Wataalamu waje watueleze, mazoezi mengi yanaua vipi mchezaji au ndio humuimarisha mchezaji?
Mazoezi makali humuathiri mchezaji kama yatafanyika karibu na mechi, mfano siku moja kabla na labda siku mbili kabla. Tofauti na hapo, mazoezi makali humjenga mchezaji.
Kitu kingine labda useme Cadena anawapa mazoezi makali halafu hawali vizuri, wanakula chips, hapo lazima waathirike. Pia, useme, wachezaji wa Simba wamezeeka.
Kwa mechi ya Simba, na Asec unaona kabisa wachezaji wa Simba hawana mazoezi ndio maana walichoka sana baada ya kukimbizwa na madogo wa Asec.
Hivi unahisi madogo wa Asec hawafanyi mazoezi makali sana kwa pumzi ile?
Kipindi tunacheza soka la mchangani, kocha alikuwa anapenda tucheze dakika 120 ili tukija uwanjani dakika 90 inakuwa mteremko.
Kingine, wachezaji wetu waishi kiprofesheno. Yaani, wajiongeze, mfano kama mazoezi yanaanza saa moja, yeye afike saa kumi na moja na nusu aanze mazoezi yake, ikifika saa moja anaunganisha na wenzake, pombe, sigara anaacha mpaka astaafu.