SoC02 Jinsi biashara ya viatu inavyonitoa mavumbini

Stories of Change - 2022 Competition

Innocent Kirumbuyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2014
Posts
4,641
Reaction score
4,457
Hello

Mimi ni ndugu yenu innocent kirumbuyo kwa miaka miwili nimekuwa nikiweka story biashara ya viatu

1) Biashara ya viatu inaweza kukutajirisha

2) Utajiri uliojificha kwenye viatu vya mtumba

Nafarijika sana kwa kupokea maoni mengi na mawazo jinsi watu walivyo badili mitazamo yao na maisha yao kupitia mandiko yangu.

Cha pili Kipekee kabisa niwapongeze jamii forum kwa ili jukwaa limekuwa muhimili wetu wakubadili maisha yetu na jamii kwa ujumla kwasababu kupitia jamii forum nimekutana na watu wengi sana na muhimu sana kwenye maisha yangu.

OK

Niende kwenye mada moja kwa moja

Ni mwaka sasa toka nilivyoandika uzi kuhusu biashara ya viatu vya mtumba

3) Utajiri uliojificha kwenye viatu vya mtumba

Na leo niko mbele yenu kwa unyenyekevu kuwapa mrejesho na wapi nilipo paka sasa
Kwa kweli kila fursa uja na changamoto yake miezi miwili tu baada ya kuandika ule uzi

Nasikitika kusema nilivunjiwa magoli yangu yote na serikali kwasababu atukuwepo sehemu rasmi.

Pamoja na yote ayo sikufa moyo nilikuwa na akiba ya milioni moja (1000000).

Nikifikiri kitu gani cha kufanya na hiyo milioni

Ilinibidi niende kwanza kwenye maeneo machinga waliopelekwa kufika kule kwa kweli biashara ilikuwa ngumu sana wiki linapita aujauza pea ata moja nikaona huu ni ujinga

Nilichukuwa uwamuzi wa kuuza banda langu nikaanza kutembeza viatu mtaa kwa mtaa.

Kutembeza ni ngumu kidogo ila ilikuwa afadhali kwasababu kwa siku nauza ata pea mbili hadi tano.

Kwaiyo kidogo hali ikawa nzuri
Ndio siku moja nilipokea simu ya dada moja akiomba nimtafutie mtu anapangisha banda lake liliopo mjini mitaa ya lumumba Kwa laki moja kwa mwezi kwa mwaka Niliona kama ni fursa imekuja kwangu

Niliongea na mke wangu tukashauriana tupachukuwe hapo nikaenda kumuomba yule dada anifanyie milioni moja kwa mwaka yule dada akakubali
Nilimlipa pesa yake nikapewa banda ila sikuwa na pesa ya mtaji

Ikabidi niuze simu yangu ya mkononi nikauza na simu ya mke nikapata pesa kidogo nikaagiza mzigo Dar.

Baada ya kuagiza mzigo dar kwa kweli mimi na wife tulikuwa tunafanya kazi kwa juhudi sana baada ya mwezi moja tulianza kupata matokeo kwasababu tulianza kuona mabadiliko makubwa sana

Baada ya miezi 3 nikawa na mtaji kabisa na pesa za kutosha kwa kweli maisha yalikuwa yanaenda vizuri kabisa
Kuna siku mke wangu akaniambia Kuna eneo la mbele yetu linauzwa ni zuri na kubwa sana.

Na mimi kwakeli nilivyoliona lile eneo lilikuwa zuri sana ikabidi niongee na mwenye eneo akaniuzia lile eneo

Mara moja

Nikaanza kulijenga kwasababu lilikuwa eneo wazi tu nilijenga kwa kipindi kifupi kisha nikaamisha mzigo wangu

Kule nilipokuwa nimekodi ikabidi nimtafute mtu wa kunirudishia kodi ya miezi yangu iliyokuwa imebaki

Nilipata mtu akanirudishia kodi yangu miezi 6 nikamuachia pale mimi na mke wangu tukawa tunakomaa na pale tuliponunua

Nikiri tu kwa muda mfupi nimeona mafanikio makubwa sana paka naagiza mzigo paka wa milioni mbili na zaidi
Naona kabisa mafanikio makubwa mbeleni
Nakaribisha maoni ushauri na maswali kuhusu hii biashara

Pia nipo tayari kumsaidi mtu yeyote kufanya hii biashara viatu

Kama upo Mwanza nakukaribisha mitaa ya lumumba karibu na vunja bei ndio eneo banda langu lipo hapo tutabadilishana mawazo kama unatamani kufanya biashara ya viatu kwa vitendo nitakuelekeza BUREEE KABISA

ASANTE SANA
Moja goli langu lilovunjwa na serikali hapa ndio eneo nililoanzia na kukusanya mtaji.

IMG_20201109_194157_876.jpg
 
Upvote 54
Unatosha kabisa boss Mimi viatu vya kwanza vya biashara nilianza kwa laki nikawa nanunu viatu vya bei ndogo vya 6000 8000 na 10000 mwisho wa siku nilikuwa napata faida hadi laki 3
Nina mpango WA kuja kutafuta shekeli huko mwanza mkuu nitakutafuta mkuu unipe A B C
 
Mkuu nami nipo bush nahitaji sana kufanya iyo biashara. Naomba muongozo wa viatu vipi vinapendwa sana kijijini
 
Karibu sana boss ni jiji zuri sana kwa kutafuta maisha nadhani kwa Tanzania Mwanza ni best

Nasema hivyo kwasababu garama za maisha zipo chini sana hali ya hewa nzuri usafiri siyo shida alafu ni jiji linalotegemewa na mikoa ya kanda ya ziwa na jirani karibu sana
 
Hello

Mimi ni ndugu yenu innocent kirumbuyo kwa miaka miwili nimekuwa nikiweka story biashara ya viatu

Nafarijika sana kwa kupokea maoni mengi na mawazo jinsi watu walivyo badili mitazamo yao na maisha yao kupitia mandiko yangu.

