******
Jumatatu asubuhi tuliondoka wote kwenda mzigoni, lakini tulianzia kwanza dukani na tulikuta dada kafungua tayari. Nilimtambulisha Mary pale dukani na hatukukaa sana tukaondoka kwenda goli lingine workshop .
Baada ya kuwasili pale, dogo alikuwa busy akiziba pancha na nilifanya utambulisho kwa haraka. Mary aliendelea kushangaa mazingira kwa umakini nami niliingiandani ofisini kwa Sanchi ili nimsalimie na yeye.
Sanchi alikuwa bize sana na laptop yake, lakini alishtuka kuniona, tulisalimiana kwa furaha. Niliamua kuvuta kiti na kukaa karibu naye, kisha tukaanza kupiga stori. Mazungumzo yetu yalijikita zaidi kwenye simu aliyotaka nimuagizie. Nilimuuliza anataka iPhone toleo lipi, naye bila kusita akajibu, "Latest, 14 Pro Max."
Nilimpigia simu jamaa yangu wa Mlimani City mbele ya Sanchi, naye akanipa bei. Nilimuomba jamaa atupunguzie bei ili niweze kununua simu hiyo. Wakati tunaendelea kuzungumza na jamaa kuhusu punguzo la bei, Mary aliingia ofisini. Nilimpisha akae, na mimi nikasimama kwa sababu hakukuwa na kiti kingine cha kukaa.
Baada ya kumaliza kuzungumza kwa simu, Sanchi alisema kwamba tutakuwa tumelipia simu hiyo ifikapo mwisho wa wiki. Wakati huo, alianza kumuangalia Mary kwa makini sana. Bila kuchelewa, nilifanya utambulisho ili kuweka mambo sawa.
MIMI: βSanchi, huyu unayemuona mbele yako, anaitwa Mary, ni mpenzi wangu kutoka Dar es Salaam na amekuja Dodoma kwa ajili ya research. Baby, huyu unayemuona ndiyo boss top manager wa hapa kituoni anaitwa Sanchi, mwanamke mwenye bunango lake hapa mjini.β
Niliamua kumtambulisha Mary kama mpenzi wangu ili asinichukulie poa, awe na heshima, atambue ninamiliki chombo kali.
Wakati huo, Sanchi alikuwa akicheka kutokana na utambulisho na akaanza kuzungumza na Mary pale;
SANCHI: βKaribu sana Mary, nilishakutambua toka hata sijatambulishwa, jumamosi wakati anakufata mimi naelewa kinachoendelea japo alinigomea.β
MIMI: βNilitaka nikupe surprise kama hivi. Vipi mbona hunisifii nina miliki chombo kali? Au unamuonea wivu mpenzi wangu?β. Na nikamkiss Mary shavuni βMwaahβ.
SANCHI: βChombo unacho ufanye mpango uoe sasa, wifi yangu nimefurahi kukuona. Insider ni rafiki yangu sana wa hapa kazini, muda wote ni matani kama hivi, usijisikie vibaya.β
MARY: βAhsante sana, nimefurahi kukufahamu pia.β
Niliwaacha waendelee kuongea nami nilitoka kuendelea na majukumu ya kazi. Baada ya dakika 10 Mary alitoka, akasema nimpe kazi ya kufanya, hataki kuwa idle.
Mchana muda wa lunch, nilimpeleka Mary kwa mama Gire, na ilikuwa mara ya kwanza kwa Mary kula kwa mama ntilie katika historia yake. Mama Gire alishangazwa sana kuona mtu wa hadhi kama Mary akila pale kwake, na hata watu wengine walikuwa wamkishangaa.
Tuliagiza wali na nyama sahani mbili na tukaanza kula huku tukipiga stori za hapa na pale. Mary alikula nusu ya chakula chake, akasema ameshiba. Nilipomaliza changu, niliendelea kula kile kilichobaki na hivyo kumwacha Mary kwenye mshangao.
