Uchunguzi ufanyike
Inawezekana hata Magufuli hakuwa na details
Za yote yaliyo endelea chini yake
QUOTE="The Boss, post: 38702245, member: 18247"]
Uchunguzi ufanyike
Inawezekana hata Magufuli hakuwa na details
Za yote yaliyo endelea chini yake
[/QUOTE]
Lengo la huo uchunguzi Ni Nini?
- kupata ukweli Kama Magufuli anahusika ama hahusiki na uharamia huo?
- kumtenganisha Magufuli na uharamia huo?
-kujua Kama Mbowe Kadanganya?
-kujua Kama TRA wamesingiziwa?
Mbowe kaishasema Sasa sheria ichukue Mkondo wake.
Lakini Kama Magufuli hahusiki je Ni raia wangapi wameteswa na Amiri jeshi mkuu katika nchi hajui.
Kuna Mambo mengine hayahitaji uchunguzi wala ushahidi.
Je ilikua Ni lazima na muhimu Sana kuvunja Club Bilicanas?
Je Magufuli pia hakujua Bilicanas inataka kubomolewa na Kisha ikabomolewa?
Je ilikua muhimu Sana kuvuruga mashamba ya mbogamboga ya Mbowe?
Je Magufuli pia hakujua Mashamba ya Mbowe yameharibiwa?
Mbowe Ni mtu mkubwa Sana hapa Tanzania( KUB) ,mbunge na Mwenyekiti wa chama kikubwa Sana Cha Upinzani hapa nchi.
Je Magufuli hakujua pia Mbowe Ameenda nje kutibiwa?
Je Magufuli pia hakujua Mbowe Yuko jela?
Je TRA inaweza kuwa na wataalam vilaza namna hiyo kumbambikia Kodi kubwa zaidi ya uwezo wa Mfanyabiashara?
Kama Ni hivyo Magufuli pia hajui uwezo wa wataalamu wa kufanya tax assessment wa Tanzania?
Usalama wa wawekezaji ukoje.
Tuwe waungwana kufanya uchunguzi Ni matumizi mabaya ya fedha za walipakodi.
Kila kitu kiko wazi.
Ukimuona mbwa juu ya mti ujue Kuna mtu kamuweka.