Ni ukweli kuwa Ally alikuwa juu sana kuanzia 2007-2010....baada ya Dimond kuja na kuteka soko la Muziki huku akiwazima watu kama taa ally kiba alipotea kwa kasi ya kimbunga kabla ya kuanza kupanda juu kwa kutumia upepo wa Dimond...
Naposema upepo wa Dimond namaanisha kama ally kiba angekuwa na bifu na wasanii wengine kama Barnaba, Belle 9 asingepata kick hii anayoipata kutoka kwa watu ambao wengi wao wanamchukia Dimond for fun , Wengine sio hata mashabiki wa ally kiba..
Napenda kumpa sifa kijana ally kiba kwa kutumia nafasi hii vizuri na pia ameonyesha kubadilika katika sekta zifuatazo..
1. Mavazi, Before ally alikuwa anavaa tu ilimradi amevaa ila sasa amebadilika anapiga mavazi mazuri sana na anapendeza
2. Perfomance.. Kabla ya ujio na mapinduzi ya Dimond kiba alikuwa hatumii sana dancers pia alikiba alikuwa hajishughulishi na masuala ya kucheza na kuimba kwa pamoja kitu ambacho kilikuwa kinamnyima maxi miongoni mwa macho ya wapenda Burudani..
All and all nampa sifa Dimond kwa kumuathiri ally kiba Positively maana pengine bila Dimond ""ally kiba"" angeendlea kutuimbia nakshinakshi zake huku akiwa kavaa vibaya ni mapinduzi ya Dimond yaliyombadilisha ally kiba..
Pia Dimond asikate tamaa kwaajili ya wale wanywa viroba wa jana waliokuja kupiga buuuu...aendelee kufanya muziki mzuri na siku nyingine asipige shoo za viingilio vya mbuzi kama ya jana maana huwa zinajaa wahuni ambao hawana maana, kama wanampenda kiba mwambieni kiba aanze kupiga shoo za 50000 tuone kama wataenda..
#Muzikimzuridaima