Cha pili Kipekee kabisa niwapongeze jamii forum kwa ili jukwaa limekuwa muhimili wetu wakubadili maisha yetu na jamii kwa ujumla kwasababu kupitia jamii forum nimekutana na watu wengi sana na muhimu sana kwenye maisha yangu.

OK

Niende kwenye mada moja kwa moja

Ni mwaka sasa toka nilivyoandika uzi kuhusu biashara ya viatu vya mtumba

Na leo niko mbele yenu kwa unyenyekevu kuwapa mrejesho na wapi nilipo paka sasa
Kwa kweli kila fursa uja na changamoto yake miezi miwili tu baada ya kuandika ule uzi

Nasikitika kusema nilivunjiwa magoli yangu yote na serikali kwasababu atukuwepo sehemu rasmi.

Pamoja na yote ayo sikufa moyo nilikuwa na akiba ya milioni moja (1000000).

Nikifikiri kitu gani cha kufanya na hiyo milioni

Ilinibidi niende kwanza kwenye maeneo machinga waliopelekwa kufika kule kwa kweli biashara ilikuwa ngumu sana wiki linapita aujauza pea ata moja nikaona huu ni ujinga

Nilichukuwa uwamuzi wa kuuza banda langu nikaanza kutembeza viatu mtaa kwa mtaa.

Kutembeza ni ngumu kidogo ila ilikuwa afadhali kwasababu kwa siku nauza ata pea mbili hadi tano.

Kwaiyo kidogo hali ikawa nzuri
Ndio siku moja nilipokea simu ya dada moja akiomba nimtafutie mtu anapangisha banda lake liliopo mjini mitaa ya lumumba Kwa laki moja kwa mwezi kwa mwaka Niliona kama ni fursa imekuja kwangu

Niliongea na mke wangu tukashauriana tupachukuwe hapo nikaenda kumuomba yule dada anifanyie milioni moja kwa mwaka yule dada akakubali
Nilimlipa pesa yake nikapewa banda ila sikuwa na pesa ya mtaji

Ikabidi niuze simu yangu ya mkononi nikauza na simu ya mke nikapata pesa kidogo nikaagiza mzigo Dar.

Baada ya kuagiza mzigo dar kwa kweli mimi na wife tulikuwa tunafanya kazi kwa juhudi sana baada ya mwezi moja tulianza kupata matokeo kwasababu tulianza kuona mabadiliko makubwa sana

Baada ya miezi 3 nikawa na mtaji kabisa na pesa za kutosha kwa kweli maisha yalikuwa yanaenda vizuri kabisa
Kuna siku mke wangu akaniambia Kuna eneo la mbele yetu linauzwa ni zuri na kubwa sana.

Na mimi kwakeli nilivyoliona lile eneo lilikuwa zuri sana ikabidi niongee na mwenye eneo akaniuzia lile eneo

Mara moja

Nikaanza kulijenga kwasababu lilikuwa eneo wazi tu nilijenga kwa kipindi kifupi kisha nikaamisha mzigo wangu

Kule nilipokuwa nimekodi ikabidi nimtafute mtu wa kunirudishia kodi ya miezi yangu iliyokuwa imebaki

Nilipata mtu akanirudishia kodi yangu miezi 6 nikamuachia pale mimi na mke wangu tukawa tunakomaa na pale tuliponunua

Nikiri tu kwa muda mfupi nimeona mafanikio makubwa sana paka naagiza mzigo paka wa milioni mbili na zaidi
Naona kabisa mafanikio makubwa mbeleni
Nakaribisha maoni ushauri na maswali kuhusu hii biashara

Pia nipo tayari kumsaidi mtu yeyote kufanya hii biashara viatu

Kama upo Mwanza nakukaribisha mitaa ya lumumba karibu na vunja bei ndio eneo banda langu lipo hapo tutabadilishana mawazo kama unatamani kufanya biashara ya viatu kwa vitendo nitakuelekeza BUREEE KABISA

ASANTE SANA
Moja goli langu lilovunjwa na serikali hapa ndio eneo nililoanzia na kukusanya mtaji.

View attachment 2337121
Mkuu keshokutwa ntakuwepo Mwanza nakuja kumsalimia Maza, ntapita golini kwako nichukue hata pea moja halafu tupige stori za biz,
 
Mkuu nami nipo bush nahitaji sana kufanya iyo biashara. Naomba muongozo wa viatu vipi vinapendwa sana kijijini
Ukitaka boss ufanye biashara ya viatu asa vya mtumba ukapata pesa paka ukafurahi kwa vijijini kwa uzoefu wangu

Ukienda mlango moja Kama upo mwanza ukifungua yale marobota wewe usichaguwe subiri paka muda watu wameshachambua wewe nenda kwa yule alifungulisha mwambie akuuzie kwa top

Kwa kila kiatu unaweza nunua ata 2000 mbili mnahesabu unaweza kupata ata pesa 400 ukishanunua unachukuwa unaenda kijijini kwenye masoko yao huko wewe unamwaga kila kiatu usema 8000 watachambua ukiona vizuri vimepungua unakata bei tena 6000 watachambua tena ukiona vimepungua tena 3000 paka viishe
 
Kwa mtindo huu unaweza kuuza nusu ukarudisha pesa yako na faida juu
 
Back
Top Bottom