Jioni dada wa dukani alinipigia simu na kunitaarifu kwamba amepatwa na msiba wa Uncle yake pale kwao, hivyo anaomba ruhusa aende nyumbani. Ni taarifa mbaya ambayo ilinishtua, hivyo nilimuomba anisubiri kwanza ili tuonane tuzungumze.
Nilimpa Mary taarifa juu ya hili, kisha tukaondoka wote kwenda dukani kuonana na dada. Baada ya kuonana naye, tulimpa pole na alianza kunipa mkasa kuhusu kifo cha Uncle yake. Nilimpa laki mbili cash kwaajili ya msiba na nikamwambia tutaendelea kuwasiliana.
Usiku tuliwasiliana tena kuhusu mazishi na dada alisema kwa taarifa za haraka watazika kesho Gairo. Baada ya kuongea na dada niliwaza nikaona ni busara nikaenda kwenye huu msiba, pia itasaidia kutengeneza mahusiano mazuri.
Nilimpigia tena simu kumuuliza muda watakao kwenda huko Gairo, akanambia bado hana ratiba kamili. Nikamuomba anielekeze kwao ili kesho mapema niende, dada alinielekeza anakaa Mnadani.
Kipindi naongea na dada, Mary alikuwa bafuni na baada ya kutoka nilimtaarifu kuwa kesho nitaenda msibani. Kwa upande wake alitaka twende wote, lakini nilimuomba anisaidie kushinda dukani, ili mimi niende huko na akakubali.
Niliona kuna umuhimu wa kumuazima gari Aggy ili nisipate tabu hata nikienda huko Gairo. Nilimpigia simu Aggy kumuelekeza kuhusu msiba, akasema kesho asubuhi niende ofisini kwake tukaongee kuhusu hili.
Saa mbili asubuhi, tulienda dukani pamoja na Mary kwa ajili ya kumuonyesha bei za bidhaa. Kulikuwa na price list, hivyo hilo lilikuwa rahisi. Tatizo lilikuwa kwenye matumizi ya mashine ya EFD, kwani Mary alikuwa mgeni kabisa na mashine hizo. Ilibidi nimfundishe jinsi ya kutoa risiti na kuingiza taarifa za mteja kama TIN, jina, na kadhalika.
Nilikuwa nimeamua kufuata sheria za biashara, sikutaka konakona. Mteja akija kununua bidhaa, lazima apewe risiti. Hii ilisaidia sana katika kuvutia wateja wengi, hasa makampuni, kwani wakifanya malipo, wanapewa risiti mpaka upande wa service.
Kwenye kampuni, gharama zote zinazotokana na matumizi kama petrol, kufanya service, na nyinginezo zinahesabika kama 'expenses.' Ikiwa gharama hizi hazina ushahidi wa risiti, TRA haiwezi kuzielewa. Hii ndiyo sababu kampuni nyingi zinapenda kufanya kazi na watu wenye uaminifu ambao wamenyooka, kwani risiti ni muhimu kwa ajili ya kuthibitisha matumizi.
Baada ya Mary kumasta kwenye kutoa risiti niliamuaga pale na nikamwambia kama kutakuwa na tatizo awe anapiga simu namuelekeza.
Niliondoka kwenda workshop kuonana na Juma βdogoβ, kisha nikamuaga nakwenda msibani. Baada ya hapo niliingia ndani kuonana na Sanchi na kumwomba awe ananisaidia kuangalia ofisi na nikaondoka kwenda kuonana na Aggy.
Kutoka workshop mpaka ofisini kwake hata sio mbali na ndani ya muda mfupi nilikuwa nimewasili. Baada ya kuonana tuliongea kuhusu msiba wa dada, lakini kwa upande wake alisema amebanwa sana na kazi. Aggy aliomba nimuwakilishe na akatuma 150,000 kwenye simu, laki moja kwaajili ya dada na inayobaki ichangie wese.
Habari nyingine alinambia ijumaa atachukua likizo, hivyo ataondoka kwenda mkoani kuwasalimia wazazi. Tuliagana pale, kisha nikaondoka kuelekea Mnadani msibani kwa dada.
