Master Legendary
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 576
- 876
Jana umewahi kulala kama nini na wewe...ukatuacha tunasherehekea
Yaani natamani uundwe mpambano wao pale leaders
Najuta kutokukusikiliza nisilale. Wajua sikutaka kutibua pilau nililolishwa na Kiba, coz show yake ilikuwa class sana na fans walinogesha haswa.
Mpaka sasa sipati picha ilikuwaje hadi wapambe wa Diamond wametepeta hivi, kwa vyovyote mtu wao alikalishwa ile kisawasawa hadi akanyoosha mikono juu.
Ova
Kama wapambe wake tu mmechanganyikiwa hivi, sijui huyo Diamond mwenyewe atakuwa kwenye hali gani muda huu.
Ali Kiba kajua kuwavuruga aiseeh!
Ova
We endelea kujitekenya na kucheka mwenyewe
Ni ukweli kuwa Ally alikuwa juu sana kuanzia 2007-2010....baada ya Dimond kuja na kuteka soko la Muziki huku akiwazima watu kama taa ally kiba alipotea kwa kasi ya kimbunga kabla ya kuanza kupanda juu kwa kutumia upepo wa Dimond...
Naposema upepo wa Dimond namaanisha kama ally kiba angekuwa na bifu na wasanii wengine kama Barnaba, Belle 9 asingepata kick hii anayoipata kutoka kwa watu ambao wengi wao wanamchukia Dimond for fun , Wengine sio hata mashabiki wa ally kiba..
Napenda kumpa sifa kijana ally kiba kwa kutumia nafasi hii vizuri na pia ameonyesha kubadilika katika sekta zifuatazo..
1. Mavazi, Before ally alikuwa anavaa tu ilimradi amevaa ila sasa amebadilika anapiga mavazi mazuri sana na anapendeza
2. Perfomance.. Kabla ya ujio na mapinduzi ya Dimond kiba alikuwa hatumii sana dancers pia alikiba alikuwa hajishughulishi na masuala ya kucheza na kuimba kwa pamoja kitu ambacho kilikuwa kinamnyima maxi miongoni mwa macho ya wapenda Burudani..
All and all nampa sifa Dimond kwa kumuathiri ally kiba Positively maana pengine bila Dimond ""ally kiba"" angeendlea kutuimbia nakshinakshi zake huku akiwa kavaa vibaya ni mapinduzi ya Dimond yaliyombadilisha ally kiba..
Pia Dimond asikate tamaa kwaajili ya wale wanywa viroba wa jana waliokuja kupiga buuuu...aendelee kufanya muziki mzuri na siku nyingine asipige shoo za viingilio vya mbuzi kama ya jana maana huwa zinajaa wahuni ambao hawana maana, kama wanampenda kiba mwambieni kiba aanze kupiga shoo za 50000 tuone kama wataenda..
#Muzikimzuridaima
Na bado,mtaongea mengi sana juma hili!Katiba inawaruhusu!!Ila naikumbuka methali hii"mbaazi ikikosa maua husingizia jua"Hakika kuzomewa inauma mno.
Weee ilikua hatari nakuambia....diamond chozi lilimlengalenga hakuamini,akajidai kupima upepo eti nimemaliza akidhani ataombwa arudi aaagh wapi watu wakawa wanamfukuza,davido alivyopanda alimuita akidhani watu watamshangilia wapi....Usiku wa jana ulikua mrefu sana kwa ndomo na mashabiki wake [MENTION=81108]honey Faith
Hahahaaa usiku ulikuwa mrefu. Ukiongeza na migwanda aliyovaa nadhani hata kutembea alikuwa hawezi.
Kufunikwa na msanii mwenye ngoma nyingi za miaka mitatu iliyopita ni sawa na kuelezwa kwamba kwa miaka yote aliyokuwa nje ya muziki hukuweza kufanya ngoma ilizozipita ngoma zake.
Jamani mwacheni Diamond usiku uwe mrefu kwake, yalimfika makubwa jana.
Ova
Kilele cha fiesta siku ya jana tarehe 18 octoba 2014 Tanzania na dunia nzima kwa ujumla imeshuhudia msanii Ally Kiba akioyesha kuwa uchawi hauna nafasi kabisa kwenye muziki baada ya kumkalisha Diamond ambaye siku chache zilizopita alijinadi kupitia Clouds fm kuwa yupo tayari kumsaidia Ally Kiba kufanya nae collabo na sasa kibao kimemgeukia yeye ndiye atakayesaidiwa kufanya collabo.
MASHABIKI: Mashabiki walikuwa hawataki kusikia lolote zaidi ya Ally Kiba. Mashabiki wengine walienda mbali zaidi na kusema bora wasimuone T.I wao wanamtaka Ally Kiba tu.
DIAMOND AZOMEWA KAMA MBWA: kila akiimba mashabiki kila kona ya uwanja walikuwa wakimzomea Diamond huku wakitaka Ally Kiba arudi stejini. Mashabiki wasikika wakisema ''kiba kiba kiba kiba kiba'' huku wakimzomea Diamod ''buuuh buuuh buuuh''
Diamond apata wakati mgumu, Davido na Ney wa Mitego watumika kumbeba Diamond lakini mashabiki hawakuacha kumzomea.
DIAMOND ATAFUTA MCHAWI WAKE: Diamond huku akitapa tapa anahisi amechezewa mchezo na Clouds fm au Ally Kiba eti kwa kile anachokiita mafanikio yake, mashabiki wamjibu ''nani akuchukie wewe? kwa mafanikio yapi? kubadilisha wanawake au kutokumaliza nyumba? kama tunachukia mtu mwenye mafanikio wa kwanza angekuwa Mengi na Bakhresa sio mtu ka wewe''
Alizomewa Kikwete mwaka 2012 pamoja na Yoweri Museven chuo kikuu cha dar es salaam, who is Diamond bwana?
Msanii huyo aliyekulia Tandale na kufanya biashara ya kuuza mitumba na voucher, siku kadhaa zilizopita alinukuliwa na vyombo vya habari kuwa Jiji la Mbeya halina hotel inayoendana na hadhi yake, baadhi ya mashabiki kutoka Mbeya pia waahidi kumzomea siku akienda Mbeya kwani kumuacha ni kumuendekeza ipo siku atasema hajaona hotel ya kulala Tanzania nzima/hajaona chakula cha kula Tanzania na hatimae atasema watanzania wote sio level yake.
Ukweli ni kwamba Diamond kwasasa hapendwi nchini Tanzania, si kwamba ni msanii mbaya ila sababu kubwa ni dharau zake na kiburi. Hivyo aashauriwa aache kusingizia watu. ''Waliomzomea ni watu waliotoka kwao na wakalipa pesa zao''
Nimeamini kuwa ''MBELE YA ALLY KIBA UCHAWI HAUNA NAFASI''
nasikilizaa hapa Chuki ni bure by Sharo millionea