Jinsi gani Mkapa nimfikishe The Hague?

MchunguZI

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2008
Posts
4,011
Reaction score
2,185
Ningependa asiwe BASHIR PEKE YAKE. Nataka kumfikisha Rais Mstaafu B.W. Mkapa wa Tanzania pamoja na washirika wake ktk mahakama ya Dunia kwa mauaji ya Pemba.

Nadhani nahitaji msaada wa wanasheria. Je, kabla Luis Moreno-Ocampo hajayaona makosa ya mtu au kiongozi kama huyu na makosa yake, ni jinsi gani naweza kuyapeleka kwenye hii Mahakama inayoitwa ya Dunia?


Nataka nifanye hivyo kabla ya uchaguzi ujao wa 2010 ili hata huyu wa sasa asifanye hivyo.
 

Ukitaka mambo yende haraka Mshitaki katika Mahakama ya BELGIUM kule wakitowa waranti inamaana wanaweza kumtia mikononi katika anga yoyote ya kule ulaya kwa hiyo itambidi mzee safari za mataibabu zimalizikie huku huku ulimwengu wa 3
 
Mtafute De Campo wa ubeligiji ndio mtaalamu. Ameshatoa waranti ya Al Bashir. Nafikiri anaweza kukusaidia
 

I hope you'll find this info useful
 
nyinyi ndiyo sampuli ya wale aliosema rais kikwete-mmekula ugali na maharage mmeshiba...
 
Kesi ya Nkapa ipo katika hatua za mwisho na si peke yake wamo na viongozi wengine ambao walikuwepo maofisa wa polisi wakuu wa mikoa ,ni jalada ambalo litaitikisa Tanzania na kuivua nguo kutokana kujivalisha koti la ngozi ya kondoo kuwa ni Nchi ya amani ,hapo ndio itakapojulikana wazi kuwa walio na amani ni wananchi na sio viongozi.
Kwa ufupi ilitakiwa ionekane Tanzania ni nchi ya wananchi wapenda amani ila viongozi wake ni devils waovu ,vampires ambao wanakunywa damu za wananchi ili CCM ibakie madarakani milele ,hakuna shaka yeyote ile katika kumfikisha Mkapa mahakamani ,ikiwa hapa wanamlinda na wanasema aachwe apumzike.Mwacheni msimkurupushe akaja akaingia mitini.
 
Ndege katulia tunduni nyie mnaanza kumkurupusha!
 

Hii mahakama ya Dunia ni kwa maslahi ya nani? manake wanaoshtakiwa wengi ni watu weusi tu! kwanini? Bush Mtoto na Washirika wake hasa Tony "the Blair", Na yule Makamu wake wa Rais Dick Cheney na Donald Rumsfield Aliyekuwa waziri wake wa ulinzi kabla ya Gates na wao washitakiwe kwa
1.Kuisambaratisha Iraq
2.Kuua watu bila Hatia hasa wakina mama na watoto kule Iraq
3.Kumpindua na kumnyonga Sadam Hussein(Rais!!!!!)
Kama hiyo mahakama ni kwa maslahi ya Dunia.
 
Last edited:
MKOKOTE BABAA... Na yeye akanyee kidebe
 
Jamani sasa kama BWM tunasema tumfikishe The Hague- sii bora tu ashitakiwe hapa hapa?

Basi ukisema hivyo maraisi wengi wastaafu itabidi wapelekwe huko yaani akina Muluzi, Moi, Chilluba n.k

BWM ashitakiwe tu hapa hapa kwetu!
 
nyinyi ndiyo sampuli ya wale aliosema rais kikwete-mmekula ugali na maharage mmeshiba...

Eeeh! we naona unajaribu kum-quote kila mtu. Jaribu ku-quote watu ambao ni itellectual!

Nadhani mi nimeshapata pa kuanzia. Maana labda viburi vyao vitapungua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…