Saa tano asubuhi niliwasili pale kwao na yeye ndo aliyenipokea na kunikaribisha ndani na akanitambulisha kwa ndugu zake. Baada ya hapo nilienda kukaa na wanaume wenzangu ambao walikuwepo pale msibani.
Saa saba mchana tulianza safari ya kwenda Gairo kwa ajili ya mazishi. Tulitumia kama masaa mawili kuwasili pale mjini na tuliendelea tena na safari nyingine kama ya nusu saa hivi, kwani tuliingia ndani kidogo.
Kufikia 12 jioni mazishi yalikamilika, sikutaka kuondoka mapema ili niweze kuonana na dada nimuage. Nilifanikiwa kuonana naye na tukaongea kidogo, na kubwa nilimwambia akikaa sawa ndo arudi kazini na aondoe wasiwasi.
Nilipata wazo nilale hukuhuku Gairo ili kesho yake asubuhi nifanye kazi ya kutafuta wateja wapya, nisiwe nimekuja bure. Nilitafuta lodge ya karibu na mazingira ya barabarani kwaajili ya kulala.
Kipindi chote niko msibani mpaka naenda Gairo nilikuwa nawasiliana sana na Mary. Wakati niko lodge nilimpigia simu kumpa taarifa kwamba sitoweza kurudi mpaka kesho, nilimwambia dhumuni langu ni kutafuta wateja wapya.
Kesho yake, ilikuwa siku ya Muungano. Nilipoamka, niliona missed call mbili kutoka kwa Mary, hivyo nikaamua kumpigia haraka kwani nilihisi labda alikumbana na changamoto. Tulipoongea, aliniambia kuwa alinipigia simu ili kuuliza sehemu duka lilipo, lakini alifanikiwa kufika. Aliendelea kuniuliza nitarejea lini?.
Nilitoka lodge saa nne asubuhi na kuanza kazi ya kutafuta wateja. Kwa kiasi kikubwa, nilifanikiwa kupata wateja wawili wa uhakika na wengine waliahidi kunitafuta. Hivyo, sikujutia maamuzi yangu ya kwenda Gairo.
Baada ya hapo, nikaamua kuanza safari ya kurudi Dodoma kwa spidi kali ili nifike mapema. Nilitaka kurudi gheto kwanza kubadilika, kisha niende kwa dogo ili nioshe gari kabla ya kurudisha kwa Aggy. Nilianza kwa kupitia dukani kuonana na Mary ili nichukue funguo za gheto. Tulipiga stori kidogo, kisha nikamuaga na kuondoka kwenda kuoga.
Nilipofika gheto, baada ya kuingia ndani naona kila kitu kilikuwa kimeboreshwa sana. Mary alikuwa amenunua kitanda kipya, jiko la gesi, kabati la vyombo ambalo juu linaweza kuweka jiko, na pia fridge dogo. Nilipolifungua, nikaona tayari limejaa mazaga ya kutosha, na hakusahau kununua microwave pia.
Gheto lilikuwa limependeza sana halikuwa tena la kisela. Niliishia kuketi kitandani huku nikitafakari mambo aliyofanya Mary. Ni vigumu kwa wanawake wa kipindi hiki kufanya mambo kama haya na hili jambo lilizidi kunikosha.
Niliingia kuoga haraka na wakati nikijiandaa, Aggy alipiga simu kuniuliza kama nimerudi na akasema tukutane workshop. Niliendelea kujiandaa kwa haraka, kisha nikatoka kwenda golini.
Baada ya nusu saa Aggy aliwasili pale ofisini na tukaanza kuongea, na kubwa ilikuwa kuhusu msiba na baadae tulianza kuongea masuala mengine;
MIMI: βAggy hii gari nikupe hela maana inanikosha sana.β
AGGY: βHii gari sijawahi fikiria kuuza naenda mwaka 2 inadunda, sijawahi fanya service kubwa zaidi ya kubadilisha oil na service ndogondogo.β
MIMI: βIko vizuri sana kwakweli, pia unajitahidi sana kuitunza.β
AGGY: βKesho nitakuwepo, nitakusaidia kushinda dukani.β
MIMI: βKwani holiday inaendelea na kesho?β
AGGY: βHapana! Nishapewa barua yangu ya likizo kuna haja gani ya kwenda?β
MIMI: βHapo sawa, lakini kule dukani kuna mtu toka jana alikuwepo.β
AGGY: βOoh! ni nani?β
MIMI: βMy friend from Dar es Salaam, atakuja utamuona.β
AGGY: βWa kike au kiume?β
MIMI: βWa kike kama wewe.β
AGGY: βAu ndo unakaa naye? Ndomana hutaki nipajue kwako.β
MIMI: βAna masuala yake ya research ndo yamemleta huku na amekuja jumamosi.β
AGGY: βMhh! Nikimuona nitajua kama kuna something fishy.β
MIMI: βUnapenda sana kuyafuatilia mambo yangu.β
Saa 12 jioni, Mary alifika pale golini na alinikuta nikiwa na Aggy. Alifika hadi usawa wetu, akatusalimia, na akaanza kuniuliza kuhusu habari za msibani. Nami nilimuuliza kuhusu maendeleo ya biashara. Wakati wote tulipokuwa tukiongea, Aggy alikuwa kimya sana akitusikiliza, na nikafanya utambulisho.
MIMI: βMary huyu unayemuona anaita Aggy ni moja ya rafiki yangu mkubwa sana. Tumesoma pamoja O`Level na chuo tumesoma kimoja, anafanyia kazi taasisi X kama mchumi.β
MARY: βWaow! Iβm happy to know you, Aggy.β
MIMI: βSijamaliza bado utambulisho, Aggy huyu anaitwa Mary ni rafiki yangu mkubwa kwa Dar, licha ya kuwa na ratiba zake, lakini bado amenisaidia kushinda dukani.β
AGGY: βNimefurahi kukufaham Mary, karibu sana Dodoma na karibu kwetu upajue.β
MIMI: βNafikiri tukitoka hapa tukapate dinner ya pamoja, Aggy utalipia.β
AGGY: βHahahaa! Kama ulikuwa kwenye mind yangu nilitaka kusema vivyohivyo.β
Mary aliaga anakwenda msalimia Sanchi, nikaendelea kuongea na Aggy pale;
AGGY: βInsider hawa wanawake unawapatiaga wapi? Na mama J hasemi kitu?β
MIMI: βKwamba anipe limit ya marafiki wa kuwa nao? Embu acha zako, leta story zingine za kuongea.β
AGGY: βAcha nifunge bakuli langu, huchelewi kusema nakufuatilia.β
Tulienda Collina kupata dinner na baada ya hapo tuliagana na Aggy, tukarudi home kulala. Tulikuwa tumepanda bodaboda mshikaki, na muda huu nilikuwa nalifeel joto la Mary mpaka mwili ukaanza kusisimuka.
Baada ya kuwasili nyumbani, kwanza nilienda kumsalimia Michael. Sikutumia muda mrefu nikarudi Geto, na Mary alikuwa amelala kitandani kwa kujiachia sana.
Nilisogea mpaka usawa wake nikaanza kuongea naye;
MIMI: βMummy nashukuru sana kwa haya uliyofanya, lakini haikuwa na haja, ni sawa na kuchezea pesa. Mimi huku niko kwa muda na nitaondoka biashara ikisimama.β
MARY: βHata kama unakaa kwa muda mfupi, kwani si utakuwa unarudi? Mimi nimefanya kama ukumbusho wangu kwako.β
MIMI: βSawa mummy nashukuru, pole kwa uchovu wa dukani.β
MARY: βHata hakuchoshi ndiyo kwanza napata marafiki wapya wa huku, wewe ndo nikupe pole msibani, hujui tu! umefanya jambo la utu sana.β
MIMI: βTumezika salama, nimemwambia dada akiwa tayari ndo aje dukani.β
MARY: βNakuwazia kesho utafanyaje maana natakiwa kuanza kwenda kukusanya data nadhani nilikwambia kuhusu research yangu.β
MIMI: βUsijali kwa hili mummy. Halafu kwanini usitafute consultant akusaidie haya? Huoni kama utateseka sana?β
MARY: βHii research cunsultant atanisaidia hasa kwenye secondary data ila kwa hizi primary natakiwa kwenda direct kuonana na wakurugenzi, HODβs nknk, natakiwa kuwafanyia interview kabisa.β
MIMI: βHapo nimekuelewa na vipi kuhusu permits?β
MARY: βYule kaka niliyekutana naye jumamosi ndo amenisaidia hili na kesho tutaonana naye.β
MIMI: βNext week nitakupa kampani mummy sawa?β
MARY: βNa duka utamuachia nani?β
MIMI: βItafahamika hapohapo wewe niachie hili.β
Mimi nilikuwa nimechoka sana na kabla ya kulaa nilimwambia Mary tusali kwanza ndo tulale. Toka Mary anafika hakuna hata mmoja aliyeonesha dalili yoyote ya kutakana kimapenzi.
Kwa upande wangu sikuwa na mizuka kabisa maana akili yangu ilikuwa inawaza bishara tu. Pia sikutaka kumuingiza Mary kwenye majuto ndomana niliona ni bora tuendelee kuishi kama kaka na dada.
Niliamka asubuhi nikiwa na Upwiru sana, bunduki yangu ilikuwa imejikoki tayari kwa vita. Nilipiga jicho pembeni nauona mzigo wa Mary huu hapa yaani daah! Mawazo ya ngono yalianza kutawala akili yangu, lakini niliamua kwenda kuoga ili niondoke eneo hili.
Nijiandaa kwa haraka sana maana kwa asubuhi mara nyingi nilikuwa naondoka na Michael, ananiacha ofisini kwangu na yeye anaendelea na safari ya kwenda ofisini.
Wakati nataka kuondoka nilisikia Mary akiniita:
βInsider..β Nikageuka kumsikiliza pale,
βKazi njema see you laterβ
βThank you Mummyβ, nikatabasamu na kuondoka.
Muda huu Michael alikuwa kashawasha gari akinisubiri mimi ili tuondoke. Nilipotaka kufungua mlango mbele, nikakuta mtu, hivyo nikaamua kuketi kwenye siti za nyuma.
MICHAEL: βOyaa Insider, huyu mbele ni kaka yetu anaitwa Bony anakaa nyumba kubwa ana mke na watoto wawili. Kaka huyu ndo Insider ni mgeni hapa ana mwezi tayari toka ahamie, wakati anafika wewe ulikuwa safari.β
BONY: βDogo hongera unamiliki chombo kikali sana mpaka nikasema hivi kwanini niliwahi kuoa, umetisha sana.β
Tuliishia kucheka wote mle ndani ya gari nami sikutaka kuchangia neno, bali nilinyamaza kimya.
MICHAEL: βInsider badae itabidi tuonane kuna jambo tuongee kama utakuwa tayari.β
MIMI: βSawa! Tutawasiliana kaka.β
Waliniacha barabarani karibu na ofisi na wao wakaendelea na safari yao. Mimi nilitembea kuelekea ofisini na kwa mbali nilimuona Sanchi akiongea na wafanyakazi wake nami nilipita kama sijamuona.
Nilifungua ofisi na kuanza kutoa vitu pale nje na nilimuona Sanchi akija usawa wangu;
SANCHI: βToka mpenzi wako aje umekuwa na jeuri sana.β
MIMI: βKwanini unasema hivyo?β
SANCHI: βUnanipita kama hunipni, hata kunisalimia hakuna.β
MIMI: βNimekuona upo busy unatoa maelekezo isingekuwa heshima kukuharibia pale, lakini nilipanga ukimaliza nije ofisini tuongee.β
SANCHI: βHaya bhana, sikukupa hongera siku ile, lakini unakojolea pazuri sana.β
Nilicheka pale na wakati akielekea ofisini kwake nilikuwa nampa sifa kwa namna ambavyo kabarikiwa makalio, naye alikuwa anafurahi sana kusifiwa.
Kwa upande mwingine, toka nimtambulishe Mary niliona heshima imeongezeka sana maana alikuwa akinichukulia poa. Nilijisemea pale, kama Mary wanamuona pisi kali, hivi hawa watu wakimuona Iryn itakuwaje?
Baada ya Juma kuwasili, nilimuachia ofisi kisha nikaenda dukani. Kipindi niko dukani nikifanya mahesabu nilibaini hizi siku mbili ya katikati ya wiki, mauzo yalikuwa juu sana kuliko kipindi chote.
Haikupita nusu saa alikuja kaka mmoja akamuulizia Mary,
βKaka habari yako, kuna dada juzi alikuwa hapa dukani sijui yupo?β
βLeo hajaja, vipi ulikuwa unashida naye?.β
βNo! Nilipita kumpa feedback kutoka kwa fundi, oil ni original maana alihakikishia sana siku ile.β
βAhsante sana kwa feedback jumatatu atakuwepo.β
βAhsante sana.β
Niliwaza pale huenda jamaa alikuja kwa lengo la kuomba namba ya simu.
Mchana Aggy alikuja pale dukani kushinda na kubwa alisema jumamosi atakwenda kwao, hivyo ataniachia gari yake maana hawezi kusafiri umbali mrefu na gari, anaogopa.
Aggy ni moja ya watu wangu wa karibu sana, tukiwa pamoja huwa tunapiga sana story za kila aina. Ni moja wa wanawake ambao wananijua mimi kiundani zaidi, mimi na yeye ni kama ndugu.
Jioni Mary alikuja dukani na alinikuta bado niko na Aggy na alisema anawahi kwenda kupika. Eeh! bhana Aggy sindo kunipiga jicho kali sana muda huu baada ya kusikia yale maneno kutoka kwa Mary.
Bada ya Mary kuondoka alianza maswali pale;
AGGY: βInsider kumbe unaishi na huyu dada aseee wewe ni hatari.β
MIMI: βUnazingua, toka lini mimi kwangu na jiko? Na unajua fika naishi kisela?.β
AGGY: βSasa anakwenda wapi?β
MIMI: βAlikofikia kwa ndugu zake Aggy.β
AGGY: βKila nikigusia hili naona unakuwa mkali.β
MIMI: βKufuatilia mambo yangu unapenda sana.β
Aggy alinipa kampani mpaka Gheto na aliishia nje ya fence akaondoka. Baada ya kuingia ndani namuona Mary amekaa kibarazani anakatakata nyanya na vitunguu. βNikajisemea pale huyu Mary sasa too much ndo nini tena hii? Yaani daah! nilikuwa sitaki michoro lakini sasa sikuwa na jinsi.β
Nilienda kwa Michael maana alisema badae tuoanane atakuwa ana mazungumzo na mimi. Baada ya kuonana alinambia jumapili ataondoka kwenda Mtwara, hivyo alitamani sana nihamie pale kwake, kwani bado ilikuwa imebaki kodi ya miezi mitatu.
Licha ya kuhamia pale, bado alikuwa ana vitu kama TV, fridge kubwa, sofa, kitanda, kabati la nguo, home thieta, na vitu vingine vingi, alisema hawezi kusafiri na hivi vitu, hivyo nimpe hela na alihitaji million 2 tu.
Baada ya kupiga hesabu za haraka nikaona miezi 3 inanitosha sana kumaliza malengo yangu, hivyo wacha nihamie hapa. Kuhusu vitu niliona ni asset navyoondoka nitauza na kupata faida.
Nilimshirikisha Mary kuhusu suala la kuhamia pale kwa Michael, lakini alisema haina haja maana nitakuwa nachezea hela. Baadae alikubali baada ya kumwambia kuna kodi ya miezi mitatu imebakia na amenipa offa. Pia, kaniuzia vitu kwa bei chee, muda wa kuondoka ukifika nitaviuza.
***
Kesho yake ratiba yangu ilikuwa kwenda kushinda dukani na Mary aliendelea na ratiba zake za kwenda kukusanya data. Aggy alikuja pale dukani kushinda na mimi pamoja na kuniaga kwaajili ya safari yake ya kwenda mkoani.
Siku hiyo pia, nilipokea simu kutoka kwa mama J, na tuliongea kwa kirefu kuhusu mustakabali wa Junior. Alipendekeza aanze shule kuanzia Julai kwa sababu amekuwa na utundu mwingi. Lakini, kwa upande wangu, niliona bado ni mdogo kwani atakuwa na miaka miwili tu, hivyo nikamshauri tusubiri hadi Januari mwakani.
Baada ya kufunga duka niliondoka na Aggy kwenda kwake na alinikabidhi gari mpaka atakaporudi. Wakati narudi home Sanchi alinipigia simu na kuniomba niende Rainbow tukaonane ni muhimu.
Nilienda kuonana naye na baada ya kuwasili pale nilimpa taarifa, akasema niingie ndani na alinielekeza alikokaa. Walikuwa wako wawili na alinitambulisha ni rafiki yake, nami bila kuchelewa nilimuuliza sababu ya kuniitia pale.
SANCHI: βAgiza kinywaji hatujawahi kutoka tukakaa kama hivi, leo nimeamua nijiongeze.β
Nilitafakari pale, nikaamua niagize chupa mbili tu;
MIMI: βNafikiri sahivi unaweza kuongea unashida gani?β
SANCHI: βLengo la kukuitia hapa nataka nikupe pesa ya simu.β
MIMI: βSasa ndo unitie hapa? Kesho si tungeweza onana?β
SANCHI: βKesho sitokuwepo ndomana mpaka jumatatu.β
Mary alianza kupiga simu, lakini nilizichunia simu zake na haikuchukua muda akanitext kuuliza narudi muda gani, nikamwambia niko workshop nitarudi baada ya lisaa.
Baada ya nusu saa kupita, alipiga tena simu ikabidi nitoke nikapokelee kwenye gari sababu ya kelele,
MIMI: βNambie mummy.β
MARY: βInsider uko wapi?.β
MIMI: βNilikwambia niko ofisini mummy.β
MARY: βNiko hapa ofisini nimeambiwa hujaonekana muda mrefu.β
Nikajisemea hii imeshakuwa soo! Ina maana Mary kaenda ofisini?
MIMI: βIna maana huniamini mpaka ukaamua kunifuata?β
MARY: βNilikuwa bado sijarudi, nilikuwa nakusubiri turudi wote. Upo sehemu gani?
MIMI: βPanaitwa Rainbow mimi nakuja nisubiri hapo.β
MARY: βWewe ndo unisubiri mimi nakuja hapo.β
Niliwaza pale, hivi Mary akija akaniona na Sanchi na nmemdanganya hivi atanichukuliaje?. Hata hivyo nilijisemea βMary sio demu wangu potelea mbali asinifanye nishindwe fanya mambo yangu kisa yeye, kwanza aliforce kukaa na mimi.β
Nilirudi ndani kwa Sanchi na haraka niliagiza mbuzi choma na chipsi yai kwaajili yake na nikaagiza zifungwe vizuri;
SANCHI: βIs everything okay?β
MIMI: βNilikuwa naongea na Mary, yuko njiani anakuja. Akifika tu mimi naondoka nitakuacha mummy.β
SANCHI: βHata mimi sina maisha marefu hapa, tutaondoka wote.β
Baada ya dakika 10 Mary aliwasili pale Rainbow na alipiga simu kunipa taarifa, hivyo nikatoka nje kumchukua.
MARY: βUpo na nani hapa Insider, mpaka unanidanganya?β
MIMI: βNiko na Sanchi, aliniomba nipitie hapa kuna mzigo anikabidhi, kesho hatakuwepo.β
Nilimuomba aingie ndani ili amsalimie na Sanchi, akanigomea kwamba hawezi kuingia, hivyo atanisubiri pale nje. Nilimpa funguo ya gari ili akanisubiri kwenye gari, nami nilirudi ndani.
Baada ya kurudi ndani, Sanchi alishangaa kuniona narudi peke yangu bila kuwa na Mary;
SANCHI: βUlinambia baby wako anakuja yuko wapi?β
MIMI: βAmeishia hapo nje ananisubiri, dada akiniletea odda yangu mimi nitaondoka.β
Baada ya nusu saa kupita niliondoka huku nimeongozana na Sanchi kuelekea kwenye gari yake ili anipe pesa. Baada ya hapo tuliagana, kisha nikaenda kwa Mary kwaajili ya kuondoka na alionekana kununa sana, uvumilivu ulimshinda na alianza maswali;
MARY: βInsider una mahusiano gani na Sanchi?β
MIMI: βIna maana kipindi kile nafanya utambulisho hukunisikia?.β
MARY: βWhat did you say?β
MIMI: βTambua mimi na wewe sio wapenzi, kuanza kuniuliza masuala yangu binafsi unavuka mipaka na unanikosea sana.β
MARY: βNatambua hilo, pia naheshimu tunaishi pamoja kwa kipindi hiki ambacho niko huku. Siwezi kufurahi kuona unaenda kwa wanawake zako wakati mimi nipo ndani, si sawa naomba uniheshimu kwa hili.β
MIMI: βSanchi aliniomba nipitie, anipe pesa kwaajili ya simu ambayo anataka kuagiza kutoka Dar, lakini wewe unawaza vitu vingine kabisa.β
MARY: βWhy ulinidanganya sasa kama hakuna tatizo?. Nimeambiwa workshop hujaonekana toka mchana.β
Hapa sikuwa na cha kujibu ikabidi ninyamaze. Tulipofika home Mary alikuwa bado amenuna sana hata hakutaka kula.
Asubuhi na mapema sana niliondoka kwenda dukani nayeye alikuwa bado amelala. Hii siku nilipata ugeni kutoka kwa moja ya rafiki yangu tuliyefahamiana tukiwa jeshini. Ibrah alikuwa ni moja ya washikaji zangu wakubwa pamoja na Bob mjeshi jamaa yake Lucy.
Ibrah alikuja pale dukani na tulishinda siku nzima tukipiga story na nyingi hasa zilikuwa kuhusu jeshi. Ibrah alisoma chuo Dodoma baada ya kumaliza, alianza kufanya harakati zake za maisha palepale mjini Dodoma mpaka sasa.
Nilimpa story kuhusu kukutana na Bob Dar es Salaam na aliomba nimpe namba yake ya simu ili wawe wanawasiliana. Kwa upande mwingine Ibrah alinishauri niweke na lubricants za pikipiki, kwani itasaidia kuongeza mzunguko wa pesa.
Saa moja usiku, nilifunga duka na kisha tukaenda nyumbani kwake alikopanga, na tulianza kucheza PlayStation game pamoja. Wakati huo, nilikumbuka zawadi ya PlayStation game niliyopokea kutoka kwa Iryn, lakini sikuwahi kuifungua kabisa.
Game lilinoga sana kiasi kwamba nakuja kuangalia muda umeenda sana. Saa yangu ilionesha ni saa nne kasoro usiku, hivyo nikamuaga Ibrah kwa ahadi ya kukutana siku nyingine.
Nilipofika Gheto mazingira yalikuwa kimya sana. Nilihisi huenda Mary atakuwa amelala, hivyo acha nimpigie simu anifungulie mlango.
Baada ya kutoa simu mfukoni nakutana na missed call ya Michael, nikakumbuka kesho ni jumapili anaondoka halafu hatujaonana, wacha nimpigie simu ili kama kuonana tuonane leoleo.
Baada ya kumpigia simu, alipokea haraka na akaniambia kwamba alitaka kunijulisha kuwa Mary alimpa funguo za ghetto. Alipoona sioneshi dalili za kurudi mapema, ndipo akaamua kunipigia simu ili kunipa taarifa hiyo.
Mimi nilibaki nashangaa inakuwaje Mary ampe funguo Michael bila kunipa taarifa?
TO BE CONTINUED